TPA: Ni kweli Mizigo imepungua Bandarini

TPA: Ni kweli Mizigo imepungua Bandarini

hata kama likiwepo kontena moja bandarini ni bora kulikokuwa na msululu wa makontena ambayo hayana tija kwa taifa letu.Acheni longo longo na kutaka mambo mepesi mepesi .kodi lazimwa zilipwe.Hapa kazi tu
Hamna shida, hebu nikuulize hivi mapato ya mwezi August tra wamekusanya kiasi gani? Kama huna jibu la swali hili kawaulize hata nyumbu wenzio lizabon na wenzake
 
Ni sawa na Tajiri anayeacha kufanya biashara ili kuwakomoa wanaomdokolea.....matokeo yake anafilisika...ukimuuliza anakwambia 'nimewakomoa waliokuwa wananidokolea'

Ama kweli kua uyaona🙂🙂🙂
 
Mizigo hamna wa Zambia na wa Congo wanpitia Msumbiji wafanyibiashara wa kwetu wanashindwa kuagiza maana kodi i akusanywa kwa nguvu sasa kutakuwaje na mizigo.
Baadae wakaja kusema hela zimefichwa ndani kumbe ni salio linapungua kila kukicha.

Hivi siku hizi huwa tunatangaziwa makusanyo TRA kila mwezi au wamesahau kututangazia?

Tz ya Viwanda ina mambo
 
Naona kuna hii kadhia ya mizigo kupungua bandarini
Kamati ya Bunge imekutana na wadau Bandarini na wamekiri mizigo kupungua na kuomba wahusika kukutana na kutafuta suluhisho, huku wakiwalaumu Wataalam kwa kushindwa kumshauri Mh Rais vizuri

Chanzo ITV news

Hawataki wapinzani wasimame na kuyasema haya mpaka yanafikia hatua ya kuharibika kabisa, hawajui hii ni nchi ya watanzania wote
 
Sibishani na kamati ya Bunge wala Tv nachosisitiza mtuwekee trend ya data za TPA na TRA kuhusu mizigo na kodi ili habari hiyo iwe na mashiko na siyo tu lugha za jumla jumla
Kusoma hujui hata picha huoni, naona wana lumumba ndiyo wamekutuma uje ulete hizi pumba
 
Kodi zimeongezeka maradufu kwa wafanyabiashara..Ndio maana hawapitishi tena mzigo bandari ya Dar.
Kodi gani imeongezwa mkuu. Labda tufahamishe. Isiwe unasema kinyume maana kipindi cha nyuma watu walikuwa wanakwepa kodi na hawalipi. Lakini this time wanawajibika kulipa no matter what. Tunajua ujanja wa wafanya biashara. Hata wewe unajua. Sema ukweli mzee.
 
Yap,ndo maana nikasema wabunge wangeshauri vyema kuhusu hilo katika kikao cha bajeti kilichopita basi mawaziri wangefikisha ushauri huo kwa Rais ila kama waliona hakuna tatizo wasibebeshe mzigo huo watu wengine ila waseme tu kila mmoja hajafanya kile kinachotakiwa.
Wabunge waliokuwa na uwezo wa kuyaona haya na kushauri walifanyiwa figisufigisu wakatoka nje wakabaki wale wa kushangilia na kupitisha kila kinacholetwa mezani,wacha tuisome namba.
 
Baadae wakaja kusema hela zimefichwa ndani kumbe ni salio linapungua kila kukicha.

Hivi siku hizi huwa tunatangaziwa makusanyo TRA kila mwezi au wamesahau kututangazia?

Tz ya Viwanda ina mambo
Yale mapato waliyokuwa wakitangaza hayakuwa mapato halisi kwa maana ya fedha iliyopo mkononi; ndani yake walijumuisha madeni uthibitisho wa hili angalia taasisi za serikali wanavyolia wamepelekewa hela ya matumizi ya mwezi mzima ambayo haiwezi kuwafikisha hata wiki moja
 
Hamna shida, hebu nikuulize hivi mapato ya mwezi August tra wamekusanya kiasi gani? Kama huna jibu la swali hili kawaulize hata nyumbu wenzio lizabon na wenzake
wewe sio mzima
 
Naona kuna hii kadhia ya mizigo kupungua bandarini
Kamati ya Bunge imekutana na wadau Bandarini na wamekiri mizigo kupungua na kuomba wahusika kukutana na kutafuta suluhisho, huku wakiwalaumu Wataalam kwa kushindwa kumshauri Mh Rais vizuri

Chanzo ITV news

Ukiona katibu mkuu wa wizara ya fedha baada ya muda mfupi amepumzishwa ujue hali ni tete.Ushauri umetolewa kwa TRA kukusanya kodi ya majengo(p/tax) ,miamala ya simu na benki ili kufidia.
 
Mimi sio muumini sana wa ushababi lakini ninawasiwasi kuwa suala la bandari lina mambo Mwawili:
(1)Ama misamaha ya kodi toka serikalini ilikua ni mingi.

(2)Au tra walitia mfukoni mwao mapato mengi waliyokua wanakusanya mana haiwezekani Tani 1000 ziwe zinaingizia serili pato kubwa kuliko tani 40000.

Kama ni kweli kuwa rani 1000 zinatupa pato kubwa kuliko tani 40000 basi bora hiyo mizigo isije mana haina faida kwa watanzania zaidi ta watu wachache.
Rais wetu kwenye utawala wake ameamua kusimamia maslahi ya wengi hasa watu wa chini.
Kwa hiyo naamini bado kuna nafasi ya kutazama nini tatizo kati ya tra na misamaha ya kodi.

Ni bora sasa wabunge wa CCM ambao mara nyingi wamekua wakituangusha wakakaa na kutunga sheria mpya ya sera ya uchumi wa taifa. Viongozi wa umma wanaolipwa mishahara minono wasijihusishe na biashara moja kwa moja ili wafanyabiashara nao waachane na kujipenyeza kwenye siasa. Serikali ibaki kusimamia watendaji wake tu na sio kuingilia wafanyabiashara ambao wanawajibu wa kisheria wa kulipa kodi tu .
Suala la misamaha ya kodi lifutwe kabisa. Kila mtu na taasisi walipe kodi.
Hii misamaha ya kodi ni janga kubwa sana linalosababisha kodi kuwa kubwa kwa wale wanalipa.
Matokeo ya misamaha ya kodi ni kusababisha taasisi za kibiashara kufilisika kutokana na kulundikiwa makodi mengi ili kufidia ile misamaha ya kodi kwa taasisi nyingine. Matokeo ya kufilisika kwa walipa kodi ni kuendelea kupungua kwa walipa kodi na mapato.

Mfano hakuna haja ya kuwa na misamaha ya kodi kwa taasisi za dini wakati sinakusanya mabilioni ya walipa kodi kama sadaka. Ndio maana wanabaki kukenua meno tu bila kujua kuwa nchi ni uchumi. Bila uchumi hata pesa za kununua magari ya washawasha hazitapatikana.Waumini wao watakua hawana pesa za sadaka na serikali itashindwa kusomesha watoto wa maskini bure.

Kodi zipunguzwe na kila mtu alipe kodi. Misamaha ya kodi ifutwe kwa taasisi zote.
 
Kodi gani imeongezwa mkuu. Labda tufahamishe. Isiwe unasema kinyume maana kipindi cha nyuma watu walikuwa wanakwepa kodi na hawalipi. Lakini this time wanawajibika kulipa no matter what. Tunajua ujanja wa wafanya biashara. Hata wewe unajua. Sema ukweli mzee.
Ukweli unasemwa kila mara tatizo hamkubali. Kumbuka la sukari mpaka tahadhari ilitolewa watu wakatokwa povu kubisha ukweli namkumbuka lizaboni jinsi alivyotoka jasho mpaka la ukucha. Leo nina uhakika ananunua sukari tsh. 3000
 
Kwa Kadri ninavyojua ni kweli Mizigo Bandarini imepungua,But kwa uhakika pia ni kweli TRA inakusanya kodi zaidi mda huu ambao mizigo imepungua, Hapo Awali watu walikuwa hawalipi kodi sasa wanalipa tena vizuri,Hii Concept ya Mizigo kupungua kwanza Hiyo kamati ya Bunge Lazima ijiulize ni Mizigo gani Kwa Kadri ninavyojua baada ya kuanzishwa utaratibu wa Single custom territory Na Marais wa Nchi za Maziwa makuu Rwanda na Kongo wamekimbia na sasa wanapita Msumbiji lakini lazima tuwaeleze watu ukweli je Hizo contena (Mizigo) iliyokimbia ambayo ni Transit ilikuwa inalipa kodi?

TRANSIT hazilipi kodi ni Zero ndio Maana watu wanashangaa kontena zimekimbia TRA wanavuta malengo Transit zimekumbia sababu zimewekewa VAT lakini walikuwa hawalipi Kodi TRA kwa TPA walikuwa wanalipa Port Charges tu na kwa utaratibu wa Single custom Territory contena haikai hata hiyo Pot charges ni sawa na hakuna,Mizigo Ambayo ni 4 Home consumption imepungua but sio sana na ndio Maana tuna collect kama Nchi, Waliokimbia watumiaji wa Ndani si kwa sababu eti kodi kubwa walikuwa hawalipi kabisa kodi but nina ukakika watarudi mdogo mdogo,

Nchi hii ipo kwenye Transition watu walizoea hela za wiz kuanzia Kwenye kupitisha kontena Bure,Vikao watu walikuwa wanaenda kufanyia nje na ni watumishi wa Selikari kwa mwezi mtu anaingiza Mil 30 Kwenye Harmashauri hela zilikuwepo watumishi hewa wanalipwa watu kwa mwezi hao mjumuiko wa wizi wote hela ilikuwa unaingia mtaani kwenye matumizi na inaonekana wasomi wanaita Multiplier Effect mi sijui tho ni ya Hela za Magumashi mwisho wa siku watu wana hela Selikari haina hela Miradi unakufa watu wanatanua kwenye mabaya, Leo unaona impact za kubanwa hotel zinafungwa jiulize kwanini Nimesikia Snow view Crest na Mount Meru Arusha zinapigwa Mnada sijui ni kweli na kama ni kweli jiulize kwa nini,

In short run Tutaumia sana But in Long run tutafika Mbali kuna watu wanabeza Tanzania ya Viwanda Haiwezekani itawezekana sasa hivi Nchi ina hela Tunajenga Infrastructure wasomi wanaita ya kuja ku support viwanda Mtandao wa Balabala unamalizikia Nchi Nzima,Reli ya kati Standard Gauge inaenda mpaka Rwanda,Tuna Bomba la Mafuta toka Tanga mpaka Uganda,Hivi vikimalizika tutapiga hatua hata ktk viwanda tujipe mda hapa najua tuna Argue kwa upande mbili ukawa ana interest zake na CCM ana Interest zake hatufanyi Research tunakulupuka tu na ushabiki wa Kisiasa but ndio TANZANIA

Tumuunge Mkono Rais katika kipindi hiki CHA MPITO

ILI MBEGU IZAE LAZIMA IFUKIWE IOZE NDIO ITOE MATUNDA MEMA...
 
IMG-20160904-WA0036.jpg
 
Ukweli unasemwa kila mara tatizo hamkubali. Kumbuka la sukari mpaka tahadhari ilitolewa watu wakatokwa povu kubisha ukweli namkumbuka lizaboni jinsi alivyotoka jasho mpaka la ukucha. Leo nina uhakika ananunua sukari tsh. 3000
Hahaha ule ulikuwa uhuni uliokuwa ukifanywa na baadhi ya wafanyabiashara wasio waaminifu !Unscrupulous businessmen.! Angalia hivi unajua kuna tani zaidi ya 1,000 za sukari zimetelekezwa pale bandarini hazina mwenyewe. TRA na TPA wametoa tangazo la kupiga mnada. Very soon ?? Walidanganya kuwa ni sukari malighafi ya viwanda kumbe ni ya matumizi ya madukani. Hii ndio wafanyabiashara. Tunapotetea tuwe na hoja wajameni.
 
Back
Top Bottom