TPA: Ni kweli Mizigo imepungua Bandarini

TPA: Ni kweli Mizigo imepungua Bandarini

Kwa kiwango changu kidogo cha uelewa nadhani Kodi kubwa kwenye biashara hulia ni kikwazo cha mapato. Mfano kuna msululu wa maduka sehemu moja alafu wewe ukaongeza bei ya vitu ukatarajia kupata faida kubwa ili utajirike mapema matokeo huwa Wateja kupungua na kwenda kwenye maduka ya jirani yenye bei ndogo. Hivyo ili tufanikiwe inabid tuweke kodi walau ya chini kidogo kuliko wenzetu katika biashara zetu zote na utalii halafu tusimamie kwa uadilifu makusanyo na matumizi yawe yale yenye tija kwa nchi yetu. Na wananchi tujitume kufanya kazi za kutuongezea vipato na tupunguze matumiz ya anasa. Nchi yetu nahisi itastawi. NCHI YETU ITAJENGWA NA SISI WENYEWE.
 
Endeleeni kupika data Muda utatoa majibu yote
 
Alikosea sana aliemshauri hayo Madudu ya aina za kodi Wazambia wanaonunua mizigo nje wana chama chao tutoe hayo madudu ya VAT katika transit goods ndipo wafuatwe hao na Wazimbabwe waje wapitishe magari yao tuu tupate hizo gharama za bandari zilizokuepo hapo nyuma hili hakiitaji hata shule SA kusikia tuna VAT wao wakapunguzana gharama zingine sasa wanapitishia Durban ila usalama ni kidogo kuriko Dar es salaam wakati Nchi zingine bidhaa bora na nzuri kitu cha kawaida tuu Tanzania kila kizuri ni Anasa tuu kodi juu...
 
Yupo wapi yule mteteaji wa Serikali na CCM JF....? Kila Post alikuwa Anakommenti
 
Magufuli ni kiongozi makini sana..Mizigo imepungua lakini mapato yameongezeka....bora uwe na mizigo michache lakini ilipiwe kodi...
 
Magufuli ni kiongozi makini sana..Mizigo imepungua lakini mapato yameongezeka....bora uwe na mizigo michache lakini ilipiwe kodi...
Ilikuwaje katika post moja akachagua zaidi ya mtu mmoja au ndani ya mwezi mmoja unabadilisha/ kutengua uteuzi.
 
Mkuu sialisema bora tupate mizigo kidogo lakini tukusanye kodi.

Kulikoni tena hataki tena mizigo kidogo.
 
Muda huwa ni muamuzi mzuri, watu wakisema kwamba hii serikali inajitekenya yenyewe wanaambiwa ni wachochezi, Hatari kubwa tuliyonayo ni kuwa na viongozi ambao wanalinda vyeo badala ya kuvitumikia vyeo vyao, sasa unajiuliza MTU anapika data za mapato ili nini sasa,Serikali hii naona inashindana na serikali iliyopita kwamba ni ipi inafanya vizuri ukilinganisha na nyingine ndo maana hzi data zinapikwa. Ukweli ni kwamba kwa MTU mwenye akili ukitizama ile budget iliyopitishwa unaona kuwa haitupeleki kokote, tulihitaji sana mawazo na michango ya wapinzani katika ila budget ila kwa bahati mbaya wabunge wa ccm waliamua kufanya walichofanya, badala ya bunge kuwa sehemu ya kuapambanisha hoja ili tupate njia itakayo tupeleka pale ambapo jicho la kila mtanzania mpenda maendeleo linapatizama imekuwa ni sehemu ya kuilinda serikali. YAANI IKITOKEA UMEONA MAENDELEO TANZANIA UJUE YAMETOKEA TU SABABU WAKATI WAKE UMEFIKA NA SI KWAMBA YALIANDALIWA KUTOKEA.

Well said,ni kweli wanalinda vyeo vyao na si kuwajibika inavyotakiwa.Time will tell.
 
Uchumi wa viwanda!

Mwekezaji gani (wa viwanda) sensible atakuja kuwekeza Tanzania (kwa hali kama hii)?
- Meli zikipungua, export na import inakuwa ni ya gharama kubwa sana
- Umeme na miundombinu mingine mibovu/haitoshi
- Kodi nazo ndio hivyo tena

Nini kitawavutia wawekezaji? Amani? Demokrasia? Hii ya polisi na jeshi?

Tunahitaji kuisadia nchi yetu. Viongozi wetu wafungue masikio ili nchi yetu ipone.
 
Tunataka wingi was mizigo au makusanyo zaidi?
Enzi hii ya Magufuli wakwepa kodi lazima wayeyuke. Watabaki wachache wafanyabiashara halisi. Yuko wapi Home Shopping Centre ambaye alikuwa ndiyo bandari na TRA mwenyewe?
Sishangai kusikia mizigo ya Congo kupungua. Huenda ilikuwa chaka la kukwepa kodi tu lakini mizigo iliishia Kariakoo! !
Mwezi July pekee kwa mara ya kwanza, Vodacom wamelipa excise duty ya 1.7 billion badala ya million 350! Tigo nao zaidi ya 1.2 billion badala ya million 250!
Kwa mwaka mzima Vodacom na Tigo watalipa kiasi gani? Kwa trend hiyo, haitapungua billion 45. Hayo ndiyo mapato yote ya SMZ kwa Mwezi mzima.
Na Mitandao ya Airtel, sasatel na ttcl vip? Makusanyo yao. Maana siamini viwango vidogo vinavyokusanywa na makampuni ya simu apa Tanzania. Mfano mdogo kwamba kalibia kila kijana aliyefikisha miaka 18. Anatumia simu, Leo hii mapato kodi yake inadhidiwa na sigara na bia kitu ambacho Watumiaji wake ni asilimia chache sana
 
Back
Top Bottom