political monger senior
JF-Expert Member
- Nov 26, 2020
- 1,827
- 5,994
Nchi ya ajabu sana hii
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Majirani zetu wanatumia bandari zetu wanatumia magari ya kuanzia 2015 and above. Sisi tunagangana na Carina ya 1999 na inauzwa milioni 20 just amagine!!Tunatumia nguvu kubwa sana ku survive! Yaani hata vitu vinavyo pitia hapa kwenda nchi jirani ni rahisi kuliko vinavyofikia hapa
Yaani inafikirisha sana! Kuna gari hapa bongo tunaogopa kumiliki ila zambia zipo na watu wanadunda nazo kama kawaida! Huko kongo tu balaa!Majirani zetu wanatumia bandari zetu wanatumia magari ya kuanzia 2015 and above. Sisi tunagangana na Carina ya 1999 na inauzwa milioni 20 just amagine!!
Tugome sote.
Na ina maajabu mengi sanaNchi ya ajabu sana hii
Ongezea na mafanikio ya wasaniiYanga / Simba ikitwaa ligi na kushiriki caf mawazo yanayeyuka.
vijana wakifika vileleni kwao washamaliza maisha.
Mkuu usiwalaum sana wasomi ukjikuta mjuaje wanaoanguka papai kwa kutumia gobole au huenda wasomi unao wasemea wanafaidika kwa kupitia izo tozo na kodHii nchi ina wasomi wengi wajinga wajinga sana.
Ndio maana kuwa kiongozi wa TRA hata felia wa kidato cha NNE anaweza tu.
Kuwa meneja wa Tanessco hata darasa LA saba anaweza tu,kuwa waziri wa fedha,hata mtu yeyote anayejua tu kiingereza cha kuingea na wazungu anaweza.Kwani ni kuongeza kodi,maji yakipungua kata umeme,wabunge wakihoji matumizi mabovu,wajibu kwa kiingereza tu hata kama wewe hukijui pia Trab na Trat
Wanashida sana wale zinawabana ndio maana wanaanza kupata akili. Sisi tupo comfortable sana.Unakuja kukuta asilimia 70 ya watanzania hawapo aware na hivi vitu na kibaya zaidi unakuta hawajali!..
Hivi wakenya na sisi tuna tofauti gani mbona wenzetu raia wao wapo smart sana vichwani mwao!!? Sisi huwa tunakwama wapi?
Yaani inafikirisha sana! Kuna gari hapa bongo tunaogopa kumiliki ila zambia zipo na watu wanadunda nazo kama kawaida! Huko kongo tu balaa!
Hata bidhaa zingine na zinapitia hapa hapa kwetu ila huko kwao ninafuu sana
Halafu hii VAT sasa si inakuwa kama double taxation maana navyojuwa VAT ni pale bidhaa inavyonunuliwa kwa mtu wa mwisho, na hili sio shida ya TRA ni ya wale waliopanga haya nakutunga sheria maana mfanyakazi wa TRA anachoweza kucheza nacho ni yale makadirio tu lakini akiweka number makato yote yanakuja na hii ndio shida nyingine kwenye makadirio, pamoja na haya yote kodi ni kubwa sana tena sana bado sijui kodi za manispaa sijui halmashauri sijui mazingira sijui usalama hapo takataka yaani mambo ni mengi kweli ukija huko kwenye mafuta unawakuta mpaka EWURA wa nini wakati wanalipwa mishahara na serikali muhimu ni vichaka vya kukusanya tu yaani ni balaa kama unafanya biashara halali utoboi ni lazima na wewe ujiongeze ndio haya ya rushwa na kukwepa kuna mfanya biashara wa mafuta alisema bila kujiongeza hutoboi lazima gari mbili halali moja haramu vinginevyo utafunga kituo na hawa wafanya biashara contoiner 2 halali moja pitisha tu maana ndio faida yao vinginevyo watafunga biashara tu. Mwigulu na team yake ni janga sheria za kodi ni lazima zipitiwe na makato yote isizidi 25% ya gharama ya mzigo itachochea biashara kwa wingi na pia kuongeza biashara kukua na kujenga matajiri wengi maana ni afya kwa nchi, kuwa na watu maskini hawakui ni kudumaza nchi pia. Nitatoa mfano mdogo huko nje mfano Voda wanakupa simu mpya Iphone ila sharti simu ile inakuwa lock inatumia line ya voda kwa miaka miwili matokeo Iphone wanauza sana na voda wanapata sana huku kwetu hata vitu vidogo kama hivi tu tunashindwa kuna wale Azam badala ya kutoa bure ving'amuzi ili waongeze watumiaji na wao wanufaike na virushi baada ya muda inawalipa gharama zote na wateja wamekamata lakini wanauza kitu bei kubwa warudishe gharama siku moja, natoa mifano hii ndio serikali badala ya kuweka kodi ndogo ili volume ya biashara iwe kubwa na kuvutia na kukua na siku za mbeleni watakusanya mapato kama haya lakini kubwa wananchi kuwa na maisha bora maana ndio lengo. wamechemka kwenye tozo za simu wamepunguza watumiaji badala ya kutanua wigo kwa matokeo yasiokuwa chanya ukuaji mdogo kwa faida za muda mfupi.
Hiyo kazi unayoitaka ni rahisi.Mbona hamuweki wazi huko inje hzo bidhaa mnanunua kwa bei gani? Wekeni wazi.... serikali wanajua ndo maana wanafanya hvo kwani hyo Sheria ya tax imeanza leo si ilikuwepo toka enzi za....
Wale wanachajiwa PORT CHARGES TU na kwa muda maalum na muda huo ukiisha ndio kunakua na ishu za STORAGE hivyo maswala yao mengine yakiKODI yanaenda kuendelea mpakani ambapo kimsingi ndio BANDARI zao mf: mizigo ya zambia bandari yao ni pale TUNDUMA/ NAKONDE, na mizigo ya kongo bandari yao ni KASUMBALESA hivyo huko zambia inapita tu wanalipi njia tu! Hivyo kinachoenda kuleta urahisi kwao no sera zao za kikodi ambazo zina utofauti kidogo na hapaKwani wageni wanachajiwa cost tofauti na sisi pale bandarini?
18% sio pesa ya mfanyabiashara anayotakiwa kuilipa TRA bali Mfanyabiashara ni wakala tu wa kuikusanya na kimsingi haimuumizi kivyovyote mfanyabiashara! Hapa ndipo ambapo watu wanajichanganyaVAT hatozwi mlipakodi.
Ni kodi anayolipa mlaji wa mwisho wa bidhaa au huduma.
Inahitajika elimu uweze kuelewa.
Mfanyabiashara ni wakala wa kukusanya na kuipeleka TRA hivyo tu.
Hata kodi ya ajira PAYE si ya mwajiri bali mfanyakazi ndiye anyekatwa .
Mwajiri ni wakala wa kuikata na kuipeleka serikalini (TRA).
Nadhani ungesoma nimeandika nini kabla hujajibu, nimesema VAT ni mtu wa mwisho sasa nani mtu wa mwisho? Mlaji ndio analipa VAT rudia kusoma tena nilishoandikaVAT hatozwi mlipakodi.
Ni kodi anayolipa mlaji wa mwisho wa bidhaa au huduma.
Inahitajika elimu uweze kuelewa.
Mfanyabiashara ni wakala wa kukusanya na kuipeleka TRA hivyo tu.
Hata kodi ya ajira PAYE si ya mwajiri bali mfanyakazi ndiye anyekatwa .
Mwajiri ni wakala wa kuikata na kuipeleka serikalini (TRA).