Polisi jamii
JF-Expert Member
- Mar 22, 2013
- 2,603
- 1,385
sasa gari la milion 5 ushuru wake milion 7 ?? yaana ushuru unabei kubwa kuliko gari bora upitishie msumbiji
Kuficha noti nayo ni single kama ile ya wafanyakzi hewa na ajira mpya. Tusubir kidogo hiyo nayo ikichuja kwa vyovyote vile kuna nyingine jikoni.Upinzani walilalamika Sana hili la bandari na utalii lakini jamaa akasema yeye Ni baunsa WA njaa, njaa ikimuona inakimbia nasubiri mwisho wa mpambano nani ataibuka kidedea ingawa mmoja kaanza kulalamika uchumi umechoka kisa watu wameficha noti
lakin mbona IMF wametuambia kwamba ni nchi inayokua kwa kasi snaa kiuchumiHapana tusijipe mda tuamke sasa maana mda tukiamka Beira Durban na Mombasa zitakuwa mbali hatutakuwa na uwezo tena wa kuvutia wateja hivyo watakuwa na sauti
We kumbe kuna muda hua unaongea points? Usipende kujifunika kitambaa cheusi muda mwingine.Unauliza aliyofanya Jk?!
1) Ukiona tunajadili kupungua Mizigo bandarini ujue tunalinganisha na Wakati wa Jk.
2) Ukiona Kuna UKUTA ujue wanapigania uhuru Urudi Kama wakati wa JK
3) Ukiona Rais analalamika Mzunguko wa Fedha umepungua ujue analinganisha na Wakati wa Jk
4) Ukiona Hotel kubwa Kama Mount Meru inatangazwa kuuzwa ujue Biashara sasa hivi ni tofauti na Wakati wa Jk
5) Ukiona watu wanalalamika kupandishwa Passmark kuingia Vyuoni ili kupunguziwa mzigo Loan Board ujue wanalinganisha na Wakati wa Jk
6) Ukiona watu Wanalalamika kuropoka ropoka kwa Pombe Jua wanalinganisha na busara na hekma za Jk.
7) Wabunge waliokufundisha kushangilia Ziara za kustukiza Bandarini na kuwatimua Wateule wa Jk ndio Leo wanakufundisha ustuke Hali ya Bandarini ni zaid ya Hatari kutokana na fukuza fukuza na uvamizi ule.
8) Kama ulimuona Msigwa Ikulu kwny kugawa Madawati Jua anayapeleka kwny Madarasa yaliyojengwa wakati wa Jk sio anapeleka chini ya Mwembe!
Unaniuliza watu wakinyooshwa mie ntakuwa wapi Kwan nimekwambia Mie nitakwenda kuandamana kwny Ukuta? Mie sihitaji ajira Serikalini zilizozuiwa, sihitaji Promotion ya Mishahara iliyozuiwa, Sihitaji Bunge Live, Sitegemei kuja Kutumbuliwa kwa kuwa sio Mtumishi wala Mteuliwa, Shughuli zangu hazihitaji Ziara za kustukiza wala Maelekezo ya Wanasiasa. Tambua Mnyoosho huu unawahusu Watanzania Wengi ila si wote
Kumtukuza Jk sijaanza Mie wameanza wale waliokufundisha Kumchukia, hujamsikia Godbless Lema aliefikia hatua ya kupiga Marufuku Amiri Jeshi asikanyage Jamhuri ya Kaskazini yeye na Joshua Nasari wakajitangaza ndo Rais na PM wa Kaskazini lakin hata Onyo hawakupewa lakin Juzi Kati kamtukana Mrisho Gambo tu RC wake Maisha Lupango mpaka kasusa Kula ndio kapewa Dhamana? Hujamsikia Tundu Lissu? Jee nao akili zao Full Majanga kwa kuwa tu wamemtukuza Jk?
Walau umeleta wazo mbadala. Linachangamsha ubongo hiliNafikiri ni wakati mzuri wa kubadiri mfumo! Baada ya kusubiri mizigo ambayo haipo, sisi tufanye yafuatayo. 1. Tusafirishe nje malighafi na bidhaa. 2. Tuwekeze viwanda maana bidhaa zitakua adimu sokoni, kwahiyo tuna nafasi ya soko la bure. Ni wakati wa kuitanua nchi ila kwa wavivu wa kufikiri wanazani Sera za Raisi Magufuli zinaferi, lakini Mimi nadhani ni wakati muafaka wa kuimarika ndani ya nchi kwa kila kitu kinachokosekana tutazalisha hapa. Mfano, Mimi mwenyewe nimeona faida, maana pesa hakuna lakini kampuni yetu imeongeza mauzo, kwa maana bidhaa kutoka nje hakuna kwahiyo waliokua wanazarahu bidhaa zetu wamekuja kununua, ingawa kwa kiasi kidogo, lakini Malengo na nia zinaelekea kutimia. Namsifu Magufuli kwa maana katika shida tulio nayo sasa, tunaona tumaini la Kiwanda chetu kukua. Tujiamini watanzania, ni wakati wa sisi kuzarisha.
ukiitwa ccm umelaniwaNdoto
Hana uwezo wa kukanusha hili. suala lipo wazi bandari sasa inaweza kugeuka uwanja wa mpira, mizigo hamna. Wafanyabiashara wamehamia bandari ya Beira.bosi wa TPA najua atakanusha
kumbe madai yenyewe ni hayo hata wasipolipwa hakuna shidaHela ya uhamisho na mafao ya likizo
Mkuu mpaka asaiv ndo anaetamba mule majini kuna meli mbili tu zinangoja kushusha nimetoka zenji jana tu nimeliona hiloKufika mwakani tarehe kama za leo kule itakuwa inatamba mv kilimanjaro pekee
Tan 40,000 hadi tan 1000, uko wapi wewe bandari unajua ilipo? Pita ujionee..............hii habari ya kijumla sana, yamepungua kutoka mangapi hadi mangapi? mapato je? kama urasimu umeondolewa makontena yanaondolewa kwa wakati je? bandari sio yard wala stoo kama hayapo wenyewe wameyachukua.
Mbio za sakafuni tu ngoja stock za bidhaa muhimu zinazoagizwa na serikali ziishe ndio watasema wenyewe hakuna hela ya kuagiza nyingineTRA wanatoa taarifa za kupika juu ya kuongezeka mapato nchini, ki uhalisia unaweza kukuta wanakusanya chini ya 500B kwa mwezi
Ni mtego Mzuri sana. Inaonyesha hawawezi Ku deliver good results . Liko wazi, hakuna mizigo maana yake hakuna mshara . kazi oliuombele yao inajulikana . Waliajiliwa Ku deliver good results.Halafu kuna watu wakiambiwa ukweli utasikia ooh wanakwepa kodi akili zingine za kijinga toka tani elfu 40 mpaka tani 1000 si hatari hiyo..kisha TRA wanakuja na mbwembwe za kukusanya kodi kwa 98.9% sijui kama wana mapenzi mema na nchi hii au ni kumfurahisha boss wao