TRA, inakuwaje ushuru wa kuingiza gari ni mkubwa kuliko bei ya gari lenyewe?

TRA, inakuwaje ushuru wa kuingiza gari ni mkubwa kuliko bei ya gari lenyewe?

Nimetumia kikokotoo cha TRA nimechoka kabisa, ushuru wa kuingiza gari ni mkubwa kuliko bei ya gari yenyewe
Bei ya gari huangaliwa ikiwa mpya.... then mahesabu ya depriciation hufuata... HATA UKIPEWA BURE, KODI UTALIPA... Gari ya mwaka gani? Brand gani? Ikiwa mpya inauzwa shilingi ngapi? Bei ya sasa ni shilingi ngapi? CC ngapi?
 
Hawaangalii umelinunua sh ngapi
Ndio maana kwenye TRA calculator hakuna sehemu ya kujaza bei ya gari
 
Unaweza ku appeal Kama una karatasi halali za ununuzi wa gari. Tax base wanayoitumia tra ndio inafanya Bei kuwa kubwa so Kama Bei ya gari yaani invoice price plus freight Ni ndogo kuliko tax base waliyotumia kwenye kikokotozi unanafasi ya kuappleal
Mkuu ulishawahi kufanya huu mchakato? Appeal unaifanya gari ikiwa wapi? Maana gari ikipakiwa kwenye meli na ukatumiwa documents za gari unatakiwa ufanye pre arrival declaration ikifika gari kwenye ukaguzi ndo wanai uplift hapo mpaka ujibiwe appeal yako storage ya TPA imeshaongezeka
 
Nenda kaangalie Subaru Legacy BM9 ya 2009/2010/2011/2012 uone gari ni $3500-5000 ushuru wake ni 22,000,000-25,000,000 mzee
Achananeni nazo,komaeni na B4 za mwaka 2004
 
Kuweni wazalendo, nunueni nyumbu nimewahi kuyaona kwenye sherehe gani sijui hayana ushuru wa kuingiza
View attachment 1477424
Khaaaaaa...
Hili kweli nyumbu,
Wenzetu tunaopaka nao wote wanatengeneza Magari...

Anyway tujifariji, tupo kwenye top 10, ya nchi zenye magari mengi Afrika,
Haina ubishi hili limechangiwa na Bandari.
 
Unapoambiwa "Afrika ni nchi masikini" huo umasikini ni pamoja na umasikini wa akili!
Hawataki wengi wamiliki magari.
Infact Hakuna sababu sahihi kwann ushuru ni Mkubwa, wanasema ni kuzuia dumping lakini sio sababu ni sababu za kizamani na sio za kisasa.Magari chakavu yote yanakatwa screpa watu wanapima kilo wanauza spea pia vyuma viwandani.
Labda tu Kama limesimama kwenye ile nadharia kuu yaani wafanye wawe masikini ili uwatawale.
 
Kama mkubwa achana nayo nunua trekta halina ushuru kabisa.
 
Back
Top Bottom