TRA Wamepandisha kodi kwa magari yanayoingizwa nchini

Juxi kati, niliangalia V8 ya mwaka 2011 hivi ya bei nafuu, CIF ni kama 55m bali kodi na registration ni kama 88m 🙁 Custom value ni kubwa mno kulinganisha na CIF value.
Kaka usitumie Tena xxx huku jf hata Kama una hoja nzuri kiaje utapata ukozoaji mkubwa mno .epuka neno xx huku Ni jf siyo fb

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Aisee shukrani Sana mkuu, hapo nimekusoma.
 
Tuwekee hapa na CIF za hayo magari ya 2017,ndipo utajua hujui.
 
Hizo gari vijana dola zake imechangamka huko,ndiyo maana watu tunaaford gari nzee
 

Serikali yetu ina watu zero brain haya yote ulosema hata hawakufikiria hawaangalii mbele itakuaje wanachoangalia kodi tu.
 
Na ww ndipo ulipokosea. Hivyo unavosema sawasawa na mm nafahamu hivyo. Lakini kuna gari za mwaka 1999, 2000 , 2004 nazo zimepandishwa wakati hizi zilitakiwa bei zishuke
 
kwa ninavyoelewa hata mimi mwaka ukibadilika maana yake kama gari ilibakiza mwaka mmoja iwe kwenye kutozwa uchakavu ikifika januari itaanza tozwa sababu tayari mwaka utakuwa umebadilika.

Kupandisha kodi ni Bunge ndilo linalopitisha na hupandishwa au shusha kila Julai 1.

Sasa TRA kwanza hawana mamlaka ya kupandisha au shusha kodi.wao ni wasimamizi wa kodi.

Wanaweza samehe kpdi kama sheria itakavyoelekeza tu.

Viwango vya kodi vipo pale pale kisheria Afrika ya Mashariki yote ni viwango sawa isipokuwa wenzetu Kenya gari chakavu zaidi ya miaka 5 toka kutengenezwa kwake haliruhusiwi kabisa kuingia nchini sisi sharti hilo naona serikali imelegeza kwa kuweka uchakavu.

Yote ni kuepuka kuwa dumping place
 
Hapa ndo mnapokosea. Hawapandishi bei. Ila kila new year inapanda automatically kutokana na age kuongezeka kwenye excise duty due to age...
ni kweli Planet Subaru bei zinabadilika za uchakavu kwa kuwa mwaka unabadilika.

Wengi hatuelewi hili. January kweli utaona mabadiliko sababu ya miaka kubadilika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…