Tozo zinaweza kugeuka na kuwa wizi wa dola dhidi ya Wananchi

Tozo zinaweza kugeuka na kuwa wizi wa dola dhidi ya Wananchi

Loans mnazochukua left right zinafanyia nini?mnatuibia period
Kwa hiyo Chadomo mkiongoza Nchi hautachukua loan? 😁😁.

Kuna Nchi haichukui loan Dunia hii?

Nakupa mfano mdogo,Tzn ina jumla ya km za barabara za TanRoads na Tarura zaidi ya 160,000 Kati ya hizo lami ni km 12,000 tuu Sasa tukisema tuende kwa Kasi hii ya kujenga km 600 za lami kwa mwaka sasa unategemea hizo barabara zitafikiwa lini?

Sasa iko hivyo across sectors na mahitaji yanazidi kuongezeka kwa sababu ya ongezeko la watu so loan zinasaidia kupunguza makali ya Kodi in short term na pia kutatua shida za dharura.
 
Wewe ndio mpumbavu kwa kujenga hoja Kwa kufanya reference ya Waziri unaemtaja..

Tuambie basi wewe hizi tozo ni Kwa ajili gani Ili na mimi nikuwekee ushahidi wa nachosema..

Mwisho CCM kushindwa miaka mingine haimaanishi itashindwa na leo,Leo Rais ni Mwanamama na miaka hiyo Marais walikuwa Wanaume ambao kwa hulka huwa ni wezi..

Nasisitiza Rais Samia ataweza hayo ndio maana mwaka mmja tuu kajenga vituo vya afya 252,taja Rais mwingine aliyewahi weza?

Rais Samia Ataweza ndio maana mwaka mmja huu kahamisha bajeti ya barabara Vijijini kutoka bil.252 hadi bil.802 Ili kutimiza hiyo azma..

Rais Samia ataweza ndio maana kwa mwaka mmja Katia bajeti ya Maji kutoka bil.334 hadi bil.787 na maelfu ya miradi inaendelea..

Hivyo hivyo na sekta zingine zote kama kilimo nk..So Usilete ujinga wa kujenga hoja yako kwa failures.
Hapana, bado wewe ni mpumbavu tu...!!

Kwa kuwa unataka kununua gari nyumbani kwako, ina maana utauza chakula cha watoto wako na nyumba yako ili ukanunue gari...?

Kwani kununua gari ni jambo baya? La, hasha!

Bali mtu huyu anatumia njia yenye madhara kwake mwenyewe kujipatia kitu chema vilevile...

Ndivyo zilivyo fikra zako wewe..

Na huu ndiyo utetezi wako. Kwamba, it's okay kwa serikali kuwanyang'anya watu vya kwao hata baada ya kuwa imeshalipwa cha kwake inachostahili. Huu ni wizi..

Sasa kwa kuwa wewe huyatafakari vyema mambo haya na umeamua uwe mjinga kwa sababu una uelewa wa upande mmoja (one way traffic understanding), kwamba ni LAZIMA KILA MTU ALIPE KODI lakini hutaki kujiuliza kodi zipi na kwa namna gani...

Hawa hawatafuti kodi hizi kwa maendeleo yetu kwa sababu kwa miaka 60 tangu uhuru wameshakusanya kodi nyingi sana lakini kilichofanywa na kodi hizi hakifanani kabisa...

Ndo kusema kubwa, wanakusanya TOZO HIZI ZA KIWIZIWIZI ili hawa watu CCM ambao ni highly privileged tayari, wagharamie gharama ya kubaki kwenye mamlaka na madaraka yao ya kiserikali na pia kutumia kwenye anasa zao...

Narudia tena kukuambia kwamba, kama unadhani kwa miaka hii miwili hawa nduguzo watakujengea barabara au watakuletea maji kila kijiji, basi wewe The Sunk Cost Fallacy ni mjinga na mpumbavu wa kiwango cha juu kabisa...!!
 
Tozo ni Kodi ya uzalendo yenye malengo mahsusi na Wala haiendi TRA..

VAT ni Kodi ya value addition kwa hiyo huduma..
Uzalendo wakulazimishana,,sisi tunaokatwa tunaona tunaibiwa maana kama kuchangia maendeleo tunachangia sana hakuna haja ya kulipishwa tozo pasi na hiari yetu,

Kibaya zaidi watu wanafanya manunuzi kitu cha millioni 10 kinanunuliwa millioni 100,,sasa hapo unatuaminishaje kwamba kodi nq tozo zinatumika vizuri?
 
Uzalendo wakulazimishana,,sisi tunaokatwa tunaona tunaibiwa maana kama kuchangia maendeleo tunachangia sana hakuna haja ya kulipishwa tozo pasi na hiari yetu,

Kibaya zaidi watu wanafanya manunuzi kitu cha millioni 10 kinanunuliwa millioni 100,,sasa hapo unatuaminishaje kwamba kodi nq tozo zinatumika vizuri?
Kazi ya Serikali sio kubembeleza watu wasioelewa..
 
Anakata tozo kwenda kumlipa Dario kule SBS.
Usione mtu anavaa tai ya bendera ya Taifa ukafikiri ni mzalendo kindaki ndaki.
 
tozo ni wizi 100%. Wamebadili jina tu kuita tozo lakini ukweli ni kodi. Huwezi ukamkata mtu kodi kwa sababu tu anachukua pesa zake benki. Na wakati huo huo alipolipwa pesa hiyo alikatwa kodi. Mfumo huu ni wizi uliokubuhu
 
Msingi wa kodi, tozo au ushuru ni mapato. Kutokana na mapato uliyoyaingiza, sehemu ya hayo mapato, wewe uliyeingiza unastahili kutoa sehemu ya hayo mapato kama kodi, ushuru, tozo au jina jingine lolote utakalopenda kuita lenye lengo la makato yanayyoenda kwenye mamlaka za Serikali. Hii ni kanuni mama ya kodi.

Kanuni kuu ya pili, mapato yalikwishalipiwa kodi, tozo au ushuru hayastahili kulipishwa tena kwa mara ya pili. Double taxation inazuiwa.

Wizi ni kuchukua kitu chochote ambacho siyo stahili yako. Wizi huu unaweza kuwa wa mtu mmoja dhidi ya Serikali, taasisi, mtu mwingine au kikundi au Serikali dhidi ya wananchi wake au dhidi ya mwananchi mmoja.

Serikali inapomtoza mwananchi kodi zaidi ya kiwango halali au zaidi ya mara moja kwa mapato yale yale, huo ni wizi wa dola dhidi ya mwananchi.

Maswali muhimu ya kujiuliza:

1) Kwa mfano, mfanyakazi au mfanyabiashara amepata mshahara au pesa ya mauzo, ameilipua kodi tayari, ikawekwa benki, benk amelipia gharama ya huduma, na benki inalipa kodi kwa mapato yanayotokana na utoaji huduma, huyu mteja anapotaka kuichukua pesa yake, akatozwa tena na Serikali, ni mapato gani ameyapata kule benki?

2) Kwa mfano, mfanyakazi, kwenye mshahara wake amekatwa PAYE, pesa imeenda benki, anatoa kwenye ATM, anakatwa kodi kwa mara ya pili, anaweka kwenye simu, pesa ile ile anaituma kwa mama yake kijijini anakatwa kodi, mama yake anaenda kwa wakala kuchukua ile pesa, anakatwa kodi.

Pesa siyo chakula, lazima huyu mama ataitumia, anaenda kununua chumvi anakatwa kodi. Yaani makato mara 5 kwa mapato yale yale, hii ni halali? Lakini ikumbukwe kwamba, benki kutokana na mapato yake yanayotokana na utoaji huduma imekatwa kodi, mtandao wa simu kutokana na mapato ya utoaji huduma ya usafirishaji fedha, nao umekatwa kodi, na muuzaji wa chumvi naye amekatwa kodi.

Tax regime ya Tanzania ni lazima iangaliwe upya. Siyo regime rafiki kwa wananchi wala wawekezaji.

Siku zote kodi utitiri au kubwa huua uwekezaji. Hakuna nchi hata moja Duniani iliyokuwa maskini ambayo iligeuka kuwa tajiri kwa haraka kwa kuwa na kodi utititiri au kodi kubwa.

Dubai, ilipata maendeleo makubwa, na kubadilika kabisa ndani ya miaka 15 tu kwa kufuta kabisa kodi nyingi na kubakia na kodi chache sana. Mpaka leo Dubai ni kituo cha biashara Duniani.

Anayehamasisha Tanzania kuwa na kodi utitiri na kodi kubwa ni adui mkubwa wa maendeleo ya nchi yetu.

Nchi hii inahitaji sana uwekezaji ili watu wetu wapate ajira, na Serikali iwe na vyanzo vingi vya mapato, na siyo kuongeza kodi kwa vyanzo vile vile.

Wazalendo wa nchi hii, wanaoitakia mema Tanzania tukatae mambo yote yanayoua uwekezaji katika Taifa letu.

Tukiwa na sera na sheria ambayo inachochea uwekezaji kivitendo, kama uwekezaji utasababisha japo watanzania milioni 15 kupata ajira za uhakika, na hao milioni 15 angalao kila mmoja kwa wastani akalipa kodi ya sh milioni 4 kwa mwaka, PAYE pekee yake itaipatia Serikali 4,000,000×15,000,000 = 60,000,000,000,000 (trillion 60).

Haya ni mapato ambayo ni karibu 50% ya makusanyo ya Serikali kwa sasa. Na haya ni mapato ambayo Serikali itayapata, na huku mlipa kodi akifurahi kwa kuwa ana ajira inayompa kipato cha uhakika.
Kinara wa huu wizi ni Mwigulu na ashasema asiyetaka ahamie Burundi..
Na kwa mtindo huu wataumiza mabenki.
 
Kumbe kuna mchango wa lazima?
Maendeleo ni lazima.sio hiari,wazazi wetu walikuwa wanatandikwa bakora kwa kutoenda kwenye maendeleo na kutoa pesa za Kodi ya kichwa na michango mingine..

Watu wamebomolewa nyumba zao kupisha ujenzi wa barabara nk ,hiyo ndio cost ya maendeleo ni lazima sio hiari maana bila hivi utadai huduma.
 
Njia nazo Ni Hali maana zilipitia michakato ya kisheria pia, Tuwe wazalendo tuijenge nchi yetu
Yeah chochote ukihalalisha kinakuwa halali, uzalendo unauhimiza kwa wananchi tu wanaoathirika na hizo tozo ila hao viongozi wanaolipwa mishahara mizuri na kuishi vizuri kwa gharama za hizi tozo zetu wewe huna cha kuwahimiza uzalendo.
 
Back
Top Bottom