TRA imekusanya Trilioni 11.11 kuanzia Julai hadi Desemba 2021 na trilioni 2.51 Desemba 2021 pekee

TRA imekusanya Trilioni 11.11 kuanzia Julai hadi Desemba 2021 na trilioni 2.51 Desemba 2021 pekee

Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa na Kamishna Mkuu wa TRA, mamlaka hiyo imevunja Rekodi ya kukusanya Kodi kiasi cha Shilingi Trilioni 2.51 kwa Mwezi Desemba 2021 ikiwa ni kiwango cha juu kabisa kukusanywa katika Mwezi tangia kuanzishwa kwake. Katika kipindi cha Desemba 2020, TRA ilikusanya pungufu ya kiasi hicho kwa asilimia 20. Aidha Makusanyo kwa miezi 6 iliyopita ni Shililingi Trilioni 11.11 ikilinganishwa na Trilioni 9.24 zilizokusanywa kwa kipindi kama hicho mwaka 2020.

Pongezi kwa Mhe. Samia, pongezi kwa Kamishna Kidata kwa kutokusanya kodi ya dhulma lakini matokeo yanaonekana. Watanzania lipeni Kodi kwa hiari mjenge nchi yenu.

Kazi Iendelee.

cc: Suzy Elias
Mkuu pamoja na pongenzi ni vyema tukajua vyazo vya makusanyo, ni tozo katika miradi ya ya Kiserikali ama tozo kwa wanachi e.g tozo za kodi za nyumba via luku ama tozo katika miamala ya simu katika shughuli zao za kawaida katika huduma za kijami
 
Swali zuri sana. Drivers za kodi ni biashara au sekta gani hasa.
 
Itoe tilioni 2 iwape ruzuku viwanda vya matrekta wazalishe matreka mengi waje watuuzie wakulima kwa robo bei tuzalishe Sana tuuze tupate mapato kupitia export tuwe na mapesa tele ya kufanya maendeleo bila kukopa.
Mkuu una hoja mzuri lakini haliwezekani! kama mbolea tu ya huyo mkulima ipo juu sana (kutoka 70000/- hadi zaidi 100000/-) sasa itakuwa tractor auzewe robo ya bei. Hayo yatakuwa maajabu ya Dunia.
 
Ukweli ni kwamba mwamko wa watu kulipa kodi umepungua, kwa sasa mambo ya EFD wafanyabiashara hawaogopi tena tofauti na miezi michache imepita. Hayo makusanyo ya kuvunja rekodi yanatoka wapi?

Ni sawa na kusema rushwa imepungua wakati imeongezeka mara dufu. Polisi (hasa wale wa barabarani) siku hizi wanaomba rushwa waziwazi bila kificho, na kwangu mimi hawa jamaa ndiyo kipimo cha rushwa inchini.
Mkuu fedha nyingi nadhani zinatoka via mitandao ya simu.
 
Mkuu una hoja mzuri lakini haliwezekani! kama mbolea tu ya huyo mkulima ipo juu sana (kutoka 70000/- hadi zaidi 100000/-) sasa itakuwa tractor auzewe robo ya bei. Hayo yatakuwa maajabu ya Dunia.
Jifunze kwanza kuhusu neno ruzuku ukielewa inawezekana.
 
Hivi serikali inapoleta taarifa zake huwa mnakuwa wapi? Mbona mnauliza majibu badala ya maswali? Yote unayoongea yamejibiwa na Serikali.

Na mwisho hii dhana mliyobebeshwa vichwani kwamba mkopo wa 1.3 T umejenga madarasa tuu mumepotoka.

Kuna maji,Vifaa tiba,utalii na machinga ila mumekomaa na madarasa tuu.
Toa maelezo....unazungumza Kama wewendio serikali...tunajua fika mkopo wa IMF haukujenga madarasa tu...usijipe ujiko wa kudhani kuwa wewe ndiye unajejua zaidi wakati siyo...hoja iliyopo ni ulaxima wa mkopo huo na matumizi yake...unakopa ili ujenge zahanati, darasa na kadhalika...Jenga uwezo wako...TZ siyo NGO...fahamu hovyo...uzuri ni kuwa wengi wa watz siku hizi ni waelewa...Mimi nimetembelea baadhi ya madarasa hayo na hata zahanati...sasa tukihoji msilete za kuleta hapa.
 
Kwani wewe unaona kulikuwa hakuna ulazima? Matumizi yamefanyaje? Kwani hayajaenda kadiri ya malengo?

Eti ulazima wa mkopo,ndio maana nakwambia muwe mnafuatilia maelezo ya serikali kabla ya kuandika upotoshaji..kama hujui ulazima rejea upya maelezo ya serikali mapovu hayatakusaidia.
 
Mapovu ni muhimu pale serikali isipofanys vizuri...ikifanya vizuri ni muhimu pia kuipongeza...narudia kulikuwa hakuna ulaxima kuchukua mkopo huo wa IMF...hakuna upotoshaji hapa...hatuko hapa kusifu Kila kitu...sisi ni watu waelewa....
 
Hujui Chochote ndio maana hata huelewi kwa nini serikali ikichukua yaani huna maelezo ya ku justify ukosoaji,unabwabwaja tuu.
 
Haaaaaaa, sasa mtu unakopa Trilllion 10 halafu katika kipindi hicho hicho unalipa madeni Trillion 10, na katika hiyo unayolipa kuna mariba lukuki, sasa hii maana yake ni kwamba hatukuwa na haja ya kukopa in the 1st place, hii ni sawa na unakopa pesa ili ukalipe deni, yaani unahamisha deni toka kwa huyu unalipeleka kwa huyu na bado riba juu, huu ni utaahira ?!!!
Unalinganisha vitu visivyofanana

Deni linalolipwa saivi manayake lilikopwa miaka ya nyuma tukiwa hatuna makusanyo kama haya
Pia bajeti yetu inaendeshwa kwa fedha za ndani na za nje.,
Kila fedha ina matumizi yake
 
Nimejaribu kuwawekea na summary ya makusanyo na matumizi plus hotuba lakini hivyo vichwa vimejaa chuki kubwa Sana na Samia

Screenshot_20220102-082208.png

Screenshot_20220101-080116.png
 
Hakuna kitu hapa....majedwali uliyoweka hapa hayasaidii kitu....weka katika lugha nyepesi watu waelewe...hayo matakwimu yako yanaweza kuwa cooked...labda yamechukuliwa kwenye dissertation ambayo nayo pengine ilikuwa cooked....
Fafanua hoja zako kwa lugha nyepesi..
Kwa mfano...Deni la sasa la taifa ni shilingi ngapi...na lilikopwa lini....

Halafu huyo unayemwita mwendazake kwamba alikopa kwenye benki za kibiashara utueleze alikopa kiasi gani na lini..halafu ututajie hizo benki na kiasi kilichokopwa...na masharti yake..
Ur level of illiteracy is shocking!
Unasema asiweke data yet atoe majibu
Unadhani public debt is simple hivyo?
Hizo data kakupa in the very simplest terms zinazotolewa kwa mwananchi walau apate picha in a nutshell
Ukipewa details utakufa wewe kama screenshot 2 zinakutoa roho
Cc The Sunk Cost Fallacy achana na vilaza hawa
 
Hoja ni kusitisha mikopo ya aina hiyo, kama ilikopwa awamu ya 1,2,3,4,5 au 6 haijalishi, tuachane na mikopo ya aina hiyo, maana inatuoeleka shimoni, tutakuja kupigwa mnada tukauzwe utumwani!
Unasitishaje mkopo na ushasaini mikataba na pesa umepewa?

Labda useme ifanyiwe restructuring kuboresha masharti
 
Back
Top Bottom