The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 896
- 1,427
Mtumishi wa TRA aitwaye Amani Kamguna Simbayao ambaye amefariki mchana wa leo December 06,2024 katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili alikolazwa baada ya tukio la shambulio akiwa katika majukumu yake ya kikazi katika eneo la Tegeta kwa Ndevu Jijini Dar es salaam, hii ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na TRA
Taarifa ya TRA inasema Amani na wenzake wawili wa TRA walishambuliwa baada ya kubaini kwamba kuna gari namba T229 DHZ aina ya BMW X6 lililoingizwa nchini kinyemela bila kulipa kodi za Serikali kwa mujibu wa sheria na kuifuatilia kwa lengo la kuikamata ili kuchukua hatua stahiki kwa mujibu wa sheria za kodi.
Sehemu ya taarifa hiyo imesema "Wakati Watumishi hao wa TRA wanatimiza wajibu wao, walihusishwa na kitendo cha utekaji, kilichopelekea wao na gari kushambuliwa",