DOKEZO TRA, kodi za kuingiza Magari ni kichefuchefu kwa Wananchi

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Mmae!

Yani bei ya gari haizidi milioni 20 ila kodi ni milioni 65?

Hii nchi inatakiwa hiki kizazi chote kife kije kingine ndio labda kutakuwa na mabadiriko ya akili.
 
Bandari yetu imekuwa ya kuwafaidisha warundi, wanyarwanda, wazambia, wacongo na wamalawi sisi ni kutuumiza tu. Ukieleza kuwa kodi inatakiwa iwe chini kama majirani zetu, Mwigulu anajibu kikebehi kabisa, hamieni huko Burundi.
Ni lazima kupitishia bandari ya dar?
Gharama kubwa ni za ushuru (TRA) na sio za Bandari (TPA). Ushuru wa TRA ni lazima ulipwe bila kujali gari limeingia kwa njia gani (anga, maji, reli au barabara).
 
Unaongea upuuzi Tu


Shwain

Sent from my SM-A032F using JamiiForums mobile app
 
Kwani hapa kuna ligi ya wavijijini na wa mjini...? Here we are discussing kuhusu kodi za kuingiza gari nchini. Ili tupate unafuu. Na waliomo humu sio kwamba ni wa mjini tu boss
 
Suluhu mojawapo ni kuwa na bunge 50% hao wanaosema watatawala milele na 50% upinzani.

Ila sasa sisi wenyewe wananchi ndio shida namba moja. Wacha tuendelee kulialia tu.
 
Ndio maana hatuendeshi magari mazuri,tumekazana na vi IST tu, sababu ya mikodi mikubwa , huwa najiuliza je tusingekuwa na bandari kama Uganda, Rwanda, nk si ndio tungenyooka kabisa?
 
Inatokana na mentality kwamba magari ni anasa kama ilivyokuwa kununua radio cassette miaka ya 70 na 80 wanasahau kuwa dunia imebadilika sana sasa hivi magari ni sehemu ya hitaji muhimu sana katika familia
 
Hiyo gari ina uwezekano itakua Porsche.

Maana TRA wana allergy na Porsche kabisa.

Kodi mara 3 ya thamani ya gari.
 
Mbaya zaidi hata hili andiko hawatalisoma kwa sababu magari yao sisi walalahoi ndio huwanunulia kwa kodi zetu.
wanaona mkuu! mambo mengi tu yanaanziaga humu alafu wanajibu kwa sababu kila kinachosemwa ni ukweli! tusubiri tu majibu ..... tafuta fanta!
 
Kama thinking ya watawala na hao policy makers ni kuwakamua wananchi hata vijihela vyao vya vocha maskini ya Mungu unadhani kuna kutoboa hapo? wameshindwa kutafuta vyanzo mbadala, wamshindwa kutoza kodi rafiki ili watu wengi walipe, wameshindwa kubana matumizi ya serikali wanakamua walalahoi tu, ni shida sana hiyo nchi yetu , inafika mahala mwananchi unajiuliza ilikuaje ukazaliwa TZ, lakini ndio imeshatokea sasa, na watawala hawaoni kama kuna shida wanavaa visuti tu na kupaka pickle
 
Bidhaa nyingi kwenye nchi zisizo na bandari ziko chini kuliko sisi wenye bandari
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…