proudcitizen
New Member
- May 24, 2025
- 3
- 13
Wadau, hebu tuzungumze kwa moyo mmoja…
TRA waliomba mamlaka ya kuajiri ihamie kutoka UTUMISHI kuja kwao, wakisema wataongeza ufanisi na uwazi kwenye mchakato wa ajira. Lakini tangu waanze kuendesha ajira wao wenyewe, hali imekuwa ya kutia shaka. Mwaka 2023 walifanya usaili lakini hatukuona transparency yoyote. Walifanya Written Interview, wakaendelea na Oral, lakini hakuna mahali walipochapisha list ya waliofaulu Oral Interview. Pia hakuna list ya PDF ya walioitwa kazini. Hii ni tofauti sana na utaratibu wa UTUMISHI ambao huweka wazi kila hatua.
Hii inatoa nafasi ya kujiuliza: Je, kuna figisu zinaendelea? Je, baadhi ya walioitwa kazini hawakupitia mchakato wa usaili kama wengine? Inawezekana vipi mtu aajiriwe bila jina lake kuonekana kwenye hatua zote za usaili? Au ni watoto wa wakubwa tu wanapewa ajira kimyakimya huku watoto wa masikini wakiachwa?
TRA, kama hamuwezi kuendesha ajira kwa uwazi na haki kama UTUMISHI, basi msiogope kurudisha mchakato huu mikononi mwao. Bora tufanye kwa mfumo unaoaminika na unaoweka kila kitu hadharani kuliko mfumo wenye mashaka na manung’uniko kila kona.
Transparency, transparency, na tena transparency!
Ajira za serikali ni haki ya kila Mtanzania, si zawadi kwa wachache walioko juu. UTUMISHI big up sana, TRA tafadhali – wekeni uwazi au rudisheni mfumo huu mikononi mwao.