Jioni ya leo, TRA imevamia na kufunga ofisi moja ambayo ilikuwa bado haijaanza kufanya kazi wakidai kodi. Hii ni kampuni ya Waturuki inayohusika na kutengeneza tiles za majengo. Mashine zililetwa lakini kwa bahati mbaya jamaa walishindwa kuanza kufanya kazi kutokana na mtaji kutokutosha.
Waturuki walitegemea kupata mkopo kwenye moja ya mabenki ya ndani, kitu ambacho kimechelewa. Mategemeo yao ilikuwa ni kupata mkopo mwezi wa 4 lakini hadi Desemba mkopo ulikuwa bado haujapitishwa. Kwa maana hiyo hawakuwa na jinsi ya kuanza operations zao.
Hii kampuni hipo maeneo ya Mbezi Afrikana, na kwa bahati mbaya, magari ya TRA wamevamia jioni hii na kufunga ile ofisi na kumchukua mtu anayesimamia ile mali maana wengine inaonekana wako nje ya nchi. Na kwa sababu hakuna kazi, ni mmoja wao amebakia pale kulinda mali.