TRA: Tunahitaji ajira zenye Uwazi kama Utumishi sio figisufigisu!

TRA: Tunahitaji ajira zenye Uwazi kama Utumishi sio figisufigisu!

Ni assumptions zangu lakini kuna anayejua kuhusu hili humu?
 
Sijakuelewa ulivosema hao 200 ni wengi sana. Yani ndo mchakato wa data base umeisha ama. Nachoka kuwaza
Nimeona ni wengi mno nashangaa nimekosekana itakua nlijibu utumbo mwingi au watu wengi walifaulu kwa alama za juu
 
Data base wako elf 4 kuwamaliza wote ni ngumu nadhani mwakani watatoa ajira mpya tu
Inawezekana,hiyo mwakani wakifanya tena interview wataacha tena watu elf tatu kwenye database?
 
Wadau, hebu tuzungumze kwa moyo mmoja…

TRA waliomba mamlaka ya kuajiri ihamie kutoka UTUMISHI kuja kwao, wakisema wataongeza ufanisi na uwazi kwenye mchakato wa ajira. Lakini tangu waanze kuendesha ajira wao wenyewe, hali imekuwa ya kutia shaka. Mwaka 2023 walifanya usaili lakini hatukuona transparency yoyote. Walifanya Written Interview, wakaendelea na Oral, lakini hakuna mahali walipochapisha list ya waliofaulu Oral Interview. Pia hakuna list ya PDF ya walioitwa kazini. Hii ni tofauti sana na utaratibu wa UTUMISHI ambao huweka wazi kila hatua.

Hii inatoa nafasi ya kujiuliza: Je, kuna figisu zinaendelea? Je, baadhi ya walioitwa kazini hawakupitia mchakato wa usaili kama wengine? Inawezekana vipi mtu aajiriwe bila jina lake kuonekana kwenye hatua zote za usaili? Au ni watoto wa wakubwa tu wanapewa ajira kimyakimya huku watoto wa masikini wakiachwa?

TRA, kama hamuwezi kuendesha ajira kwa uwazi na haki kama UTUMISHI, basi msiogope kurudisha mchakato huu mikononi mwao. Bora tufanye kwa mfumo unaoaminika na unaoweka kila kitu hadharani kuliko mfumo wenye mashaka na manung’uniko kila kona.

Transparency, transparency, na tena transparency!

Ajira za serikali ni haki ya kila Mtanzania, si zawadi kwa wachache walioko juu. UTUMISHI big up sana, TRA tafadhali – wekeni uwazi au rudisheni mfumo huu mikononi mwao.
Ile interview matokeo walikuwa nayo wachache, niliwahi kwenda mpaka nilifanya kuuliza kwa wengine ndiyo niikaoneshwa.

Ajabu sasa mtihani ule nilifanya pale Mbweni kama sikosei, ulikuwa rahisi na maswali ya kuchagua yote yanajibika. Kila wa kada yangu nilisoma naye alisema pale uhakika ni 90% na kuendelsa. Ila nilichokuja kukiona baada ya kuchunguza sana hayo martokeo, ambayo hata sikujulishwa, nilibaki mdomo wazi.

Kila ninayemjua tuliyoenda pale aliuliza ilikuwaje ana malksi ile
 
Kwa upande wa niseme ukweli sina ninayemjua wala sikuwa na mtihani ule wa written.Ila wakati natoka nilikuwa ninajua maswali niliyopata na niliyokosa na nilikuwa najua maksi zangu zitakuwa ngapi na kweli ziliangukia palepale kama nilivyocalculate
 
Ila database si huwa ni mwaka mmoja tu, kwa taratibu za ajira za utumishi wa umma au.
 
Alf pia kama taasisi inajua haina uhitaji na idadi hiyo ya watu sidhani kama ni jambo zuri uweke watu wengi database usiwachukue bora uweke wachache au usiweke kabisa
 
Alf pia kama taasisi inajua haina uhitaji na idadi hiyo ya watu sidhani kama ni jambo zuri uweke watu wengi database usiwachukue bora uweke wachache au usiweke kabisa
Dah yani TRa wanazingua. Na km nafasi ni chache basi wasingeweka hilo tangazo la database. Maana tulisha let go sasa wameamsha hopes zetu. Na ndio wanafanya vitu kimya kimya. Bora hata walitoe lile tangazo kwenye portal tujue mchakato umeisha.
 
Written eneo tulilofanyia hakukua na utaratibu mzuri watu walipoteza vyeti simu zilivunjika ilikua tafrani
 
Back
Top Bottom