TPA: Ni kweli Mizigo imepungua Bandarini

TPA: Ni kweli Mizigo imepungua Bandarini

Kwa kweli namba zimekuwa bolded mimi binafsi nimemaliza witiri nimeanza shufwa na hatimaye nitamalizia na tasa ila kitaifa bado hatujaanza kuzisoma vizuri.
 
Washauri, washauri, washauri!!! Ni lini tutasema rais? Ushauri una mipaka, je huyo unayempa ushauri anapenda kushauriwa na anaufanyia kazi ushauri?
 
Mkuu pia kuna uhaba wa vitabu vya passport toka mwezi wa nne mwaka huu, jamaa yangu wa uhamiaji hata hajui lini vitaletwa.!!!!

Teh teh! Vinasubiri kukamilika zoezi la uhakiki wa Watumishi hewa!
 
Magufulis worst enemy sio upinzani bali his most inner most circle.
Ni yeye mwenyewe ndiye his worst enemy kwa sababu ameshika mpini na watendaji wengine wanaenda kutokana na flow ya mchinjaji.
 
hata kama likiwepo kontena moja bandarini ni bora kuliko kuwa na msululu wa makontena ambayo hayana tija kwa taifa letu.Acheni longo longo na kutaka mambo mepesi mepesi .kodi lazimwa zilipwe.Hapa kazi tu
 
Washauri, washauri, washauri!!! Ni lini tutasema rais? Ushauri una mipaka, je huyo unayempa ushauri anapenda kushauriwa na anaufanyia kazi ushauri?

Mtoto wangu alipokuwa akipata Fedha na kuzichezea kwa anasa na kujionesha nilikuwa Namlaumu Mkewe eti Kashindwa kumshauri Mumewe kufanya Mambo ya Maendeleo. Kumbe Mkewe nae akawa analalamika kwa Watu kuwa Baba Mkwe wangu kashindwa kumshauri Mwanae kuacha Tabia za Matanuzi na Mashauzi.
Kumbe Mkwe wangu nami tulikuwa tunashuri sana kila Mtu kwa wakati wake na nafasi yake tatizo likawa kwa Mshauriwa!
 
Tulieni Mnyooke!

Wakati wa JK mlidhani mambo yanajiendea tu ndio sababu mliimbishwa nanyi Mkaitikia kiitikio eti Kuna Ombwe la Uongozi.

Bandari ilipovamiwa kwa Mbwembwe mkashangilia mlidhani anakomolewa Jakaya. Magari yamepungua kutoka 3,500 mpaka 1,500 na bado mpaka itafika 500 kwa siku.

Sasa Chanjo kadhaa zimeanza kuadimika.

Lazima Mnyooshwe na mtanyooka Tu.
Mapumziko Mema Rais Mstaafu Kikwete kuna watu walidhani wakati wako Mambo yanajiendesha tu!
Mount Meru ipo Mnadani inauzwa kwa kukosa wateja
Zingine zinageuzwa Hostel bila ya kujua Pass mark zimeongezwa kupunguza Wanafunzi Vyuo vikuu.

Wa Vietnam wamefika Dar Jana wameenda mpaka Msoga kuchota Hekma halaf kuna Vichaa walitufundisha eti ni Rais Dhaifu.
Naupenda sana Utawala na Leadership style ya Magufuli kwa kuwa inathibitisha nilichokuwa naamini Juu ya Jakaya Kikwete.

Wale walioruhusiwa kufanya Siasa kwa uhuru walituaminIsha wanafanya hivyo kutokana na Ujasiri na uthubutu wao sio Utashi wa Rais Leo hii wote wamefyata na Mwanamume Mmoja anazunguka Nchi nzima kupiga Mikutano
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] daah Kikwete ni bonge kiongozi nasikitika sikuliona hilo wakati wake, nilimtukana kwa uhuru masikini ya mungu hakunifunga bali alitabasamu kisha nae akanipiga jungu basi hayo ndo yakawa maisha yetu ila sikuwahi kuisoma namba.... Jakaya I mic u, ntakutembelea Msoga.
 
jamani ni hujuma ....!! au nini kukimbia uwajibikaji wa serikali.........?
 
Mkuu pia kuna uhaba wa vitabu vya passport toka mwezi wa nne mwaka huu, jamaa yangu wa uhamiaji hata hajui lini vitaletwa.!!!!
Wana zuiya watu wasitoke nje wakidhan wanahamisha pesa,
 
Sijaangalia taarifa ya habari leo ila kamati haiwezi kuhoji TRA eti mnapata wapi fedha za kodi wakati hakuna mahali ktk nchi ambako hapaingizi mapato.

kodi inalipwa tena kwa sasa maeneo mengi kodi na malipo yasiyokuwa ya kodi yanalipwa kwa njia ya mtandao na wizi umepungua sana na mapato yamepanda sana.

Hayo ya TPA wenye mamlaka watatoa taarifa kama kuna shida.

Naomba tuwe na positive thoughts itatusaidia ktk kujenga nchi yetu
Acha siasa zako ww uchumi hauhitaji siasa
 
Kwani hatahivyo tokea Mt.Meru hotel iliporekebishwa na kuanza kazi mpaka sasa mwenye hisa kubwa si jamaa wa Mauritius then Mkenya?

Hiyo ya kusema ni mali ya watanzania ni danganya toto.
Tunachoangalia cyo nani anamiliki bali tuangalie kwanini inauzwa
 
Tuendelee kufurahia maamuzi ya mkuu Wa nchi.bora meli moja iingie.kuna watu watakuja kukanusha
 
Sio hujuma.. Nilisoma mahali ni kwamba, ukiacha clearance fees kuna gharama nyingine ndogo ndogo ambazo anayetumia bandari anapaswa kuzilipa na wamekua wakizilipa. Mfano ni gharama za kupakua mzigo, kupakia mzigo nk.. Gharama hizi zilikua hazijawekewa VAT, mwaka huu wa fedha serikali imeongeza na VAT so hizo gharama zimeongezeka. Sasa kama ujuavyo wafanya biashara huangalia unafuu wa running costs ili kutengeneza faida.
Sasa basi kama gharama ndogo ndogo za handling ya mzigo bandari nchi nyingine ni ndogo watahamia huko.
Kumbuka sio bandari tu ambako Hii VAT kero imekua imposed. Kuna miamara ya benki ambako tulidanganywa benki zitalipa huku nasikia watu wanafungia fedha ndani sijui kweli? , kwenye utalii
pia ilileta shida nk

Huo ndo ufahamu wangu. Mwingine aweza ongezea
 
Back
Top Bottom