TRA: Pikipiki (Bodaboda) kuanza kulipa Kodi ya Tsh. 65,000/- kwa mwaka

Unajua serikali inapo anzisha au kuongeza wigo wa Kodi,inamaana hapa Kuna watu watapata ajira waliosoma Mambo ya kodi, xo nijambo jema,sema daa! Nawaonea huruma boda Boda mtapata tabu Sana alafu wafanya biashara watapumzika kidogooo,maana nyie Boda Boda mtataka kusumbua kulipa xo Kuna ka nguvu katatumika 😄 poleni bhana
 
Tutarajie ile motor vehicle licence kurudi soon
 
Hiyo kodi ya 65000 Kwa mwaka ni sawa na shilingi 200 Kwa siku.

Ni kiwango kidogo mno lakini naamini wapotoshaji watakikuza sana na kuonesha uonevu.

Uzalendo ni kuhamasisha watu kulipa Kodi Kwa maendeleo yao.
Nitajie miradi mitano tu ya awamu hii ambayo imejengwa kwa kodi
 
 
Boda wawe na kadi maalum za kununulua mafuta ili hiyo Kodi ikatwe kwenye mafuta hivyo Liwe jukumu la Sheli kuhakikisha boda wote wamekatwa kwa siku
 
kipindi kile Lema alivyosema boda boda sio kazi rasmi walikuja juu na kudai wanaingiza pesa nyingi kupitia boda boda na wengine wamejenga. kuna mwingine alisema anaingiza hata milioni kadhaa kwa mwezi. Sasa leo 65,000 kwa mwaka ni kubwa? 🤣🤣 boda boda bhana
 
Mule mule!.
 

Hamna cha lema wala nani kikubwa ni kulipa kodi tena wamehurumiwa wanatakiwa kulipa zaidi ya 365000
Wengine ni hawa bajaji za abiria
Bajaji za mizigo wote hawa wanapata hela bila kukatwa kodi
Usipolipa kodi maendeleo yatatoka wapi ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…