TPA: Ni kweli Mizigo imepungua Bandarini

TPA: Ni kweli Mizigo imepungua Bandarini

Tulieni Mnyooke!

Wakati wa JK mlidhani mambo yanajiendea tu ndio sababu mliimbishwa nanyi Mkaitikia kiitikio eti Kuna Ombwe la Uongozi.

Bandari ilipovamiwa kwa Mbwembwe mkashangilia mlidhani anakomolewa Jakaya. Magari yamepungua kutoka 3,500 mpaka 1,500 na bado mpaka itafika 500 kwa siku.

Sasa Chanjo kadhaa zimeanza kuadimika.

Lazima Mnyooshwe na mtanyooka Tu.
Mapumziko Mema Rais Mstaafu Kikwete kuna watu walidhani wakati wako Mambo yanajiendesha tu!
Mount Meru ipo Mnadani inauzwa kwa kukosa wateja
Zingine zinageuzwa Hostel bila ya kujua Pass mark zimeongezwa kupunguza Wanafunzi Vyuo vikuu.

Wa Vietnam wamefika Dar Jana wameenda mpaka Msoga kuchota Hekma halaf kuna Vichaa walitufundisha eti ni Rais Dhaifu.
Naupenda sana Utawala na Leadership style ya Magufuli kwa kuwa inathibitisha nilichokuwa naamini Juu ya Jakaya Kikwete.

Wale walioruhusiwa kufanya Siasa kwa uhuru walituaminIsha wanafanya hivyo kutokana na Ujasiri na uthubutu wao sio Utashi wa Rais Leo hii wote wamefyata na Mwanamume Mmoja anazunguka Nchi nzima kupiga Mikutano
Hahaha.,.mkuu mtu akikusoma between the lines atakuelewa Sana,,......so what is the way forward?
 
Mweeh!kweli ccm inapaswa kujilaumiwa kwa kueneza ujinga TZ hi..yani kwa akili yako tani 1000 ndo zinaongeza mapato
wewe kunakitu huelewi...

Hela inayo kusanywa sasa inaonekana na inatangazwa wazi

wewe hiko kipindi cha tani 40000 ilikua unayajua mapato
 
Juzi kati kuna huyo boss wa bandari alisema...bandari mambo safi mizigo ni mingi....leo wamekanusha..
Alikuwa anatudanganya sisi wananchi na muheshimiwa raisi pia kwa vile huangalia taarifa ya habari! Kama angejuwa namna uheshimiwa mpendwa wetu anavyochukia kudanganywa, angelikwisha nunua jeneza tayari!
 
Kosa tulilolifanya ni kudharau maoni ya watu eti kwa vile hawakuwa 'wenzetu', nakumbuka kumsikia mtu anayeitwa Ngatunga akitahadharisha kila mara kwamba VAT itakimbiza mizigo ya nchi jirani na wakati huo mizigo ilikuwa bado ipo lakini alipuuzwa sasa tatizo limekuwa kubwa ndio wanakuja na wazo la kuitisha mkutano wa wadau!
Mkitaka kujua ubaya wa siasa katika biashara ndio hapa maana kama mfanyabiashara atakuwa ameenda kwingine akajaribu huduma na labda akagundua utofauti itakuwa ngumu kumshawishi kurudi maana hwa hawaendeshwi kwa amri za wanasiasa katika kuamua mizigo ipitie wapi.
Nikuulize mkuu. Hivi hii va unayosema katika kipindi cha awamu ya nne na ya tatu haikuwepo au ilikuwaje. Naomba kufafanuliwa.ni kitu gani baada ya kuingia Magufuli kimebadilika pale bandarini.
 
Duu nawe umekuja na Kali ya mwaka!umejibu kisiasa,hujasikia bosi wa bandari anakiri mizigo kupungua,icd kuikosa mizigo?
Mkuu ina maana huyu jamaa anaendeleza propaganda na Porojo hadi muda huu? Hajaangalia taarifa ya habari? Jamani siasa kwenye mambo ya msingi tuyaache.
Tuwe wakweli, huo ndiyo uzalendo. Hali iliyofikia bandari kuendeleza propaganda hakutasaidia chochote. Hali ni mbaya halafu mbaya zaidi bado kuna watu wanatetea ovyo kabisa

Kuna jambo moja limenishtua kidogo, Dr Kafumu(kama sikosei) wakati akiwa bandarini anakiri kuwa kamati yao ilishauri kuhusu VAT ya Benki na Miamala ya Simu ila anasema, USHAURI WAO HAUKUCHUKULIWA.

ninavhoweza kucoment kama ni kweli basi Bunge la Mwez huu Wabunge waondoe dosari zote. Kuna mambo mengi yanatakiwa kuboreshwa.
 
wewe kunakitu huelewi...

Hela inayo kusanywa sasa inaonekana na inatangazwa wazi

wewe hiko kipindi cha tani 40000 ilikua unayajua mapato
Uwe unaangalia na makodi yaliyozidi kwa wananchi. Leo hii kila kitu juu alafu unashangilia pato kuwa juu
 
Tatizo sio kupungua mizigo bandarini, ishu hapo ni kodi. Wapo waliozoa kupiga dili, kupitisha mzigo bila kulipa kodi, bora kuwa na mizigo michache inayolipiwa kodi
 
Mizigo hamna wa Zambia na wa Congo wanpitia Msumbiji wafanyibiashara wa kwetu wanashindwa kuagiza maana kodi i akusanywa kwa nguvu sasa kutakuwaje na mizigo.
Ungeshauri kodi ikusanywe kwa kubembelezwa eti kamanda. ?? Basi sawa. ! Ni hayo tu
 
wewe kunakitu huelewi...

Hela inayo kusanywa sasa inaonekana na inatangazwa wazi

wewe hiko kipindi cha tani 40000 ilikua unayajua mapato
Si bora hela ikusanywe kidogo lakini maisha yawe mepesi kwa wananchi. Kuliko kukusanya pesa nyingi alafu watu mlo mmoja tu shida
 
Si bora hela ikusanywe kidogo lakini maisha yawe mepesi kwa wananchi. Kuliko kukusanya pesa nyingi alafu watu mlo mmoja tu shida
ndugu yangu unafanya kazi wapi?

au umejiajiri?
 
Naona kuna hii kadhia ya mizigo kupungua bandarini
Kamati ya Bunge imekutana na wadau Bandarini na wamekiri mizigo kupungua na kuomba wahusika kukutana na kutafuta suluhisho, huku wakiwalaumu Wataalam kwa kushindwa kumshauri Mh Rais vizuri

Chanzo ITV news

Ningependa wabunge watoe mawazo yao kama kuishauri serikali kwa suala hili. Ndio kazi yao ya msingi. Na we hope wakiondoka pale basi tutaona mabadiliko chanya pale.Mungu ibariki Tanzania
 
Si bora hela ikusanywe kidogo lakini maisha yawe mepesi kwa wananchi. Kuliko kukusanya pesa nyingi alafu watu mlo mmoja tu shida
Kamanda una maana hela ikusanywe kidogo na nyingine iende mifuko! mwa watu mojakwa moja ili watu wakafaidike na wizi huo mtaani au siyo. Kuliko serikali kukusanya mapato yote bila kuachia wizi ufanyike kidogo. Haya ndio mawazo yako kamanda. Basi sawa !! Safi sana. Umesoma mpaka la ngapi wewe
 
Hao waliovujisha hii siri wanataka kutushitaki kwa wananchi hiiiiiiiii
 
Wale vyura wa lumumba wako wapi sasa waje watoke povu?
 
Wamshauri Raisi....? Amewataka ushauri....??
 
Back
Top Bottom