TPA: Ni kweli Mizigo imepungua Bandarini

TPA: Ni kweli Mizigo imepungua Bandarini

Ndoo hivyo tena mtukufu wetu ame decided kutomsilikiliza yeyote yule,yetu macho sisi na kumuombea......
 
Muda huwa ni muamuzi mzuri, watu wakisema kwamba hii serikali inajitekenya yenyewe wanaambiwa ni wachochezi, Hatari kubwa tuliyonayo ni kuwa na viongozi ambao wanalinda vyeo badala ya kuvitumikia vyeo vyao, sasa unajiuliza MTU anapika data za mapato ili nini sasa,Serikali hii naona inashindana na serikali iliyopita kwamba ni ipi inafanya vizuri ukilinganisha na nyingine ndo maana hzi data zinapikwa. Ukweli ni kwamba kwa MTU mwenye akili ukitizama ile budget iliyopitishwa unaona kuwa haitupeleki kokote, tulihitaji sana mawazo na michango ya wapinzani katika ila budget ila kwa bahati mbaya wabunge wa ccm waliamua kufanya walichofanya, badala ya bunge kuwa sehemu ya kuapambanisha hoja ili tupate njia itakayo tupeleka pale ambapo jicho la kila mtanzania mpenda maendeleo linapatizama imekuwa ni sehemu ya kuilinda serikali. YAANI IKITOKEA UMEONA MAENDELEO TANZANIA UJUE YAMETOKEA TU SABABU WAKATI WAKE UMEFIKA NA SI KWAMBA YALIANDALIWA KUTOKEA.
 
Hivi huwa ni nani anawapangiaga hayo malengo yao. Yaani mapato yapande, yashuke wao utawasikia tumevuka lengo. Usikute wanajipangiaga lengo baada ya wao kuwa wamekusanya mwishoni mwa mwezi.
 
Labda uelewa wangu mdogo. Nahisi mapato yetu ni madogo sana ukilinganisha na bajeti ya tr. 29. Ili tuweze kujitegemea ilitakiwa walau tukusanye tr. 2.5 kwa mwezi. Lakini naona kama kwa wastani tunakusanya tr 1 kwa mwezi ambayo ikiendelea tutakuwa watumwa kwa wakubwa. Tujaribu kupanua uwigo wa ukusanyaji kodi hasa kwenye madini na tupunguze kodi kwa wafanya biashara ili wengi wawe wanatoa kodi kwani kwa kodi kubwa inawafanya wengi kukwepa na bei za vitu zinakuwa juu kwa kisingizio cha kodi kubwa. Hivyo wananchi tunapata shida ya gharama kubwa ya vitu. Wizara husika iangalie njia za kusaidia tuweze kijitegemea kwa mapato yetu na hivyo kusaidia nia njema ya babaetu wa nchi itimie. Ni mtazamo wangu.
 
Sijui ni mara ngapi wadau mbalimbali wamesema kwamba haya mambo ya kubandika kodi za bandarini kama VAT kwenye transit goods yanakimbiza wateja toka bandari ya Dar. Kwa kusikitisha sana, serikali yetu ikawa kila ikiambiwa hivyo inakuwa kama tunampigia mbuzi gitaa. Sasa serikali imekiri kwamba mizigo katika Bandari yetu imepungua kwa asilimia 42. Sasa serikali inapanga mikakati kwenda kuwabembeleza watumiaj wa bandari ya Dar warudi.

Sasa ujumbe kwa serikali ni kwamba, ubishi hautatupeleka mbali, ni muhimu sana kuwasikiliza wadau badala ya kujifanya ukiwa kigogo basi unajua kila kitu na wengine wote wanaongea pumba.

Sasa bado suala la kuongeza VAT kwenye mambo ya utalii, na mengineyo.

See: IPPMedia
Govt caves in, admits to 42 pc business slump at Dar port
Kwenye hili la muundo wa kodi za 2016/17 serikali imechemsha.
Kuna watu ningekuwa na uwezo ningewapiga miaka 15 jela kila mmoja.
Taifa limepata hasara kubwa sana ya mapato, ukiachilia mbali kodi (hiyo watadai mizigo ya nje hailipiwi kodi)
Kuna mapato yanayotokana na huduma k.v makampuni ya usafirishaji, mafuta ya magari na mitambo, chakula na malazi, e.t.c ambavyo vyote vilikuwa vinachangia pato la ndani la mwananchi wa tanzania.
40% drop...ni kubwa na mbaya sana.
Kuna biashara (hasa za mafuta) zimeathirika sana kwenye njia kuu.
Serikali ijenge utaratibu wa kukaa na kushauriana na wadau kabla ya kutoa amri na matamko...
Kule kwenye mabenki nako wateja wa chini wametwishwa mzigo na kodi ile haikusanyiki kirahisi na ni gharama kubwa kwa mabenki kuunda mfumo mpya wa hesabu na kodi.
 
Wanasema wanavuka lengo hata mchanganuo wa hayo makusanyo hawatuwekei ukiambiwa umepika data sijui utajiteteaje
 
Inachukua miaka mingi sana kujenga nchi yenye uchumi Imara, lakini ndani ya mwaka mmoja unaweza kuharibu uchumi uliotengenezwa kwa miaka zaidi ya 50
 
Sijui ni mara ngapi wadau mbalimbali wamesema kwamba haya mambo ya kubandika kodi za bandarini kama VAT kwenye transit goods yanakimbiza wateja toka bandari ya Dar. Kwa kusikitisha sana, serikali yetu ikawa kila ikiambiwa hivyo inakuwa kama tunampigia mbuzi gitaa. Sasa serikali imekiri kwamba mizigo katika Bandari yetu imepungua kwa asilimia 42. Sasa serikali inapanga mikakati kwenda kuwabembeleza watumiaj wa bandari ya Dar warudi.

Sasa ujumbe kwa serikali ni kwamba, ubishi hautatupeleka mbali, ni muhimu sana kuwasikiliza wadau badala ya kujifanya ukiwa kigogo basi unajua kila kitu na wengine wote wanaongea pumba.

Sasa bado suala la kuongeza VAT kwenye mambo ya utalii, na mengineyo.

See: IPPMedia
Govt caves in, admits to 42 pc business slump at Dar port
Selikali inafanya sawa kabisa. Nakupa mfano ulio hai. Ndani ya emirates kuna nchi inaitwa Ajman.kuna port ya Ajman ambayo kipindi cha miaka5 ya nyuma bandari ilikuwa full of vessel full of cargo na kipato kilikuwa juu.Badae walitangaza tenda ya kubinafsisha bandari. Kuna kampuni inaitwa Hutchison ilishinda tenda. Huyu Hutchison ndio mmiliki wa Ticks hapo Dar.

Hii kampuni ilianzisha kodi ktk vitu vya transit,huduma ya bandari ilipanda mfano kushusha kontena moja kwa kutumia shore krane za bandari sasa imefika 1700dirham. Wateja wengi wamekimbia bandari ipo empty. Kwa wiki zinakuja meli za contena 6. Lkn cha kushangaza bandari inaendelea wameweka maghala 13 ya kuhifadhi vitu vya baridi,wafanyakazi mshahara umepanda.

Ktk udadisi nimegundua kitu kimoja hii kampuni ya kichina inavyofanya inafanya kazi na kampuni moja ambayo meli zake ndio zinakuja hapa.inauhakika na kipato ambacho hakina njia za panya. Kwa hiyo kipato si kikubwa kama mwanzo lkn ni kikubwa unapotoa matumizi na kubaki na faida. Faida ya mwanzo kipindi meli ni nyingi ni ndogo kutokana na upotevu,matumizi.

Ukilinganisha na sasa vyombo vichache uhakika wa mapato l,matumizi madogo.faida kubwa. Google Hutchison Ajman free zone utaona. Meli ni zatu zinazopishana hapa.Dubai fortune,Dubai enterprise and Maratan..
 
umungu mtu wa magufuli unaua taifa!


Sijui ni mara ngapi wadau mbalimbali wamesema kwamba haya mambo ya kubandika kodi za bandarini kama VAT kwenye transit goods yanakimbiza wateja toka bandari ya Dar. Kwa kusikitisha sana, serikali yetu ikawa kila ikiambiwa hivyo inakuwa kama tunampigia mbuzi gitaa. Sasa serikali imekiri kwamba mizigo katika Bandari yetu imepungua kwa asilimia 42. Sasa serikali inapanga mikakati kwenda kuwabembeleza watumiaj wa bandari ya Dar warudi.

Sasa ujumbe kwa serikali ni kwamba, ubishi hautatupeleka mbali, ni muhimu sana kuwasikiliza wadau badala ya kujifanya ukiwa kigogo basi unajua kila kitu na wengine wote wanaongea pumba.

Sasa bado suala la kuongeza VAT kwenye mambo ya utalii, na mengineyo.

See: IPPMedia
Govt caves in, admits to 42 pc business slump at Dar port
 
Sasa kama mapato yanashuka mapema hivi utalipwaje huo mkopo wa Exim ya China wa standard gauge sababu tumekopa zaidi hata ya budget ya mwaka na nusu?
 
!
!
tumeipenda wenyewe tintiiiii chaguo letu wenyeweee tintiiiii wacha waisome namba eeeeh wajinga waleee sisiem mbele kwa mbeleee ooooh mbele kwa mbeleee waacheni waandamanee eeeh waandamane sisiem mbele kwa mbeleee
 
Back
Top Bottom