TRA waunde kitengo cha upangishaji wa nyumba, kila mwenye nyumba aripoti TRA anapotaka kupangisha na iwe kwa mujibu wa sheria

Udalali uko kila mahali
Udalali haukwepi

Ova
 
Ipo hivi Duniani kote kuna courses Mtu anaetaka kuwa Real Estate agent/broker anaenda Darasani anasoma 3-12 months baada ya hapo anakata Leseni ya kuwa Real Estate agent.Hapa pia atakata Leseni ya Biashara na TIN. wenye nyumba /vyumba vya kupangisha wanawa contact na kuwapa kazi ya kutangaza uwepo nyumba za kupanga na kiasi cha kodi kwa mwezi .Real estate agent yeye anatop up few %.mpangaji anapewa acc ya Bank analipia Bank-Mfano South Africa Real Estate Agents Account zao Mpngaji akilipa kuna settings bank wameweka zinaenda moja kwa moja kwa mwenye Nyumba na agent inabaki comission yake.So kama agent amepangisha wateja mia au zaidi anauwezo wa kupata mpaka 10M za kitanzania kwa mwezi. Hii ni nzuri kwani kila mwezi agent anapata hela kiasi na ni endelevu .Hapa Tz kodi ya mwezi ata kama dalali anafaidika lakini ni kidogo sana pia sustainability aipo na wengi wanaishi maisha ya kubahatisha bahatisha.
 
Udalali uko kila mahali
Udalali haukwepi

Ova
Mleta mada hajielewi huwezi kabidhi Mali yako ya Mamilioni kwa mtu usiyemjua mfano huwezi mkabidhi bodaboda ,au bajaji,au daladala au nyumba mtu usiyemjua Akiuza au kutoroka au afanye tukio baya utampata wapi?

Ndio maana wamiliki wengi material wa properties ikiwemo nyumba za kupanga hutaka mtu apitie kwa madalali

Dalali akisema ok owner anakubali deal
Fikiria unamiliki bodaboda , bajaji au daladala au nyumba mtu anakuja humjui ohhh nipe !!!! Una akili kumpa? Kunatakiwa third party refference ambaye Ni dalali
Wanaokataa dalali asiwepo Ni majambazi

Madalali sio majambazi wao ndio majambazi
 
Kwani mpangaji/anayetaka nyumba si anapatikana kwa juhudi za madalali
Sasa kuwa na nyumba yako alafu uipangishe
Bila kutegemea madalali
Uone

Ova
 
Udalali uko kila mahali
Udalali haukwepi

Ova
Wenzetu wanafanya kiprofesional sio kama huku kwetu Boss Mrangi.Na pia iwapo Serikali ikairasimisha hii professional itawasaidia ata hao madalali wenyewe.So wakati umefika hii sekta kuboreshwa na kuifanya iwe fani inayotambulika
 
Ndo maana Serikali inatakiwa kuja na mkakati wa kurasimisha hii kada iwe kama ya wanasheria,wahasibu etc .Ukikiuka miiko ya kazi unafungiwa
 

Kwangu binafsi kuwakutanisha wenye nyumba na TRA sijaona kama imekaa sawa.

Nadhani, hii ni fursa kwa watu waliosoma IT,

FURSA KIAJE?
Dalali ni nani: Ni mtu kati, anayekutanisha wajitaji pande mbili tofauti.

Patengenezwe app maalumu, au website ambapo itawakutanisha wenye nyumba na wapangaji. Ifanyike marketing ya kutosha kutangaza hiyo app/website ambapo kila anayejisahili kutaka kupanga/kupangisha anafanya malipo (say 5000) (hii ni registration fee anayopata mwenye hiyo platform). Hii app ina maana itaweza tumika Tanzania nzima, East Africa, Africa na dunia nzima huko mbeleni

Mwenye nyumba awe na acess ya kujaza information kama sehemu nyumba ilipo, size, vyumba vingapi, nk hadi picha aweke na bei

Mpangaji anayehitaji anaingia na kujichagulia nyumba sehemu anayohitaji, anakutana na mwenye nyumba moja kwa moja


Vivyo hivyo, kwenye transportation services..hasa kwenye magari ya mizigo, ifanyike hivi hivi kati ya transporters na wanaosafirisha vitu vyao

Mnishukuru kwa idea nzuri



HATA HAPA JAMIIFORUM, [mention]Maxence Melo [/mention] anaweza tumia hii fursa pia
 
Kama unamuweka dalali kulinda masilahi yako, kwaninii mizigo wa kumlipa huyo dalali abebe mpangaji? Akili ya wapi hii?!
 
Sawa mradi tu na wao walipe kodi.
 
Udadali dunia nzima upo, ila kinachotakiwa ni kuutambua kisheria ili hawa jamaa walipe kodi.

Udalali ni kazi ya information flow, anayetaka nyumba hamjui mwemye nyumba kwa sababu hatuna mfumo wa kuwakutanisha hawa wawili sasa hapa ndipo Dalali anapoingia.

Udalali si kwenye nyumba tu ni katika kila secta wapo.
 
Kama unamuweka dalali kulinda masilahi yako, kwaninii mizigo wa kumlipa huyo dalali abebe mpangaji? Akili ya wapi hii?!
Sio maslahi yangu nataka third party refference .Huwezi kuja to nyumbani kwangu sikujui wewe gaidi au jambazi ohh Mimi nataka kupanga kwako pesa hii hapa.

Refference wako Nani? Third party Mimi ambaye namjua? Anayeweza take risk Kama wewe gaidi au jambazi mnayejuana naye na Mimi namjua?

Hivi kwa akili yako unadhani mtu aweza kukupangisha nyumba ya apartment mfano Ina asset za ndani za milioni Mia kwa mtu ambaye hamjui na Hana refference reliable wa kumleta kwako? Sio unayemjua mwenye nyumba tu Bali na yeye dalali anamjua

Mimi nyumba zangu sikubali kumpangisha mtu nisiyemjua hata uje na midola sikupangishi dalali ninayemjua ndio akulete malipo ya udalali mtamalizana huko huko hainihusu
 
Kweli kabisa

Alafu hizi biashara zinaenda na connection

Chain

Ova
 
Hata kwenye madini kuna mabrokers

Kwenye hisa kuna brokers etc

Ova
 
Wenzetu wanafanya kiprofesional sio kama huku kwetu Boss Mrangi.Na pia iwapo Serikali ikairasimisha hii professional itawasaidia ata hao madalali wenyewe.So wakati umefika hii sekta kuboreshwa na kuifanya iwe fani inayotambulika
Hata dalali professional atataka hela ya mwezi mmoja mkuu
Si kampata mteja
Hapa issue ni upatikanaji wa mteja

Ova
 

Kwani kodi zenyewe siyo zinaishia kwenye madege na yale mapocho pocho ya kina Jobo?
 
Kwa hiyo unataka TRA ndiyo wawe madalali sasa?

Hapana aisee...
 
Sasa si ndio umlipe wewe mwenye nyumba?
 
Kustaafu isiwe sababu ya kutolipa kodi na kutafuta huruma ili hali unaingiza kipato tena sometimes kikubwa kuliko cha wale walioko makazini.

Kumbukeni misaada mnayopewa na wazungu ni kodi za watu wakiwemo wastaafu.
Gharama za umiliki wa jengo
°Lend rent
°mantain serv
°sewerage majitaka
°Ulinzi
°Korokoro nyingine nyingi mno.
 
Kabisa mkuu,
Na Ndo maana mwenye nyumba anaheshimika sana.

Ujenzi unaumiza.
Tena ukiona mtu kajenga na kumaliza ni wakuheshim saana. Kama kipindi hiki vifaaa vya ujenzi hasa usafi havikamatiki. Ujenzi wa sikuizi nimateso jamaaniii
 
Hata dalali professional atataka hela ya mwezi mmoja mkuu
Si kampata mteja
Hapa issue ni upatikanaji wa mteja

Ova
hapana -Duniani kote hata Kenya hakuna kodi ya mwezi ! why kuna commission agents?? madalali wa magari wanaishije??? wanapata nn?? wakiuza gari??- ukweli tumekosea sana kwenye hili kama taifa na kweli kuna haja ya kubadilika
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…