TRA yadaiwa kuvamia Waturuki na kufunga Ofisi jioni ya Leo (Desemba 14, 2020)

TRA wa sasa wapo tayari hata kufunga A/C bank mfanyabiashara ashindwe kuzungusha pesa ashindwe hata kurejesha mkopo kwa visingizio vya kishamba haramu na vya kishetani
 
Jua matumizi ya lugha. Unajua maana ya neno "vamia?" Lini mamlaka halali kisheria ikiwa inatekeleza majukumu yake kisheria useme imevami?
 
Kweli hujui unachoandika kwa sababu unakula bure! Hawa waturuki wameleta Equipment, zenye gharama ambayo inaweza kuwa collateral kwenye mkopo, wanaruhusiwa kuomba mkopo. Nenda kaona pale TIC, siyo kukaaa na kwa shemeji na kula bure tu. Na nchi nyingi zinafanya aina ya uwezeshaji huo.
 
Jua matumizi ya lugha. Unajua maana ya neno "vamia?" Lini mamlaka halali kisheria ikiwa inatekeleza majukumu yake kisheria useme imevami?
Acha kutetea uonevu kwa kisingizio cha mamlaka halali wakati hizo hizo mamlaka baadhi huwabambikia wafanyabiashara kodi bandia na hata kuwabambikia kesi na uonevu mwingineo kibao
 
Mkopo hauna Uraia yeyote anakopa tu na TRA wanapaswa kutumia njia za kistarabu kudai kodi siyo ubabe wa kishamba kwa njia haramu za kishetani kutengeneza mazingira ya Rushwa
 
TRA sasa wamewafanya hata Bank kukosa pesa nyingi tokea kwa wafanyabiashara baada ya kuanza kukosa imani na mabenk kwa kuwa TRA huenda kufunga A/C za wafanyabiashara kihuni huni tu kuwapora pesa zao kwa visingizio vya VAT na mengineyo ambayo hayaeleweki,huwa wakiwa wamedhamilia Rushwa hujitoa fahamu na kuwabambikia kodi bila kujali takwimu za wakaguzi wenzao waliopita awali kwa wafanyabiashara.
 
TRA ifumuliwe isukwe upya na wale maofisa vinara wa kufunga kampuni, kufunga account za wafanyabiashara wote watajwe majina yao wapate kuchunguzwa na Takukuru juu ya mali zao
 

Mkichekewa hamuwezi kulipa kodi. Hakuna binadamu anayependa kodi siku zote. Halafu nashangaa kwa nini wanaokwepa kodi hawabanwi? Kampuni ya mzee wangu hatulipi kodi lakini sijawahi kuona wamekuja [emoji23][emoji23]..
 
Kabla hujafanya biashara ya halali, ufanye utafiti kwanza! Usishindwe wewe, ukaanza kulaumu TRA. Umesema biashara haikufanya vizuri kwa sababu ya eneo! Je! Na hilo ni kosa la TRA?
TRA wakidhamilia Rushwa hata uwe malaika tokea kwa mungu hawakosi kisingizio lazima watakubambikia chochote ili kutimiza lengo lao, wewe usikute ni mnufaika wa uonevu wa TRA ndiyo maana unatetea uovu wao.
 
Jua matumizi ya lugha. Unajua maana ya neno "vamia?" Lini mamlaka halali kisheria ikiwa inatekeleza majukumu yake kisheria useme imevami?
Umejua maana ya neno ila ume fail kuitafsiri....wote tunajua wafanyabishara ndiyo wanailisha hii nchi unaanzaje kuanza kumfungia virago instead ya kumuita offisini na kufanya mazungumzo na kufikia muafaka, wafanyabisahara sio wahalifu wanatakiwa wachukuliwe serious na sio mzaha mzaha, kuwa nao karibu wengi wanapitia magumu unakuta mtu amechukua mkopo faida haioni bado uje umfungie ofisi huo mkopo ataulipaje na kodi atalipaje?
 
Kiongozi ukifungua biashara alafu ikafa unaandika barua kuwajulisha kuwa biashara yako umeifunga hivyo wasiendelee kukudai tena kodi, lakini biashara ikifa alafu ukakaa kimya wao wanaendela kuhesabu tu kodi yao.
TRA walianzisha utaratibu wa kudai kodi ya magari yote bila kujali kama liko barabarani au la. Kama gari lako lilipata ajali au liliharibika miaka 20 iliyopita ukaliweka juu ya mawe lakini hukuwaambia, jamaa walikuletea invoice. Mheshimiwa Rais akazuia upuuzi huo. Bahati mbaya watu huwa tunalisahau jambo hili jema alilofanya na hatumpi sifa anazostahili kwa kuchukua uamuzi ule.

Amandla...
 
Unalipaje kodi haujaanza biashara? Hua nasema TRA watakuja kutuua na kiharusi kodi idaiwe kwenye faida hapo sawa unadai vipi kodi kwenye mtaji?
Hujawahi kadiriwa kodi na huku hujaanza biashara?.Tatizo linaanzia hapo mifumo yetu inawafanya TRA kutazama kodi kwanza kabla ya kuijali na kuikuza biashara yeneyewe ili iweze kutoa kodi.

Kwetu mtu kuwa na TIN number tu ya baishara tayari unatazamwa kama mdaiwa wa kodi kumbe kuna nchi mtoto akishazaliwa anapewa TIN akifikisha 18 ndipo wanaanza kuangilia kama ana kipato.

Mazingira ya kuanza biashara bado hayako favaourable sana hasa kwa weneye mitaji midogo inayowafanya kuchukua muda mrefu kuanza uzalishaji au kupata return ya uwekezaji
 

Ni sawa kabisa, Yani uje huku uchukue mkopo humu? Fungeni tu!
 
Wewe wa wapi hakuna mwekezaj anakuja na mtaji, wanakuja na kuchukua mikopo kwenye bank ndo biashara zinazofanywa, tofauti na hapo utaambiwa unatakatisha fedha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…