TPA: Ni kweli Mizigo imepungua Bandarini

TPA: Ni kweli Mizigo imepungua Bandarini

Kwa hiyo what's your argument? Mh. Rais aruhusu ufisadi kuendelea ili mizigo i rudi or? What exactly happened mpaka mizigo ipungue?

Ukiniuliza mm nitakwambia, the whole economy ilikuwa inaendeshwa kifisadi na wakafanikiwa kukamata njia kuu za uchumi karibu zote sasa unafikiri wao hawana strategies za kuilazimisha serikali ikubali kulegeza masharti kidogo? Mawazo yangu haya...

Then we need to come together as a country to decide je tuendelee na statusquo au tujenge uchumi inaomilikiwa na wengi ili in long run kusiwepo tena na carteils ambazo zitatuletea shida kama taifa.
Acheni kuchanganya mada kwa viENGLISHI vyenu vyakuombea Maji issue ni miKODI isiyozingatia kipato Halisi
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Hata wakikaa kikao bado kuna tatizo la biashara kutotabirika kutokana jinsi nchi inavyoendeshwa na pia matamko ya kushtukiza ambayo yanamfanya mfanyabiashara yoyote kusimamisha biashara ili upepo ukae sawa maana huwezi kuwekeza mtaji mara kesho unasikia serikali inahamia dodoma unajipanga kuwekeza dom mara wanaamka imeshindikana kuhamia dodoma,na kipindi hiki kipato kimekuwa kigumu sana watu wengi wamepunguzwa makazini wengine wamesemwa ni hewa wako mtaani hawana kitu hizo biashara watanunua na nini wakati purchasing power imepungua?serikali ifike mahali iweke wazi mipango yake ieleweke sio kuendeshwa kwa matamko mara hakuna kuvuta shisha mara baa kufungua saa kumi.....
Hapa ndipo lilipo tatizo Nadhani watu wengi hawajui au wanapotosha makusudi
 
Kidogo kidogo tunaanza kufahamiana. Ni hivi majuzi tu watu wa bandari walieleza ukweli kwamba mizigo imepungua bandarini na kusababisha wazifunge bandari kavu. Lakini siku mbili baadaye walilazimishwa kukanusha. Na wao bila kujitambua wakaja kukanusha kupitia mkurugenzi wa bandari. Leo, taarifa ile ile (ya kupungua mizigo bandarini) imeletwa/imesemwa na Kamati ya kudumu ya Bunge na mmeshindwa kuwashurutisha wakanushe na hata wenyewe hamna namna ya kukanusha, badala yake mmeamua kukubaliana na ukweli kwamba mizigo imepungua lakini mmekuja na ngonjera kwamba makontena yaliyopungua ni yale ya Wanyarwanda na Wakongoman ambayo hayana mchango wowote katika kuongeza pato la taifa. Kesho mtasema mengine na hatimaye mtakiri kwamba kupungua kwa mizigo bandarini kumesababisha hali tete ya kiuchumi hapa nchini. Nyie endeleeni kujidanganya wakati hali inazidi kuwa mbaya kila uchao.
Mkuu taratibu tutaelewana tu si wanasema iliyopungua ni mizigo ya transit; tusubir muda utafika tusutumie nguvu kubwa kuwaelimisha kama lile sokomoko la sukari. Wiki mbili tu zinatosha kuanzia leo
 
kumbe madai yenyewe ni hayo hata wasipolipwa hakuna shida
Haya hii ni akili. Na utashangaa ukifuatiliwa huenda wewe ni kiongozi mkubwa tu serikalini. Kwa mtindio huu wako wa ubongo kwa nini tusiyumbe
 
Unaweza kumwamini mbunge yeyote lakini siyo Dalai Kafumu wala Mary Mwanjelwa, hawa ni mawakala wa wapiga dili wanajulikana
Ni jambo la kusiktisha sana kwa CCM kuwapitisha wapiga dili na watu wasioaminika kuwa wagombea wao wakati wanadai mwaka jana CHADEMA haikushinda kwa kuwa Mgombea wake hakuwa anaaminika kwa wananchi, sasa hawa kina Kafumu na Mwanjelwa wapiga dili walishindaje?

Eng. Kakoko hajasema kuna tatizo la mizigo bali amewashauri TRA waachane na njia za zamani za kutathmini thamani za magari ambazo zinashawishi rushwa. Alipendekeza TRA watumie njia ambazo ni transparent.
Kimantiki hapa inasemwa kuwa uthaminishaji wa kodi kwenye magari unafanyika kwa mbinu za kizamani maana yake ni kuwa, kama kodi ikiwa inakadiriwa kwa kutumia uthaminishaji huo wa kizamani watu watatumia bandari nyingine kwa kuwa kodi kweye bandari ya Dar itakuwa kubwa. Kutumia Bandari ya Dar ni kwa maslahi na wala si amri ya Mungu!
 
Mimi ni dume la mbegu lililokomaa kama beberu la mbuzi.unatafuta bwana?nenda chit chati.


Swissme
 
Hiyo Kamati ya bunge nani kaipa mamlaka ya kuhoji utendaji wa taasisi za serikali
 
Huku TRA wanadai
Ni kweli makusanyo ya kodi yameongezeka maradufu
Na Huku mtaani wanadai pesa ngumu kupatikanikupatikana
Halafu yule bwana anadai et watu wameficha mihela, huku akizidi kujitwisha mizigo mizito ya kiuchumi
Kwa stahili Hii sidhani kama tutafika kwenye vile viwanda
 
Hebu watz tujadiliane kwa misingi ya ukweli kama kweli tuna nia ya kwenda mbele kama taifa.
Ukweli ni mchungu lakini kilicho wazi ni kuwa zaidi ya 50% ya biashara wakati wa awamu iliyotangulia ilikuwa ni upigaji. Ndio maana ikasemekana kuwa kuna watu walijenga hadi yard China na waliweza kuwaletea wafanyabiashara mizigo hadi mlangoni kwao bila kujua ushuru, bandari vimelipwaje maana wenyewe walishakuwa na mtandao kote huko (ukitafuta hapa jf haya yote yapo tena kitambo). je, hii ilikuwa sahihi!?
Kwa maana hiyo kuzuia wakwepa ushuru ni wazi lazima mizigo ingepungua kwa zaidi ya 30% (japo) sio kama sasa. Ila kichocheo kingine ndio hicho cha VAT kwenye transit cargo (mizigo ya Zambia, Congo, Malawi nk). Kuna kitu kingine kilichowakimbiza Watu wa DRC na hakisemwi, kwamba kutokana na mkataba kati ya Tanzania na DRC makadirio ya ushuru huko kwao yanafanyikia hapa kabla mzingo haujaondoka. Hiyo nasikia inawafanya walipe kodi stahiki huko kwao kitu amabcho wafanyabiashara wote duniani huwa ni tatizo hivyo wanachagua kupitisha mizigo kwenye nchi ambazo ushuru unakadiriwa mzigo ufikapo DRC.
Pia issue ya magari kupungua tukubaliane kiungwana, hivi unadhani mtu aliyekuwa na mishahara hewa labda tuseme 7 (saba) kati ya sijui 15,000 waliokwishajulikana unadhani purchasing power yake itabaki sawa!? Na unajua huyu alikuwa ananunua magari mangapi kila mwezi!? Je, hizo barabara hewa, tenda hewa, uniforms hewa unadhani pesa zao zilikuwa zikichangia kuagiza magari mangapi kila mwezi!?
Suala la VAT, TRA waliambiwa wakapuuza lakini wabunge ndio wakapuuza zaidi kwa kulipitisha basing on ushabiki wa vyama. JPM sawa 'anavuruga' lakini kuna mambo logically lazima ayatekeleze na makosa mengi ni ya watangulizi na yatamsumbua kutokana na watu waliomzunguka ila wajuzi wa mambo wanasema chama hiki kikiondoka ndipo tutapata mwelekeo.
Hitimisho ni kwamba, zile kontena zilizokuwa zimeibiwa bandarini bila kulipiwa ilikuwa ni kweli na maofisa wa bandari kula pesa za tozo ilikuwa ni kweli pia. Sidhani kama ilikuwa ni busara kwa PM, JPM na serikali kuwaachia hawa watu waendeleze upigaji kwa kisingizio cha mizigo kupungua
.
Muhimu hapa ni Kuwa na mifumo shirikishi MTU mmoja hawezi. Mungu mwenyewe anasaidiwa na Malaika wake. Lingine shida yenu vijana wa Tz uwa mnajadiri masuala kulingana na egemeo la maslahi
 
Uchumi unategemea zaidi kodi au uzalishaji ??
 
Acheni kuchanganya mada kwa viENGLISHI vyenu vyakuombea Maji issue ni miKODI isiyozingatia kipato Halisi

But we communicate this is enough for me...kiinglish hakina tofauti na kihaya sasa whats your problem...wewe labda unayedhani kiinglish ndiyo science ndiyo upo na mind long as ume elewa then am okay sawa....kama hujaelewa nitamia luga yangu ilinieleweke vizuri maana hata kiswaheli ni cha wa pwani ambapo mimi siyo sasa nitumie luga gani kama hizo mbili zote sizifahamu vizuri?

Acha utoto mada hii inahusu nchi na siyo nani anajua kuremba luga ya wakoloni either kiswahili chenye mchanyato wa wakoloni wa zamani na kiwazungu wale walioondoka kabla mimi sijazaliwa!
 
Back
Top Bottom