TPA: Ni kweli Mizigo imepungua Bandarini

TPA: Ni kweli Mizigo imepungua Bandarini

Moro¹One¹ said:
pesa hakuna lakini kampuni yetu imeongeza mauzo, kwa maana bidhaa kutoka nje hakuna kwa hiyo waliokua wanazarahu bidhaa zetu wamekuja kununua...Malengo na nia zinaelekea kutimia.
Kwa nini bidhaa zenu zilikuwa hazinunuliki? Kwa nini bidhaa zenu zilidharauliwa? Kwa hiyo unamshukuru Magufuli kwa sababu wananchi sasa wanalazimika kununua bidhaa ambazo zilidharauliwa na zilikuwa hazinunuliki! Sasa mambo poa kabisa, mnatengeneza hela kweli kweli! Duh, hii mentality kweli ya mwendo kasi, je tutafika?
 
Awamu hii imekosa ubunifu bora enzi za waziri wa fedha Saada Mkuya.
Wanasiasa kuingilia shughuli za uchumi ni hatari sana.
 
Nikuulize mkuu. Hivi hii va unayosema katika kipindi cha awamu ya nne na ya tatu haikuwepo au ilikuwaje. Naomba kufafanuliwa.ni kitu gani baada ya kuingia Magufuli kimebadilika pale bandarini.
Kodi zimeongezeka maradufu kwa wafanyabiashara..Ndio maana hawapitishi tena mzigo bandari ya Dar.
 
Nafikiri ni wakati mzuri wa kubadiri mfumo! Baada ya kusubiri mizigo ambayo haipo, sisi tufanye yafuatayo. 1. Tusafirishe nje malighafi na bidhaa. 2. Tuwekeze viwanda maana bidhaa zitakua adimu sokoni, kwahiyo tuna nafasi ya soko la bure. Ni wakati wa kuitanua nchi ila kwa wavivu wa kufikiri wanazani Sera za Raisi Magufuli zinaferi, lakini Mimi nadhani ni wakati muafaka wa kuimarika ndani ya nchi kwa kila kitu kinachokosekana tutazalisha hapa. Mfano, Mimi mwenyewe nimeona faida, maana pesa hakuna lakini kampuni yetu imeongeza mauzo, kwa maana bidhaa kutoka nje hakuna kwahiyo waliokua wanazarahu bidhaa zetu wamekuja kununua, ingawa kwa kiasi kidogo, lakini Malengo na nia zinaelekea kutimia. Namsifu Magufuli kwa maana katika shida tulio nayo sasa, tunaona tumaini la Kiwanda chetu kukua. Tujiamini watanzania, ni wakati wa sisi kuzarisha.
mnazalisha bidhaa gani?
 
Sijaangalia taarifa ya habari leo ila kamati haiwezi kuhoji TRA eti mnapata wapi fedha za kodi wakati hakuna mahali ktk nchi ambako hapaingizi mapato.

kodi inalipwa tena kwa sasa maeneo mengi kodi na malipo yasiyokuwa ya kodi yanalipwa kwa njia ya mtandao na wizi umepungua sana na mapato yamepanda sana.

Hayo ya TPA wenye mamlaka watatoa taarifa kama kuna shida.

Naomba tuwe na positive thoughts itatusaidia ktk kujenga nchi yetu
Wenye mamlaka TPA ni pamoja na Kamati ya bunge...Na hiyo ndio taarifa wameitoa
 
Halafu kuna watu wakiambiwa ukweli utasikia ooh wanakwepa kodi akili zingine za kijinga toka tani elfu 40 mpaka tani 1000 si hatari hiyo..kisha TRA wanakuja na mbwembwe za kukusanya kodi kwa 98.9% sijui kama wana mapenzi mema na nchi hii au ni kumfurahisha boss wao
Unataka wakose kaziiiiii
 
Yap,ndo maana nikasema wabunge wangeshauri vyema kuhusu hilo katika kikao cha bajeti kilichopita basi mawaziri wangefikisha ushauri huo kwa Rais ila kama waliona hakuna tatizo wasibebeshe mzigo huo watu wengine ila waseme tu kila mmoja hajafanya kile kinachotakiwa.
hukumsikia kafumu anasema walipeleka mpaka mapendekezo yakakataliwa
 
Mwengine alikua biased akasema hataki watalii maskini nasubiri matokeo yake, wana shingo ngumu kwenye ushauri mpaka yawafikie tuu.
waziri wa utalii alishasema watalii wameongezeka sana pamoja na ongezeko la VAT[emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1]
 
Upinzani uliposema wakaonekana wanawatetea wakwepa kodi, jamaa akasema asiyetaka na asije, jamaa akatuaminisha watz kuwa anaweza kushindana na njaa na akashinda watz tukamuachia uwanja yetu macho tunasubiri nani atainuka kidedea lakini juzi Kati mmoja kaanza kulalamika uchumi umechoka watu wameficha noti kwenye makabati
Ushaaambua uchumi unakuwa,huo wa kushuka unaotoa wapi
 
Mkuu hujuwi?

Hii ni awamu ya mambo ya hewa

wanafunzi hewa

wafanyakazi hewa

MAPATO HEWA...Tra

mauzo hewa
Duhhhh kumbeeee maaapatooo nayo ni hewaaaaaa,eeee baba wa mbiguni,Mungu mkuuu tusaidie wanao tunaangamia kwa kukosa maarifa[emoji24] [emoji24] [emoji24] [emoji24] [emoji24]
 
Hivi kiongozi ukiwa unaogopa kumshauri boss wako kuna umuhimu gani wa kufanya kazi kama mshauri na je unakuwa na mapenzi mema na nchi yako maana Rais siyo mungu anakosea na anatakiwa aelekezwe.
Nalinda kazi yangu,nina familia inanitegemea
 
jamaa kaua uchumi wa nchi kwa kutaka misifa,iwe funzo kwa watanzania sikila mtu anaweza kuwa rais wa nxchi,na haya ni matokeo ya kupambana na wafanya biashara,leo maskini wanaanza kulia
 
Eventually tutarudi na kukubali wataalamu wetu ni tia maji tia maji; watu wameshauri sana na kutoa prediction zao humu what would happen na sera zao za kodi these fools do not know nothing kuhusu Tanzania economics challenges and the appropriate remedies needed; probably they are more concerned jinsi ya kuhudumia deni la nchi na sera uchwara wanazopewa na IMF lakini ubunifu wao wenyewe sifuri.
 
Back
Top Bottom