DOKEZO TRA, kodi za kuingiza Magari ni kichefuchefu kwa Wananchi

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Ukiongea sana utaambiwa kama hutaki kanunue baiskeli
 
Inasikitisha SANA. Watanzania tunaishi kama mashetani yani...Ukiwa Tunduma unashuhudia lundo la gari nzuri nzuri za aina tofauti tofauti na hizi yebo yebo zetu tulizozizoea kuziona hapa bongo zikivuka boda kwenda nchi jirani.
Hiv mkuu ukiwa nchi jirani ukanunua gari ukiwa huko hv kulileta hapa kwetu Kuna usumbufu tena ama huwa inakuwaje?
 
Ndo maana nchi yetu ina magari used na machakavu kila kona...na ajali haziishi...
Kwa sababu watu hawawezi kuingiza magari mapya
Harafu Polisi ikitokea ajali wao wanakimbilia kusema chanzo ilikua mwendo kasi kumbe magari ni chakavu tuu haya na hili hawawezi kulisema kwa kuwa wao ndio chanzo...na hawawezi kushauri kwa zile gari za nje hao trafiki watakagua nini kila saa si itakua salamu tu na wao wanapenda raia wakiendesha gari chakavu ili wapate utumbo..
 
Tushushe kodi halafu tupige ban kuagiza gari juu ya miaka 5. Ila tukishusha kodi halafu tukaacha kama jinsi ilivyo, miundombinu hautamudu kuhimili wingi wa magari.
Sasa miundo mbinu si ndo jukumu la serikali kujenga na kutengeneza sasa fikiria kama sasa hivi kodi za magari zipo juu na hio miundo mbinu ni mibovu yani huwezi hata kufurahia gari iliochini
 
Sasa miundo mbinu si ndo jukumu la serikali kujenga na kutengeneza sasa fikiria kama sasa hivi kodi za magari zipo juu na hio miundo mbinu ni mibovu yani huwezi hata kufurahia gari iliochini
Hili ni tatizo sugu boss.
 
Hili niliwahi lisema kupitia huu uzi:

 

Mkuu hongera sana sana kwa mada nzuri kabisa, umeona mbali sana.

Mkuu Maxence Melo, tafadhali hii mada msiiondoe, iwepo online muda wote, ikiwezekana na wewe mkuu Maxence utusaidie ujumbe huu uwafikie walengwa kwa namna yoyote, na sio kujali matumbo yao huku tusio na uwezo tunaumia.
 
Mfumo wa elimu umeleta aina ya viongozi waliokuwepo.

Akili ya kuwaza nje ya boksi hawana. Wanatafuta kitu ambacho ni obvious kwao then wanakirundika mikodi kibao.

Angalia petrol na diesel zinavyorundikwa makodi mara mbili ya thamani ya hayo mafuta.
 
Ubunifu katika kukusanya kodi hakuna ndio maana kunakua na mlundikano wa kodi kwenye kitu kimoja
Ndo akili zao zilipoishia ndio maana huwezi ona jipya lolote.

Telecom sector imepigwa kodi mpaka imeyumba, Petrol na Diesel zimesharundikwa mikodi kibao.

Uber na Bolt wameona wanapata faida sana, wamewapiga mikodi mpaka wameondoka.

Viongozi wanaowaza kijamaa ni nuksi sana kwa ustawi wa uchumi.
 
Yaani wanakamua kodi sawa na bei ya gari, aisee bongo bahati mbaya....

Ni hatari mno mkuu, kwanzia nyerere mpaka awamu ya 6 limekaliwa kimya suala la ushuru,sijui kwanini aise wanatufanyia hivyo!!

Ndugu zangu tupazeni sauti, tusikate tamaa na hilo, tunaumia tunaumia, magari dubai, Japan n.k bei ya kutupa, linunue sasa na ulilete huku aise kodi utakayolipizwa ni heri ukanunulia huku hata kama limechoka sawa tu.
 
Kodi inawekwa Kubwa Ili kupunguza idadi ya waagizaji magari. Kodi Ikiwa chini Kila mtu atanunua gar na itakuwa fujo. Mfano nchi ya Vietnam usafiri wao mkubwa ni pikipiki maana gar yoyote utakayonunua Kodi yake Kwa TSH n 80M.

Hivyo wanaotumia magari ni ni kama anasa tu.

Hata watumishi wengi wa serikali huko Vietnam wanaotumia pikipiki.

TRA Wako sahihi
 
Yaani wanakamua kodi sawa na bei ya gari, aisee bongo bahati mbaya....

Fikiria mzalishaji anakuuzia bei rahisi wao wanadandia kodi mara mbili hadi tatu ya bei ya manunuzi kesho wanaanza kulialia mapato hayatoshi wanashindwa kukumbuka mzunguko wa kiuchumi wameufunga wao wenyewe.
 

Gari chakavu lazima watu watakufa kila siku na wataleta visababu kibao kumbe kodi inachangia hadi basi la abiria mtu anabembeleza used za miaka kibao kumbe kodi himilivu watu wataleta vyuma vipya, magari imara huokoa pia uhai wa watu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…