TRA, inakuwaje ushuru wa kuingiza gari ni mkubwa kuliko bei ya gari lenyewe?

TRA, inakuwaje ushuru wa kuingiza gari ni mkubwa kuliko bei ya gari lenyewe?

Bei ya gari huangaliwa ikiwa mpya.... then mahesabu ya depriciation hufuata... HATA UKIPEWA BURE, KODI UTALIPA... Gari ya mwaka gani? Brand gani? Ikiwa mpya inauzwa shilingi ngapi? Bei ya sasa ni shilingi ngapi? CC ngapi?
Kodi ya nn wakati gari zinakuja inua uchumi
 
Zambia,Malawi, Mozambique,Uganda Kodi ipo chini.
Sisi hapa nyumbani timechanganyikiwa hata uchangiaji wa mada tu jukwaani hatuijadili mada kila mmoja anakuja na lake.

Huyu analaumu serikali zote za Afrika anashindwa kufuatilia kodi za magari za nchi zingine.

Tukijifunza kutokutolea maelezo mambo tusioyajua itasaidia saana.
 
Decision makers wa nchi hii ndo wanafanya maisha yawe magumu kuliko uhalisia.

Magari yakiwa mengi nchini serikali itafaidika maradufu kuliko kukaba kwenye hiyo kodi ya kuagiza tu ambayo imekwamisha watu wengi tu kumiliki magari ya ndoto zao.

Kuna sekta kibao tu zingekua ikiwa pamoja na ajira kuongezeka.
Wenye akili ya kuamua hawapati nafasi.CV yako ni uwezo wako binafsi wa kusifu na kuabudu ndio cv ya teuzi,hapa upate cream wapi?
 
Wanafanya hivyo ku-avoid tanzania kuwa dumping place
Hoja dhaifu kabisa Tanzania nchi changa bado tunahitaji nondo kwa ujenzi wa miundombinu so hayo magari yakichoka kabisa tunayeyusha kupata nondo
 
Ok sawa ngoja wake wataalamu

Okay, tumefika wataalam.

Tanzania tunathaminisha magari kwa bei ya soko la ndani.

Kama ulinunua IST kwa laki tano Japan tunajua huwezi kuja kuliuza laki nane, bei ya boda boda chakavu, utaliuza milioni nane kwenda mbele.

Kwa hiyo tuna ORODHA YETU ya thamani ya magari kuanzia Nyumbu, DongFen, HongQi mpaka Lambogini, Bugati, Maserati and everything in between.

We don't give a good goddamn if you went to Japan and got it for free! Tax is flat rate.
 
Nenda kwenye point wewe bwege, shule ipi unayoulizia?
Umepaniki mkuu? Ni upuuzi kuleta hoja ya kuokoteza kwamba kodi ikiwa chini magari yatakua mengi hivyo kuharibu barabara wakati asimilia ya magari yanayizungumziwa kua na kodi kubwa ni magari madogo binafsi ya watu...
 
Umepaniki mkuu? Ni upuuzi kuleta hoja ya kuokoteza kwamba kodi ikiwa chini magari yatakua mengi hivyo kuharibu barabara wakati asimilia ya magari yanayizungumziwa kua na kodi kubwa ni magari madogo binafsi ya watu...
Kweli uwezo wako wa kuelewa ni mdogo wapi nimezungumzia kuharibu barabara?
 
Tatizo kubwa ni kwamba kwenye kitengo cha Valuation ya magari wamewawela watu waliotoka shamba hivyo kufanya makadirio makubwa ya magari ya kawaida sasa mtu katoka ileje au misungwi kaja mjini chuo kikuu anaambiwa afanye valuation ya VW Touareg au VW Jetta ya 2009 matokeo yake anafanya kodi ya gari ya CIF $3000-4000 kodi yake ina kua 18,000,000 yani faida kubwa inapata serikali zaidi hata ya wanaouza gari
 
Back
Top Bottom