Mkuu umeona hiyo video ya habari ya ITV? Imeshawekwa kwenye huu uzi. Jisikilizie, jitafunie, jitafakari wewe mwenyewe. The story is real, uchumi hauendi vizuri; mtu kama unakuwa mkweli. Magufuli kadhibiti ufisadi; huo ni ukweli hakuna mtu anaweza kupinga hilo, ila ana wakati mgumu sana kukuza uchumi. Binafsi ninaamini kabisa, kwa jinsi ambavyo nimefuatilia namna ambavyo anafanya maaamuzi na kutekeleza sera zake, kwamba Rais wetu ni "mweupe" sana kwenye masuala ya uchumi. Na bahati mbaya yeye ndo mwamuzi wa mwisho.