TPA: Ni kweli Mizigo imepungua Bandarini

TPA: Ni kweli Mizigo imepungua Bandarini

Wamuambie mheshimiwa rais, atakishughulikia hilo ndani ya dakika 5 tu!!
 
Bahati nzuri ujenzi wa ghorofa letu umekamilika kwa asilimia kubwa.. La sivyo lingekuja ku sanda kama mafuta house...
 
Acheni uswahili wenu, ripoti ya tathmini ikionesha quantitative revenue fall iko wapi? Hizi ni longo longo tu za mawakala wa mizigo waswahili wa bandarini waliokuwa wamezoea kuwatumikia wasafirishaji wasiolipa kodi. Tunapima effectiveness ya mizigo ya bandarini si kwa kuangalia wingi wa mizigo (quantity) bali pia revenue size. Ni bora mizigo iwe kidogo lakini inayolipiwa ushuru na kodi stahiki kuliko mizigo mingi sehemu kubwa yake haililpiwi ushuru na kodi stahiki. Mawakala wa mizigo bandarini walijifanya wanamkomoa JPM kwa kula njama na kuwashawishi wasafirishaji kuwa wahamie bandari nyingine mbadala, sasa inakula kwao. Na TPA tayari imependekeza serikalini kuanzishwa tena wakala wa mizigo wa Serikali (NASACO) ili kujenga imani kwa washafirishaji watumiaji wa bandari ya dar es Salaam badala ya mawakala binafsi wasiokuwa na uzalendo, wanaosaliti taifa kwa rushwa zao. Sitashangaa ikiwa nikiambiwa kuwa hata na hao wabunge tayari wametia kitu mifukoni mwao
 
1.Mamlaka ya bandari yakiri upungufu wa mizigo bandarini.
2.Kamati za bunge zaitaka TRA ieleze inatoa wapi hizo kodi wakati idara nyingine zinalalamika hali sio nzuri
3.Kamati za bunge zawalaumu washauri wa Rais kushindwa kumshauri kwa mambo yanayohitaji UTAALAMU.



ITV habari saa 2
"Rais" ana washauri wa uchumi?
Kama wapo abawasikizaa?
 
Mbwembwe zote zimeishia kwenye aibu hii.

Ni wazi mapato ya mwezi tunayosomewa ni madeni ya nyuma sasa njia ya muongo ni fupi uchumi umekwama nadhani Leo ndiyo ccm watasadiki kuwa demokrasia na uchumi ni pande mbili za sarafu moja ukisigina kimoja umesigina vyote.

Na kwenye mambo ya fedha ni vigumu kudanganya maana mwisho wa siku fedha zinahesabika, na utajulikana tu unazo ngapi.
 
Kushauri mambo gani tena,na moja ya kazi ya wabunge si hiyo pia ya kuishauri serikali au wao kazi yao nini pale mjengoni Dodoma.
Si mlikataa ushauri wao mkasema wapinzani hawawezi kuwashauri nyie!
 
Hili nalo ni pigo la aibu kwa Serikali yetu
Sijui Watakuja na lipi sasa mana kila aina ya ukweli wanaupindisha uonekane ni uongo
Sasa muhimili mwingine wa Dola umetambua tatizo na kuamua kuliweka wazi, hii inamaanisha tunaongozwa na Serikali inayodangaya wananchi wake kwa kutoa taarifa zisizo sahihi
Ukisikia rais msanii ndiye huyu tuliyenae. Taratibu tu kitu kutakuwa wazi
 
threads kama hizi huwezi kumuona Lizaboni wala kijana yoyote wa Lumumba wapo kama hawapo.

Wabaridiiiiiiiii wanasoma tu comments[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Juzi kati kuna huyo boss wa bandari alisema...bandari mambo safi mizigo ni mingi....leo wamekanusha..
Na ndiye mtendaji mkuu, alienda kuzungumzia TBC1 baada ya kile kikao na wahariri ambacho kili expose kwamba bandarini kuna shida, hakuna mizigo....TBC 1 wakataka waweke sawa akaenda kuzungumza kule kitu tofauti kabisa!
 
Mbona Rais alisema acha isije.. Labda kuna namna nyingine wanapatia mapato
 
1.Mamlaka ya bandari yakiri upungufu wa mizigo bandarini.
2.Kamati za bunge zaitaka TRA ieleze inatoa wapi hizo kodi wakati idara nyingine zinalalamika hali sio nzuri
3.Kamati za bunge zawalaumu washauri wa Rais kushindwa kumshauri kwa mambo yanayohitaji UTAALAMU.



ITV habari saa 2
Mary Mwanjelwa kauliza swali zuri sana; bandari mnasema mapato yameongezeka, TRA wanasema makusanyo yameongezeka sasa inakuwaje inasemwa fedha zimefichwa hazionekani?
 
Mkuu wengine tulikuwa tunajuba mitego yetu huku kisiwani hatujaona hiyo habari, hebu tupia dondoo kidogo.

Mkuu umeona hiyo video ya habari ya ITV? Imeshawekwa kwenye huu uzi. Jisikilizie, jitafunie, jitafakari wewe mwenyewe. The story is real, uchumi hauendi vizuri; mtu kama unakuwa mkweli. Magufuli kadhibiti ufisadi; huo ni ukweli hakuna mtu anaweza kupinga hilo, ila ana wakati mgumu sana kukuza uchumi. Binafsi ninaamini kabisa, kwa jinsi ambavyo nimefuatilia namna ambavyo anafanya maaamuzi na kutekeleza sera zake, kwamba Rais wetu ni "mweupe" sana kwenye masuala ya uchumi. Na bahati mbaya yeye ndo mwamuzi wa mwisho.
 
Mwanzoni tuliaminishwa kuwa mizigo kupungua ni ile ya wakepa kodi na mambo yapo shwari sasa tunasikia kuwa hata wale walipaji wamepunguza kuleta mizigo...TRA wao mapato yanazidi kupaa, hii nchi ukifuatilia sana unaweza kuchanganyikiwa...wahenga walisema mficha maradhi kifo humuumbua
 
Back
Top Bottom