Tulieni Mnyooke!
Wakati wa JK mlidhani mambo yanajiendea tu ndio sababu mliimbishwa nanyi Mkaitikia kiitikio eti Kuna Ombwe la Uongozi.
Bandari ilipovamiwa kwa Mbwembwe mkashangilia mlidhani anakomolewa Jakaya. Magari yamepungua kutoka 3,500 mpaka 1,500 na bado mpaka itafika 500 kwa siku.
Sasa Chanjo kadhaa zimeanza kuadimika.
Lazima Mnyooshwe na mtanyooka Tu.
Mapumziko Mema Rais Mstaafu Kikwete kuna watu walidhani wakati wako Mambo yanajiendesha tu!
Mount Meru ipo Mnadani inauzwa kwa kukosa wateja
Zingine zinageuzwa Hostel bila ya kujua Pass mark zimeongezwa kupunguza Wanafunzi Vyuo vikuu.
Wa Vietnam wamefika Dar Jana wameenda mpaka Msoga kuchota Hekma halaf kuna Vichaa walitufundisha eti ni Rais Dhaifu.
Naupenda sana Utawala na Leadership style ya Magufuli kwa kuwa inathibitisha nilichokuwa naamini Juu ya Jakaya Kikwete.
Wale walioruhusiwa kufanya Siasa kwa uhuru walituaminIsha wanafanya hivyo kutokana na Ujasiri na uthubutu wao sio Utashi wa Rais Leo hii wote wamefyata na Mwanamume Mmoja anazunguka Nchi nzima kupiga Mikutano