Tozo zinaweza kugeuka na kuwa wizi wa dola dhidi ya Wananchi

Kodi au tozo haziwahi kuwa wizi ndio maana nilikuuliza kama ni wizi hizi pesa zinaenda kutumika wapi? Hukujibu..pesa inatumika kuboresha huduma mbalimbali kama hizi 👇
Loans mnazochukua left right zinafanyia nini?mnatuibia period
 
Loans mnazochukua left right zinafanyia nini?mnatuibia period
Kwa hiyo Chadomo mkiongoza Nchi hautachukua loan? 😁😁.

Kuna Nchi haichukui loan Dunia hii?

Nakupa mfano mdogo,Tzn ina jumla ya km za barabara za TanRoads na Tarura zaidi ya 160,000 Kati ya hizo lami ni km 12,000 tuu Sasa tukisema tuende kwa Kasi hii ya kujenga km 600 za lami kwa mwaka sasa unategemea hizo barabara zitafikiwa lini?

Sasa iko hivyo across sectors na mahitaji yanazidi kuongezeka kwa sababu ya ongezeko la watu so loan zinasaidia kupunguza makali ya Kodi in short term na pia kutatua shida za dharura.
 
Hapana, bado wewe ni mpumbavu tu...!!

Kwa kuwa unataka kununua gari nyumbani kwako, ina maana utauza chakula cha watoto wako na nyumba yako ili ukanunue gari...?

Kwani kununua gari ni jambo baya? La, hasha!

Bali mtu huyu anatumia njia yenye madhara kwake mwenyewe kujipatia kitu chema vilevile...

Ndivyo zilivyo fikra zako wewe..

Na huu ndiyo utetezi wako. Kwamba, it's okay kwa serikali kuwanyang'anya watu vya kwao hata baada ya kuwa imeshalipwa cha kwake inachostahili. Huu ni wizi..

Sasa kwa kuwa wewe huyatafakari vyema mambo haya na umeamua uwe mjinga kwa sababu una uelewa wa upande mmoja (one way traffic understanding), kwamba ni LAZIMA KILA MTU ALIPE KODI lakini hutaki kujiuliza kodi zipi na kwa namna gani...

Hawa hawatafuti kodi hizi kwa maendeleo yetu kwa sababu kwa miaka 60 tangu uhuru wameshakusanya kodi nyingi sana lakini kilichofanywa na kodi hizi hakifanani kabisa...

Ndo kusema kubwa, wanakusanya TOZO HIZI ZA KIWIZIWIZI ili hawa watu CCM ambao ni highly privileged tayari, wagharamie gharama ya kubaki kwenye mamlaka na madaraka yao ya kiserikali na pia kutumia kwenye anasa zao...

Narudia tena kukuambia kwamba, kama unadhani kwa miaka hii miwili hawa nduguzo watakujengea barabara au watakuletea maji kila kijiji, basi wewe The Sunk Cost Fallacy ni mjinga na mpumbavu wa kiwango cha juu kabisa...!!
 
Tozo ni Kodi ya uzalendo yenye malengo mahsusi na Wala haiendi TRA..

VAT ni Kodi ya value addition kwa hiyo huduma..
Uzalendo wakulazimishana,,sisi tunaokatwa tunaona tunaibiwa maana kama kuchangia maendeleo tunachangia sana hakuna haja ya kulipishwa tozo pasi na hiari yetu,

Kibaya zaidi watu wanafanya manunuzi kitu cha millioni 10 kinanunuliwa millioni 100,,sasa hapo unatuaminishaje kwamba kodi nq tozo zinatumika vizuri?
 
Kazi ya Serikali sio kubembeleza watu wasioelewa..
 
Anakata tozo kwenda kumlipa Dario kule SBS.
Usione mtu anavaa tai ya bendera ya Taifa ukafikiri ni mzalendo kindaki ndaki.
 
tozo ni wizi 100%. Wamebadili jina tu kuita tozo lakini ukweli ni kodi. Huwezi ukamkata mtu kodi kwa sababu tu anachukua pesa zake benki. Na wakati huo huo alipolipwa pesa hiyo alikatwa kodi. Mfumo huu ni wizi uliokubuhu
 
Kinara wa huu wizi ni Mwigulu na ashasema asiyetaka ahamie Burundi..
Na kwa mtindo huu wataumiza mabenki.
 
Kumbe kuna mchango wa lazima?
Maendeleo ni lazima.sio hiari,wazazi wetu walikuwa wanatandikwa bakora kwa kutoenda kwenye maendeleo na kutoa pesa za Kodi ya kichwa na michango mingine..

Watu wamebomolewa nyumba zao kupisha ujenzi wa barabara nk ,hiyo ndio cost ya maendeleo ni lazima sio hiari maana bila hivi utadai huduma.
 
Njia nazo Ni Hali maana zilipitia michakato ya kisheria pia, Tuwe wazalendo tuijenge nchi yetu
Yeah chochote ukihalalisha kinakuwa halali, uzalendo unauhimiza kwa wananchi tu wanaoathirika na hizo tozo ila hao viongozi wanaolipwa mishahara mizuri na kuishi vizuri kwa gharama za hizi tozo zetu wewe huna cha kuwahimiza uzalendo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…