TPA: Serikali haijaipa DP World Kandarasi ya undeshaji Bandari ya Dar es Salaam kwa Miaka 100
Waarabu ni magaidi na waharibifu hawafai kukaribishwa nchini kuwekeza kwenye uti wa mgongo wa uchumi wa nchi yetu
 
Eti miezi 12, which for what? Dili lishavurugika kiufupi TOP MANAGEMENT ya hii nchi wamesha kubali kuwa

hawawezi tafuta hela ndani ya hii nchi,na wakaona hata kama wakiendelea kukopa madeni yakua ya miaka na miaka

what to do? tugawe moja ya tulichonacho kisha kupitia hicho tutapata hela (kuna lijinga limepeleka hli wazo watu wakalipokea) wazo limeonekana BORA mchakato ukaanza.

Jinga lingine likaropoka "BANDARII" Mijitu ikaangaliana ikaunga hoja mkono,BANDARI ikapita,mchakato ukaanza wa nani apewe ,Katika woteee jinga lingine likaropoka "DUBAI" Watu wakaunga HOJA.

Kikao kikaisha,watu wameachana Kikao kikavuja,Mzigo RAIA wote tushajua kinachoendelea... Hamna kukanusha/kupinga/kukataa lisemwalo lipo tena hili sio lisemwalo ila ndio ukweli uliopo.

Sema mvujisho Huu kuna watu washapoteza kazi huko eti ...
 
Mkataba Kati ya Serikali ya Tanzania na kampuni ya DPW ya Emirates Dubai umeacha maswali mengi na kuamsha hisia za kudai Katiba mpya kwa nguvu zote.

Ni mkataba ambao ulisainiwa kwa mwendokasi bila kuchukua tahadhari juu ya madhara yake yaliyo dhahiri. Mkataba huu haukubaliki kwa sababu nyingi Sana.

Moja , ni mkataba wa milele kwa sababu hauna ukomo. Najua wapo waliosema ni wa miaka 100 na wapo waliosema ni wa miezi 12.

Hawa wote sijui wametoa wapi huo muda wa mkataba. Ibara ya 23 ya mkataba na randama zake (appendixes) zake hakuna popote zinaonyesha mkataba huu ni wa muda gani. Hii inaweza kutafsiriwa kuwa ni mkataba wa kudumu.

Ni kweli unaweza kuwa miaka mia lakini pia hakuna Cha kuzuia uwe wa miaka 1000.

Pili, mkataba huu unanguvu kuliko Sheria za Tanzania pamoja na Sheria za kimataifa ( Takes precedent over national and international law)

Mathalani Ibara 23( 4) hairuhusu kuvunja mkataba huu hata pakiwa na ukiukwaji mkubwa ( material breach) au kukitokea hali inayopelekea mkataba usitekelezeke ( fundamental change of circumstances) ambalo ni Takwa la mkataba wa kimataifa uitwao Vienna Convention on the Law of Treaties,1969 ambao Tanzania imejifunga nao.

Sasa hii tafsiri yake ni kwamba baada ya kusaini mkataba huu hata Dubai wakikiuka kabisa hatuwezi kujitoa. Hicho ni kitu Cha ajabu mno dunia itatushangaa.

Mbaya zaidi mkataba hausemi je una nafuu ili mbadala ukiachilia mbali kuvunja mkataba.

Kifungu Cha 23( 4) kinaenda mbali zaidi na kusema ikitokea sababu yeyote inayotambulika kwenye Sheria za kimataifa ya kupelekea kuvunja mkataba bado mkataba huu hautavunjwa.Tafsiri yake ni kwamba tumeingia kwenye shimo ambalo halina pa kutokea( coup de sac) .

Tatu , mawanda ( scope ) ya mkataba pia ni mapana, ni Kama hayana ukomo. Ibara ya 2(1) itaruhusu muwekezaji kujenga na kuendesha miradi ya bandari za Bahari na maziwa yote.

Mkataba unakwenda mbali zaidi hata kwenye kile kinachoitwa logistic parks na trade corridors ambazo bahati mbaya hazijatafisiriwa kwenye mkataba.

Kwa namna mkataba huu ulivyo sisi tutakuwa tumepoteza udhibiti wa bandari zote za bahari na maziwa yote.

Mkataba ungeweka wazi ni bandari zipi hasa kwa sababu kwa namna ya Sasa hata usalama wa nchi unaweza kuwekwa rehani.

Nne , mkataba hausemi sisi tutapata nini( consideration) kwa maana ya faida za mradi. Je sisi tutakusanya Kodi tu? Au tutakuwa wabia?

Tano , mkataba hauonyeshi nafasi ya mamlaka ya bandari( TPA) ni ipi katika uendeshaji wa mkataba. Kumbuka kwa mujibu wa sheria TPA ndo chombo chenye mamlaka ya kuendesha bandari zote. Sasa je mkataba huu umefuta sheria hiyo? Kwa mamlaka gani?

Mkataba hauelezei kuhusu usalama wa mapato yetu bandarini na nafasi ya vyombo vya ulinzi na usalama kwaajiri ya usalama wa nchi yetu hasa kwenye marine.

Nafasi pekee ya TPA kwa mujibu ya randama ya kwanza imeachiwa kuendesha na kusimamia " DHOW AND WHARF TERMINAL" ya bandari ya Dar es Salaam.

Sita , pamoja na kuweka kipengele Cha local content ili kunufaisha wazawa kwenye ajira na manunuzi kwenye ibara 13( 2) ibara hiyo haina maana yoyote Kwanza kwa sababu haiweki wazi kwamba threshold ya wazawa kwenye ajira itakuwaje.

Pili hata procurement( manunuzi) ya vitu au items au huduma zinazopatikana ndani hailindwi na mkataba kwa sababu kwa mujibu wa ibara ya 6(2) ya mkataba huu serikali yetu hauruhusiwi kufanya usumbufu wowote (interference) yoyote hata kwenye manunuzi yanayokiuka Sheria isipokuwa tu Kama yanahatarisha usalama( safety and security).

Sasa je wakiamua kuagiza mbao Dubai wakati hapa nchini zipo utawazuia kwa kigezo Cha usalama?

Saba , mkataba hausemi nani atawajibika kulipa fidia yoyote inayotokana na utekelezaji wa mradi pamoja na watumishi ambao ajira zao zinaweza athiriwa na mradi.

Nane , pamoja na kwamba ibara ya 26 ya mkataba inaelekea kuruhusu reservation utagundua kwa namna ibara ya 24 ilivyo imepoka kwa mkono mwingine haki ya reservation iliyopo kwenye ibara ya 26 hivyo sioni uwezekano wa nchi yetu kufanya reservation kwenye makubaliano bila kukwaza mkataba.

Kwa namna ya mkataba huu tukifanya reservation Sasa ivi inaweza kupelekea nchi iingie kwenye mgogoro wa kukiuka mkataba.

Tisa , hata kuridhiwa kwa mkataba huu na Bunge tayari umefanyika nje ya muda.

Ibara ya 25(2) ilitaka mkataba uridhiwe ndani ya siku 30 tu na leo ni zaidi ya miezi Saba.

Kumi , kwa mujibu wa ibara ya 8(3) (c ) mkataba huu ni kama unatoa umiliki wa ardhi kwa mwekezaji kinyume na Sheria ya ardhi.

Kwa mujibu wa sheria ya Ardhu Sura ya 113 Kampuni ya kigeni hairuhusiwi kumiliki ardhi Tanzania.

Tulitegemea mkataba useme ardhi zitakuwa chini ya TPA au mamlaka nyingine za serikali na wao watapata derivative rights badala ya kuwapa ardhi kwa mgongo wa lease hold.
 
Aisee Uanasheria ni mgumu Kuliko udaktari
 
Na awamu hii wasipoangalia hakuna kitu watafanikisha,, wananyenyekea kupita kiasi,, JPM alikua akiamua kitu, alikua hasikilizi kelele za mitandaoni, leo hao hao waliomchamba, wakiona miradi yake inakamilika wanarudi kumsifia
 
Tarehe 5 Juni 2023, Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lilitoa Taarifa kwa Umma kuhusu mwaliko wa Wadau wote kutoa maoni kuhusu Azimio la Bunge la mapendekezo ya Kuridhia Makubaliano kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania a Serikali ya Dubai kuhusu ushirikiano wa Kiuchumi na Kijamii kwa ajili ya Uendelezaji na Uboreshaji wa Utendaji Kazi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania la Mwaka 2023.

Kufuatia Taarifa hiyo kwa Umma iliyotolewa kupitia tovuti ya Bunge, kumekuwa na upotoshaji katika mitandao ya kijamii kwamba "Serikali imepanga kuipa kampuni ya DP World ya Falme ya Dubai kandarasi ya undeshaji wa shughuli za Bandari ya Dar es Salaam kwa muda wa miaka mia moja (100)".

Kufuatia kusambaa kwa taarifa hizo, Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) inapenda kuwajulisha Wateja, Wadau wa Kitaifa a Kimataifa na Umma kwa jumla kwamba, taarifa hizo sio sahihi, ni upotoshaji unaofanywa kwa makusudi na watu wenye nia ovu ya kukwamisha mipango thabiti ya Nchi katika kuongeza ufanisi wa Sekta ya Bandari Nchini kwa maslahi mapana ya Taifa.

Taarifa sahihi ni kuwa, Azimio la Bunge linahusu Mkataba ambao Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaingia na Serikali ya Dubai wenye ukomo wa miezi kumi na mbili (12) kwa ajili ya kutoa nafasi kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kujadiliana na Serikali ya Dubai kuhusu maeneo ambayo Serikali hizo mbili zinaweza kushirikiana katika boreshaji na endelezaji wa Sekta ya Bandari Nchini Tanzania.

Ushirikiano wa Nchi mbili za Dubai a Tanzania una lengo la kongeza ufanisi wa huduma za Bandari Nchini, kukuza ajira za Watanzania na kufungua fursa za kiuchumi na kijamii kupitia uwekezaji kwenye baadhi ya maeneo ya Bandari ya Dares Salaam, maeneo huru ya kiuchumi na viwanda (Special Economic and Industrial Zones) kwa kujenga viwanda pamoja na uwekezaji katika mnyororo mzima wa usafirishaji kutoka Bandari za Tanzania kwenda chi za jirani ambazo zinatumia Bandari zetu.

Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) inawaomba Wateja, Wadau na Umma kutambua kwamba, jitihada zote na hatua zinazochukuliwa na Serikali ya Awamu ya Sita katika kuvutia wekezaji Nchini hususan kwenye maeneo ya Banadari, zinalenga kumaliza changamoto za muda mrefu ikiwemo ucheleweshwaji wa meli, mizigo na kukosekana kwa ufanisi katika Bandari zetu.

View attachment 2648437View attachment 2648438

Pia soma: Tanzania inatarajiwa kuingia mkataba na kampuni ya DP World ya Dubai kuendeleza Bandari ya Dar es Salaam
Wewe Mkurugenzi wa TPA unajaribu kutufanya sisi wote ni wajinga siyo?

Hapa hatujadili azimio la bunge...!!

Kinachojadiliwa hapa na kilichozua taharuki kwa wananchi ni mkataba wa makubaliano wenyewe ambao tayari uko wazi na watu wameshausoma na kuona kila kitu..

Mkataba wa makubaliano hayo, hayafai na hayalengi kwenye hicho pekee kilichoelezwa katika azimio la bunge. It goes beyond that...

Kwa kifupi sana, Wazanzibar hawa (Samia Suluhu Hassan, Hussein Mwinyi na Makame Mbarawa) wanataka kutuharibia nchi yetu ya Tanganyika..

They must go!!
 
Watu wanabishana. Mpaka Lissu kasema. Kwa mara ya kwanza Lissu hakusema mkataba wa miaka mingapi. Kaishoa kusema sio wa miaka 100. Kalamba asali?

IMG_7523.jpeg

Wataalamu. Mkataba ni wa miaka mingapi?
 
Huo mkataba hauna kipengele cha duration, badala yake kuna kipengele cha confidentialty, maana yake ni kwamba, hiyo duration ndio wameenda kuificha kwenye confidentiality, ambapo wanataka sisi wakina third parties tusijue lolote.

Hiyo ndio sababu utakuta wapo wanaouliza, mbona miaka mia haionekani? nao wakiulizwa kwa swali, nyie mmeona mingapi, nao kimya!, maana yake tumefichwa kipengele cha muhimu sana kwenye ule mkataba.
 
TPA haina uwezo wa kulisemea jambo hili, acheni kujipendekeza, hili msemaji wake ni lazima iwe Serikali yenyewe.

Kwanza nyie TPA kila siku mnatimuliwa na wanawekwa watu wapya mnawezaje kuwa wasemaji wa Jambo la Kitaifa?
Kibunda cha waarabu kimewafikia pia hapo TPA waache wakanushe tu.
 
Hiyo ndio sababu utakuta wapo wanaouliza, mbona miaka mia haionekani? nao wakiulizwa kwa swali, nyie mmeona mingapi, nao kimya!,
Ujinga ni adui mbaya sana, wamefichwa na kwa ujinga wao wanatetea mkataba huo.
 
Back
Top Bottom