Kwa nini Rais alaumiwe na wabunge kwa sheria iliyopitishwa na bunge? (VAT na Bajeti na kadhalika)
Au kama ni maamuzi ya Rais kwa nini walaumiwe wataalam, tunajuaje hakushauriwa?
Na kama alishauriwa, tunajuaje ushauri waliotoa wataalam ni upi, vipi kama hivi ndivyo Rais alivyoshauriwa?
Kuna mbunge kasema tusitafute mchawi, tukae pamoja tutathmini, tukae pamoja kina nani? Haya maamuzi huwa hayafanywi pamoja, ni lazima tujue maamuzi yanafanywa na nani katika ngazi gani ili tujue pa kurekebisha ni wapi na wakuwajibishwa ni nani.