TANZIA TRA inatangaza kifo cha mtumishi wao, Amani Simbayao kilichotokea leo 06/12/2024

TANZIA TRA inatangaza kifo cha mtumishi wao, Amani Simbayao kilichotokea leo 06/12/2024

malipo ya serikali ya Tanzania kutofuata demokrasia, hali iliyopelekea usalama wa taifa kuzorota huku mamlaka nyingi zikiwa kwenye uchawa na kuacha kusisitiza watumishi wa serikali na polisi kufuata sheria za nchi kutekeleza wajibu wao kutokufuata sheria hizi ni uhalifu
Uchawa utalicost taifa. Tuache dharau na kufumbia macho uvunjifu wa sheria jamani. Hili liwe kama somo kwa serikali kwamba wananchi nao wakiamua kukiwasha inawezekana kabisa kutekeleza majukumu ya kiaskari ambao wanaonekana kushindwa kudhibiti vitendo vya hovyo haswa vikifanywa na mamlaka nyengine za serikali.
 
Big Tarimo alisaidiwa na nani? Nondo juzi katekwa stendi ya Magufuli huku anaomba msaada nani alimsaidia? Mitanganyika ina pick and choose battle za kupambana. Inaua wanaojua hawajiwezi. Hapo waliojua fika hao ni tra na wameona wanataka kamata BMW mitanganyika ikataka sifa za bure.
Big Tarimo kakamatwa mtaani ambako hamna movement ya watu. We unadhani ingekuwa kwenye macho ya watu wangeweza kumfanyia yale bila kudhibitiwa. Mbona wale wa Mwanza walidhibitiwa na raia hadi mkuu wa kituo alipofika kwenye scene.
 
Watumishi wa serikali mnapotumwa kutekeleza majukumu yenu mjitahidi kuchanganya na akili zenu kuepuka kuhatarisha maisha yenu hasa ambao hawavai uniform Kama polisi.Sasa wewe unakamata mtu usiku saatano umevaa kiraia ukizingatia na masuala ya utekaji yalivyozidi inategemea Nini?Ingekuwa mchana angalau kunauwezekano yasingetokea hayo.Ukitumwa changanya na za kwako in kikwete's voice.
 
Hao raia wenye hasira Kali walikua wapi wakati wa mzee Kibao, big Tarimo, Nondo nk waliotekwa kweupe kabisa huku wakiomba msaada? Wanaua watu wanaojua fika sio watekaji huu ni upumbavu wa mitanganyika.
Kira zama na ukurasa wake........ hata hao wengine ipo siku yao........MWENYEZI MUNGU KAWAPA NAFASI YA KUJITAFAKARI...........wasipo rekebisha hilo siku yao yaja........... hata mvua dalili huwa ni mawingu.........na siku ya kufa nyani miti yote hutereza sasa waache waendelee kufanya utumbo wa kutekana waone..............nguvu ya umma haijawai kushindwa hapa duniani toka dunia iumbwe
 
Big Tarimo kakamatwa mtaani ambako hamna movement ya watu. We unadhani ingekuwa kwenye macho ya watu wangeweza kumfanyia yale bila kudhibitiwa. Mbona wale wa Mwanza walidhibitiwa na raia hadi mkuu wa kituo alipofika kwenye scene.

Watu wapo pale wanaangalia au hujaona Ile video?

Nondo juzi katekwa 6am stendi ya Magufuli huku akiomba msaada alisaidiwa na nani?
 
Kule ilibidi wote waishe akiongozwa na "I hate death" , abakie Kishimba, Mpina na Kasheku tu.
Nimesikia huruma sana kwa huyu dogo,kuna kitu kinaniambia kwanini ajali ya wabunge wa ccm waliopata ajali asubuhi hawakuondoka angalao saba kufidia roho ya huyu?

Maana kugonga gonga meza hovyo huku sheria za hovyo zikipitishwa ndiko kulikozusha kifo cha huyu kijana.
 
Kwenye ”mob justice” utamkamata nani utamwacha nani?nadhani Samia atakuwa anajua zaidi maana alisema duniani kote mambo haya yanatokea siyo kwenye serikali yake tu.

Apumzike kwa amani japo kwa damu yake atakuwa amefungua njia kwa mamlaka za kiserikali kufanya kazi kwa kufuata taratibu na weledi,uhuni wa watu kutekwa utapungua pia.
Samia ni chaguo na mpango wa Mungu, haters mtavukwa na shanga zenu Bure.
 
Kweli hawa ndiyo watakaoangushiwa jumba bovu lakini itakuwa ni kwa mkono wa dhulma maana hapo kila mtu alipiga na siyo wote walioinua mkono kumpiga!
Eeh hapo ili Polisi kujikosha wataenda kuwanyamata maafisa usafirishaji kadhaa ili waonekane hawajashindwa kazi😂 kwa wenye akili hiko kijiwe sio cha kukaa tena. Ni kuhamia location tofauti.
 
Hii ni kusudi tu

Watekaji wanajulikana ila wakija kila mtu anaufyata mfano yule Bonge alipiga kelele hakuna aliyejitokeza, kwa kibao hakuna aliejitokeza

Kwa Nondo tena kweupe kabisa hakuna aliethubutu hata kufungua mdomo

Leo hii mnajua kabisa hawa ni tra mnaamua kuwakomesha

Sasa rungu liwafikie wote waliohusika

Maana wanaokuja na bangili mkiwaona mnakaa kimya, hawa tofauti mnajifanya vifua mbele

Shenz type
Taratibu watu watajenga ujasiri. Bado ndio mwanzo tu. Ila yajayo yatawafurahisha
 
Hii ni kusudi tu

Watekaji wanajulikana ila wakija kila mtu anaufyata mfano yule Bonge alipiga kelele hakuna aliyejitokeza, kwa kibao hakuna aliejitokeza

Kwa Nondo tena kweupe kabisa hakuna aliethubutu hata kufungua mdomo

Leo hii mnajua kabisa hawa ni tra mnaamua kuwakomesha

Sasa rungu liwafikie wote waliohusika

Maana wanaokuja na bangili mkiwaona mnakaa kimya, hawa tofauti mnajifanya vifua mbele

Shenz type
Shenz type na mjinga ni wewe ambaye uneshindwa kuelewa kuwa TRA ilikosea sana ,kufanya ukamataji nyakati za usiku na kubwa zaidi kushindwa kusoma alama za nyakati.

Hili iwe alart kwa serikali!!
 
wao hawakupaswa kumvizia mt kwa stail ya watekaji, watz wangeamin vp kam n TRA? wakt mtaan kunamatukio ya kikatili yanaendlea? polen familia ila nadhan watz tmeanz kuamka sasa
Mbaya zaidi wamekula dress code za wasiojulikana. Maana kapero na tshirt ndio code hatari sana katika matukio ya ambush.
 
Back
Top Bottom