Tozo za Miamala: Serikali yapunguza viwango kwa 30%. Watoa huduma za simu waridhia kupunguza 10%
Tulishahamia kwenye mabenk kutoka huko sio rahisi lbda hela ya mboga huko vijijini ambako bank inko 80km
 
Hivi yule wakili aliyefungua kesi kupinga tozo aliishapatikana?
 
ni ujinga kwani VAT iliwekwa kwa ajili ya nini ndio tabu ya kuwepa watu uongozi kwa kuangalia makaratasi yao kumbe weupe kichwani.
 
Yatakuja na masuti yao kusema "serikali ya fulani fulani ni sikivu,imeona tuwapunguzie wananchi huu mzigo" wakati wao wenyewe Ndo waliouleta huo mzigo in the first place[emoji38]
Na lile limama litayang'ong'a
 
Kwanini wanang'ang'ania tozo wazitoe tuu tuishi km zamani. Hiyo mitandao ilikuwa unasaidia sana maskini kule msalezi mang'ula bibi yangu nikimtumia teni tuuu anamaliza shida zake. Sasa imekuwa tabu sana turudi kwenye mpango wa zamani
 
Nimetoka sasa hivi kwa wakala nikiwa na azma ya kutuma pesa, nimemuuliza miamala mipya tayari? Kanijibu bado. Nimeghairi kutuma pesa.
 
Nimetoka sasa hivi kwa wakala nikiwa na azma ya kutuma pesa, nimemuuliza miamala mipya tayari? Kanijibu bado. Nimeghairi kutuma pesa.

Sijatuma wala kutaka kupokea muamala tangia madilu systeme aje na yake.

Ninasali Mungu anijalie nisijikute kwenye ulazima wa kutuma au kupokea muamala. Hadi sasa ninamshukuru sana bwana wa Majeshi aliyetufanyia wepesi mapema 2021.

Kwa hakika mwenye tozo achukue tu ushauri wa mzee baba wa kubakia na m@fi yake.

Hakuna miamala hapa.
 
Bado mzee,huwa natumiwa pesa kilasiku ya kijimradi changu uchwara,nimetoa naona nakatwa vilevile.
 
Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba amesaini marekebisho ya Kanuni za Tozo za Miamala ya kutuma na kutoa Fedha na kupunguza viwango vya tozo kwa 30%

Pia Serikali imejadiliana na watoa huduma za simu ambao nao wameridhia kupunguza viwango vya tozo wanazotoza kati ya mtandao na mtandao mwingine kwa 10%

Viwango vilivyopunguzwa vitatangazwa rasmi Septemba 01, 2021

Taarifa Kamili:

Huo bado ni wizi wa mchana kweupe. Huwezi kulipa kodi mara mbili, hivi hii Serikali haioni aibu! Mfanyakazi anapotuma pesa kwa ndugu au rafiki anakuwa ameshalipa pay as you earn.
 
Hivi tungekuwa hatuna madini, Bandari, Maziwa, Bahari, Nchi kubwa yenye Rutuba tungeishi vipi ?

Kipindi kile tuliacha madini kuyachimba kwanza tupate akili..., sasa hivi tunayachimba kila kona, makodi mengi zaidi ya Kodi ya Kichwa, huduma hakuna tena tunagharamia wenyewe kuanzia Afya, Elimu n.k. Sasa hayo makusanyo ambayo hatuoni Value for Money yanafanya nini ? Wakulima wanalima mpaka wabembeleze watu kununua eti hakuna wanunuzi, wakati town watu wanalia njaa kula milo mitatu ishakuwa Anasa....

Something is Very Wrong Somewhere.....
 
Mmmh alitegundua tozo katuua watanzania
Wacha hizo! Changieni maendeleo yenu! Katuua NINI!? Unadhani hao Wajapani au Waingereza au Wamarekani au Wachina wanao tuletea huku misaada, hizo pesa wanatoa wapi, kama SI KWENYE KODI WALIPAZO KAMA HIZI!? Unadhani wana zitungua MITINI?!
 
Back
Top Bottom