Tozo zinaweza kugeuka na kuwa wizi wa dola dhidi ya Wananchi

Yeah chochote ukihalalisha kinakuwa halali, uzalendo unauhimiza kwa wananchi tu wanaoathirika na hizo tozo ila hao viongozi wanaolipwa mishahara mizuri na kuishi vizuri kwa gharama za hizi tozo zetu wewe huna cha kuwahimiza uzalendo.
Nimewahimiza Sana juu ya usimamaizi mzuri wa pesa za umma, nimewahimiza na kuwashauri Kama mwananchi na kijana wa kitanzania kuwa waziogope pesa za umma Kama ukoma, wasiziguse na kuzitumia kwa maslahi yao binafsi
 
Unapotunza pesa bank harafu unakatwa unakuwa umezalisha nini?
Unajua wewe The Sunk Cost Fallacy unahitaji kuelimishwa tu ili kukamua ujinga wako huo...

Unapaswa kuelewa taxation cycle inavyokwenda. Serikali haiwezi tu kunyang'anya watu fedha zao eti kwa sababu imewaona wana fedha. This is stupidity of high quality...!

1. MOSI; Fedha inapokuwa benki, maana yake imezalishwa huko na serikali imeshachukua kila chake kwa mujibu wa sheria..

E.g mshahara wa mtu. Si utakuwa umekatiwa PAYE?. Au mauzo ya mfanyabiashara fulani. Je anakuwa hajakatwa kodi mbalimbali..? Sasa kwanini serikali izifuate pesa hizo hizo benki ili kutaka kodi tena?? Ndugu The Sunk Cost Fallacy unaweza kuwa honest ingalau kwa dakika moja ili ujibu swali hili kwa usahihi...?

2. MBILI; Mimi ninapopeleka pesa benki, ni kwa ajili kutunziwa na ofcoz at first place nakuwa najua kuwa, nitakwenda kulipa gharama ya kutunziwa. Kwa hiyo ni haki nilipe gharama hiyo. Hii kwa ajili ya benki. Maana yake benki inaingiza kipato...

3. TATU; Kumbuka pia benki naye ni tax payer. Analipa kodi na tozo kutoka kwenye mapato ya faida anayokusanya kutoka kwa wateja....

4 NNE; Serikali haipaswi kuingia benki kwa watu walewale wa mlango wa nyuma kudai tena kodi toka kwa pesa ileile ambayo imekwisha kulipiwa kodi lakini mtu ameipeleka benki tu ili kutunza...

Serikali inatakiwa kuitoza benki hiyo kodi na si wateja tena...!!
 
Kodi au tozo haziwahi kuwa wizi ndio maana nilikuuliza kama ni wizi hizi pesa zinaenda kutumika wapi? Hukujibu..pesa inatumika kuboresha huduma mbalimbali kama hizi 👇
What rubbish! Kumbe ndio maana wengi wa mamilionea wanaotuhumiwa kwa wizi hukimbilia kuichangia CCM na hivyo kujitakasa!

Wizi ni wizi, hata ukiitwa tozo ni wizi tu. Hakuna wizi mbaya kama wizi wa kidola...kwamba
serikali inatafuta njia ya kuwaibia wananchi wake, kweli!

Ingawa CCM imejengwa kwenye misingi ya rushwa na wizi, sikujua watakuja na sera ya kuwaibia wananchi wa Tanzania kupitia hiyo inayoitwa tozo!

Tozo ni wizi, hakuna serikali hapa duniani inaweza kutafuta hela kwa kubariki wizi kwa njia tunazozishuhudia zikitendeka hapa kwetu Tanzania, hakuna!

Cha ajabu sasa, wananchi wametulia kama kondoo wanaopelekwa machinjoni. Taasisi zetu nyingi zinaongozwa na vijana waliozaliwa na kukulia ndani ya CCM!

Wengi wana tuhuma za wizi toka utotoni...ama waliiba majina, waliiba mitihani, waliiba vyeti na yawezekana wengine wametumika katika wizi wa kura!

Hapana, umefika wakati wa kuita wizi kwa jina lake halisi na si kuipamba kwa majina ya ajabu ajabu.

You can put lipstick on a pig, it is still a pig, fullstop!
 
Tozo ni malipo ya uzalendo Wala haiitwi Kodi..

Wazazi wetu walichapwa bakora kuchangia maendeleo by physical na Kwa kutoa Kodi na michango mbalimbali..

Watu wamebomolewa majumba yao tena wengine bila fidia kwa ajili ya maendeleo.

Hatuna wajomba wa kutuletea maendeleo zaidi ya kujichanga wenyewe..

Utaumia in short run ila uta enjoy maisha in long-run..

Kuwa mzalendo changia maendeleo ya Nchi yako.
 
Sio wizi ndio maana watu wametulia..

Huu ukiwa ndio wizi acha uendelee 👇
 

Attachments

  • Screenshot_20220816-203211.png
    87.3 KB · Views: 2
  • Screenshot_20220812-104856.png
    259.9 KB · Views: 2
  • Screenshot_20220812-104841.png
    268.4 KB · Views: 2
  • Screenshot_20220812-104925.png
    305.9 KB · Views: 2
  • Screenshot_20220713-194118.png
    155.5 KB · Views: 2
Ukiondoa lugha chafu, hoja yako ina mashiko.
 
Nimewahimiza Sana juu ya usimamaizi mzuri wa pesa za umma, nimewahimiza na kuwashauri Kama mwananchi na kijana wa kitanzania kuwa waziogope pesa za umma Kama ukoma, wasiziguse na kuzitumia kwa maslahi yao binafsi
Wenzetu hao wana mishahara mikubwa na bado serikali inawagharamia bure kwenye huduma muhimu na bado wana nafasi za kupiga pesa, sisi huku pamoja na kwamba hakuna cha bure tunaunga unga ndio tunahimizwa uzalendo kwa kuwekwa utitiri wa tozo na tukilalamika tunaonekana tunapenda bure bure tu hatuna uzalendo.
 
Kama na wao wangekuwa wanalipa Kodi, nadhani wasingekuwa wanaumiza wananchi namna hiyo
 
Fedha za COVID ndio unajivunia kujengea Madarasa na vituo vya Zahanati??. Tozo ni za akini Mwigulu kula bata na kujitajirisha tu...
 
Fedha za COVID ndio unajivunia kujengea Madarasa na vituo vya Zahanati??. Tozo ni za akini Mwigulu kula bata na kujitajirisha tu...
Wewe acha umbumbu wako,hakuna pesa ya covid imejenga vituo vya afya bali imejenga majengo ya EMD kwenye hospital za Mikoa na Wilaya na hospital za Rufaa..

Zahanati na Vituo vya afya vinajengwa kwa pesa ya tozo na Mapato ya serikali Kuu..

Kwani kabla ya pesa ya covid madarasa yalikuwa hayajengwi? Madarasa ya uviko yalikuwa mahsusi Ili kuhakikisha maelfu ya watoto wa Elimu bure waliomaliza mwaka juzi hawakosi nafasi.
 
Halafu pesa ikipatikana inatumika katika matanuzi ya viongozi fake walioingia madarakani kwa wizi wa kura chini ya mwehu mwendazake. Singida big stars ni kati ya wanufaika wa ufisadi huu
 
Kodi au tozo haziwahi kuwa wizi ndio maana nilikuuliza kama ni wizi hizi pesa zinaenda kutumika wapi? Hukujibu..pesa inatumika kuboresha huduma mbalimbali kama hizi [emoji116]
Wizi wa kidola dhidi ya wananchi, kwa kiasi kikubwa kinachoibwa hupelekwa kuhudumia dola.

Fikiria mwananchi anayetuma mchango wa kumtibu ndugu yake au maziko ya ndugu yake kwa njia ya simu, yeye mwenyewe ameshindwa kusafiri kwa sababu hana nauli, analipishwa tozo ili tozo ikamlipe posho na kumnunulia gari la kifahari Waziri au mkuu wa mkoa, au kugharamia mbwembwe za misafara ya viongozi wakuu wa nchi.

Kama wananchi wana mapato duni, na Serikali yao ni lazima iendane na uduni wa wenye Serikali. Lakini unapokuwa na walipa kodi walio duni kimapato, lakini watendaji wakuu wa Serikali wanataka mbwembwe sawa au hata kuzipita mbwembwe za mataifa yenye vyanzo vingi vya mapato, kwa kuwarundikia walipa kodi tozo nyingi, siyo sahihi, na siyo halali.
 
Mtapiga makelele wewe ila come 2025 mtakapokuta kila Kijiji kina maji,kina barabara,kina Zahanati na vituo vya afya ,kina umeme nk mtajua kwamba kumbe mlikuwa wajinga.
Hayo yote siyo hisani, ni wajibu wa Serikali, na yanastahili kufanywa kwa kutumia kodi halali zinazolipwa na wananchi. Na yanaweza kufanyika mengi zaidi ya hayo, huku wananchi hawanyanyasiki kwa tozo utitiri, alimradi tuwe na sheria rafiki za kodi, sera nzuri za uwekezaji, na mipango mizuri ya Serikali katika kutengeneza mazingira mazuri ya kujenga uchumi.
 
Zungu alisema ni kodi ya uzalendo.

Mtamrudisha bungeni 2025?
 
Lipa tozo subiria huduma
 
Lipa tozo dai huduma
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…