TPA: Ni kweli Mizigo imepungua Bandarini

Hahaha.,.mkuu mtu akikusoma between the lines atakuelewa Sana,,......so what is the way forward?
 
Mweeh!kweli ccm inapaswa kujilaumiwa kwa kueneza ujinga TZ hi..yani kwa akili yako tani 1000 ndo zinaongeza mapato
wewe kunakitu huelewi...

Hela inayo kusanywa sasa inaonekana na inatangazwa wazi

wewe hiko kipindi cha tani 40000 ilikua unayajua mapato
 
Juzi kati kuna huyo boss wa bandari alisema...bandari mambo safi mizigo ni mingi....leo wamekanusha..
Alikuwa anatudanganya sisi wananchi na muheshimiwa raisi pia kwa vile huangalia taarifa ya habari! Kama angejuwa namna uheshimiwa mpendwa wetu anavyochukia kudanganywa, angelikwisha nunua jeneza tayari!
 
Nikuulize mkuu. Hivi hii va unayosema katika kipindi cha awamu ya nne na ya tatu haikuwepo au ilikuwaje. Naomba kufafanuliwa.ni kitu gani baada ya kuingia Magufuli kimebadilika pale bandarini.
 
Duu nawe umekuja na Kali ya mwaka!umejibu kisiasa,hujasikia bosi wa bandari anakiri mizigo kupungua,icd kuikosa mizigo?
Mkuu ina maana huyu jamaa anaendeleza propaganda na Porojo hadi muda huu? Hajaangalia taarifa ya habari? Jamani siasa kwenye mambo ya msingi tuyaache.
Tuwe wakweli, huo ndiyo uzalendo. Hali iliyofikia bandari kuendeleza propaganda hakutasaidia chochote. Hali ni mbaya halafu mbaya zaidi bado kuna watu wanatetea ovyo kabisa

Kuna jambo moja limenishtua kidogo, Dr Kafumu(kama sikosei) wakati akiwa bandarini anakiri kuwa kamati yao ilishauri kuhusu VAT ya Benki na Miamala ya Simu ila anasema, USHAURI WAO HAUKUCHUKULIWA.

ninavhoweza kucoment kama ni kweli basi Bunge la Mwez huu Wabunge waondoe dosari zote. Kuna mambo mengi yanatakiwa kuboreshwa.
 
wewe kunakitu huelewi...

Hela inayo kusanywa sasa inaonekana na inatangazwa wazi

wewe hiko kipindi cha tani 40000 ilikua unayajua mapato
Uwe unaangalia na makodi yaliyozidi kwa wananchi. Leo hii kila kitu juu alafu unashangilia pato kuwa juu
 
Tatizo sio kupungua mizigo bandarini, ishu hapo ni kodi. Wapo waliozoa kupiga dili, kupitisha mzigo bila kulipa kodi, bora kuwa na mizigo michache inayolipiwa kodi
 
Mizigo hamna wa Zambia na wa Congo wanpitia Msumbiji wafanyibiashara wa kwetu wanashindwa kuagiza maana kodi i akusanywa kwa nguvu sasa kutakuwaje na mizigo.
Ungeshauri kodi ikusanywe kwa kubembelezwa eti kamanda. ?? Basi sawa. ! Ni hayo tu
 
wewe kunakitu huelewi...

Hela inayo kusanywa sasa inaonekana na inatangazwa wazi

wewe hiko kipindi cha tani 40000 ilikua unayajua mapato
Si bora hela ikusanywe kidogo lakini maisha yawe mepesi kwa wananchi. Kuliko kukusanya pesa nyingi alafu watu mlo mmoja tu shida
 
Uwe unaangalia na makodi yaliyozidi kwa wananchi. Leo hii kila kitu juu alafu unashangilia pato kuwa juu
Hakuna kodi mpya..

kodi zilikuepo sema zilikua hazifuatiliwi.
 
Si bora hela ikusanywe kidogo lakini maisha yawe mepesi kwa wananchi. Kuliko kukusanya pesa nyingi alafu watu mlo mmoja tu shida
ndugu yangu unafanya kazi wapi?

au umejiajiri?
 
Ningependa wabunge watoe mawazo yao kama kuishauri serikali kwa suala hili. Ndio kazi yao ya msingi. Na we hope wakiondoka pale basi tutaona mabadiliko chanya pale.Mungu ibariki Tanzania
 
Si bora hela ikusanywe kidogo lakini maisha yawe mepesi kwa wananchi. Kuliko kukusanya pesa nyingi alafu watu mlo mmoja tu shida
Kamanda una maana hela ikusanywe kidogo na nyingine iende mifuko! mwa watu mojakwa moja ili watu wakafaidike na wizi huo mtaani au siyo. Kuliko serikali kukusanya mapato yote bila kuachia wizi ufanyike kidogo. Haya ndio mawazo yako kamanda. Basi sawa !! Safi sana. Umesoma mpaka la ngapi wewe
 
Hao waliovujisha hii siri wanataka kutushitaki kwa wananchi hiiiiiiiii
 
Wale vyura wa lumumba wako wapi sasa waje watoke povu?
 
Wamshauri Raisi....? Amewataka ushauri....??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…