TPDC: Gesi ya Mitungi tunayotumia Nyumbani kwasasa yote inatoka nje, bei yake hupanda kulingana na bei za mafuta duniani

TPDC: Gesi ya Mitungi tunayotumia Nyumbani kwasasa yote inatoka nje, bei yake hupanda kulingana na bei za mafuta duniani

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Mussa Mohamed Makame amsema, Gesi ya mitungi tunayotumia majumbani kwa sasa yote inatoka nje, bei yake hupanda kulingana na bei za mafuta duniani.

"Gesi, nyingi ambayo tunatumia majumbani ni ile ya kwenye mitungi (LPG). Ni tofauti na gesi asilia ambayo sisi tunaisafirisha kwenye mabomba na kupitia njia ya CNG na LNG. Ile inatokana na uzalishaji wa mafuta, na kwasasa, kwasababu hatujaanza uzalishaji wa mafuta, ile gesi yote inatoka nje.

Kwa hiyo kwasababu inatoka nje, bei yake mara nyingi inacheza kulingana na mwenendo wa bei za mafuta duniani. Kwa katika kipindi hiki kwa mfano tangu vita imeanza, tumeona kwamba bei ya LPG ile imepanda."

Soma: Uharibifu wa mazingira kupitia ukataji miti hovyo ni tishio kubwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Chunya - Mbeya

Duh kumbe mpaka TPDC kawekwa mpemba...
 
Watanzania wakija kujua hata hiyo gesi inayoitwa ya Mtwara bado serikali inainunua toka kwa wazungu sababu wao ndio wanaitafuta, ichimba na kuisogeza nchi kavu...
 
nimekupa nakala ya hansard ya bunge, inaonesha kuna nyumba zimefungiwa , hustuki unavosema hawezi tumika jikoni?

hadi hawa wawe wapo chaka?

mkuu huna taarifa, nachoongelea mimi ni kwamba kuna watu wa majumbani wachache tayari wamefungiwa, ila kwenye muendelezo wa ufungaji ndo taarifa hakuna
Kuna visima tofauti vya gas huko mtwara,kuna ambayo italetwa majumbani kwa mabomba,kuna hiyo iliyoanza kuchimbwa muda ambayo ni CNG siyo kwa matumizi ya nyumbani
 
CNG inatumika jikoni hiyo mikocheni kuna nyumba kibao za wadosi wanatumia kikubwa kuwe na pressure Regulator. Nimehusika kuweka meter kwenye baadhi ya nyumba chini ya Gasco
shukrani sana mkuu, emu tupe muhtasari hii hali ya ufungaji inaendeleaje, maana naona msukumo ni mdogo sana, kikwazo kikuu ni nini
 
Kuna visima tofauti vya gas huko mtwara,kuna ambayo italetwa majumbani kwa mabomba,kuna hiyo iliyoanza kuchimbwa muda ambayo ni CNG siyo kwa matumizi ya nyumbani

mkuu mimi sina utaalamu na mambo hayo ya gesi, mimi kama mwananchi nafatilia hotuba za serikali na taasisi zake.

hiyo gesi ya mtwara inayoongelewa toka kipindi hiko mambo itakayo fanya ndo kama vile kufua umeme, ku-power viwanda na pia matumizi ya majumbani. na kuna nyumba watu wameshaungiwa, sasa ukisema sio kwa matumizi ya nyumbani sikuelewi, unless uweke wazi kwamba unatetea serikali kwa njia yeyote ile



hemu soma majibu haya ya naibu waziri wa nishati kwend akwa mbunge, hansard ya bunge hiyo may 18 2026

1790064178455.png


hilo swali namba 284 nimehighlight na bluu hapo , naibu waziri anasema nyumba 2512 zimefungiwa miundombinu ya gesi hadi kufikia mwezi april mwaka huu, na kataja idadi katika kila mkoa katika mikoa ya Mtwara , Lindi, Pwani na DAr
 
Nchi ka kiafrika kwao kuimport ni biashara nzuri ,ilq kuanzisha vyao ...Kama pale Kariakoo ni ufahari mtu kuingiza kontena za nguo na vifaa ila haweza kuanzisha kiwanda hata kama anao mtaji.

Hizi ni biashara za uchuuzi ,zinaendelea kulifanya taifa kuwa tegemezi..Leo pakitokea tu hata vita kubwa tunaathirika kweli kweli.
Ndugu yangu kuna kitu gani tunaweza watu weusi? Sisi ni consumers mpaka dunia itakapoisha. Ni watu wa hovyo kupata kuumbwa.
 
mkuu mimi sina utaalamu na mambo hayo ya gesi, mimi kama mwananchi nafatilia hotuba za serikali na taasisi zake.

hiyo gesi ya mtwara inayoongelewa toka kipindi hiko mambo itakayo fanya ndo kama vile kufua umeme, ku-power viwanda na pia matumizi ya majumbani. na kuna nyumba watu wameshaungiwa, sasa ukisema sio kwa matumizi ya nyumbani sikuelewi, unless uweke wazi kwamba unatetea serikali kwa njia yeyote ile



hemu soma majibu haya ya naibu waziri wa nishati kwend akwa mbunge, hansard ya bunge hiyo may 18 2026

View attachment 3675560

hilo swali namba 284 nimehighlight na bluu hapo , naibu waziri anasema nyumba 2512 zimefungiwa miundombinu ya gesi hadi kufikia mwezi april mwaka huu, na kataja idadi katika kila mkoa katika mikoa ya Mtwara , Lindi, Pwani na DAr
 
  • Kicheko
Reactions: Lax
shukrani sana mkuu, emu tupe muhtasari hii hali ya ufungaji inaendeleaje, maana naona msukumo ni mdogo sana, kikwazo kikuu ni nini
Kikwazo kikuu ni miundo mbinu ndio maana hadi sasa ni sehemu chache tu wameunganisha majumbani. Mpaka sasa mteja mkuu wa hiyo gesi ni Tanesco, Viwanda vya cement, Dangote
 
Back
Top Bottom