TRA yadaiwa kuvamia Waturuki na kufunga Ofisi jioni ya Leo (Desemba 14, 2020)

TRA yadaiwa kuvamia Waturuki na kufunga Ofisi jioni ya Leo (Desemba 14, 2020)

MUONGO MKUBWA!

You have corn flakes for brains.

TIC na Serikali hawawezi kuahidi incentive ya kukopesha mjuba yeyote duniani kwa sababu Tanzania Investment Center SIO BENKI

TIC haiwezi kuiambia benki ya Exim, wee benki mkopeshe huyo Mchina!

Eti hawakujua kama watanyimwa mkopo. Wangetuma maombi ya mkopo kabla hawajaja.

Unatokaje Ulaya kuja kuomba mkopo Benki ya Maendeleo Vijijini, Madale kwa Mfuga Mbwa?

Revoke their Visas, ship them back. Instabul must refund us for the deportation tickets.

Hatuhitaji akili ya Mturuki kuendesha biashara ya vigae.
Huhitaji akili za mturuki kuendesha biashara pia na yeye hahitaji wizi wako wa kwenda kumsingizia kodi hewa
 
Jioni ya leo, TRA imevamia na kufunga ofisi moja ambayo ilikuwa bado haijaanza kufanya kazi wakidai kodi. Hii ni kampuni ya Waturuki inayohusika na kutengeneza tiles za majengo. Mashine zililetwa lakini kwa bahati mbaya jamaa walishindwa kuanza kufanya kazi kutokana na mtaji kutokutosha.

Waturuki walitegemea kupata mkopo kwenye moja ya mabenki ya ndani, kitu ambacho kimechelewa. Mategemeo yao ilikuwa ni kupata mkopo mwezi wa 4 lakini hadi Desemba mkopo ulikuwa bado haujapitishwa. Kwa maana hiyo hawakuwa na jinsi ya kuanza operations zao.

Hii kampuni ipo maeneo ya Mbezi Afrikana, na kwa bahati mbaya, magari ya TRA wamevamia jioni hii na kufunga ile ofisi na kumchukua mtu anayesimamia ile mali maana wengine inaonekana wako nje ya nchi. Na kwa sababu hakuna kazi, ni mmoja wao amebakia pale kulinda mali.
Halaf utasikia lafa jamo anakenyua meno eti "nataka netengeneze mabiorenea"
 
Huelewi chochote wewe. Tumewekeza nchi nyingine, tunajua. Kwanza nchi nyingine wanahamasisha ukope kwenye mabank yao kwa sababu unawaongezea biashara.

Unawekeza mpaka kiasi fulani cha kutosheleza kutoa dhamana kwa bank, kisha unachukua mkopo.

TRA ni genge la wahuni. Na wengi wao ni low IQ. Fuatilia hata vyuo walivyosoma.

Sent using Jamii Forums mobile app
Tatizo lao ni rushwa siyo low IQ.
Wengo wao wanajenga mazingira ya kupewa ongo.
 
Tatizo la jf wachangiaji wengi nawanaopewa kipaumbele ni wachadema.

Hawawezi kuchangia bila kuinguza siasa zao za kisariti.

Hawa waturuki kama hujui walipoanzisha kile kiwanda walienda moja ya bank (sitaitaja) wakakopeshana kwa njia isiyo halali, kwa maana ya viongozi wa bank hyo nao walikula kupitia mgongo huo.

Nadhamana kubwa ilikuwa ni aridhi kwa maana ya kiwanja na mitambo, lakini mitambo wakathaminisha zaidi ya thamani husika.
Wakapiga pesa, bank nayo ikajifia, ndo moja ya bank zilizofutwa.
Kumbuka pesa niza wanahisa naniza seeikali, waturuki wakasepa, ndo serikali inaendelea kung'ata mmoja mmoja.

TRA wako nao wanadai kodi zao. Kosa liko wapi???
 
Pamoja na mapungufu ya TRA Ila wachangiaji wengi hapa wanakimbilia kuleta Siasa. Wewe kama mtanzania unaweza kwenda uturuki au nchi yoyote hata Kenya bila mtaji wa kutosha ukitegemea benki zao zikukopeshe na ukaachwa tu!?
Kwa enzi hizi bado unauliza swali hili?

Jibu ni ndio. Mtaji siyo pesa pekee. Mwekezaji anaweza akawa na mtaji ambao sio pesa (hard currency), bali akawa anaomtaji wa ubunifu kichwani ambao akienda nao benki (local) hakosi kupewa huo mkopo.

Lakini pia najiuliza, kwa nini hao waturuki wasingeshirikiana na mwekezaji wa hapa nyumbani ili wapate mkopo haraka; kwani hiyo nayo ni option.
 
Nilikuwa na kabar kangu Kila cku hawa kwa hasira nikaita jamaa zangu tukanywa bia zote na K vant na kufunga.nasikia siku 3 walienda na kukuta hola nimesepa.
 
Tatizo la jf wachangiaji wengi nawanaopewa kipaumbele ni wachadema.

Hawawezi kuchangia bila kuinguza siasa zao za kisariti.

Hawa waturuki kama hujui walipoanzisha kile kiwanda walienda moja ya bank (sitaitaja) wakakopeshana kwa njia isiyo halali, kwa maana ya viongozi wa bank hyo nao walikula kupitia mgongo huo.

Nadhamana kubwa ilikuwa ni aridhi kwa maana ya kiwanja na mitambo, lakini mitambo wakathaminisha zaidi ya thamani husika.
Wakapiga pesa, bank nayo ikajifia, ndo moja ya bank zilizofutwa.
Kumbuka pesa niza wanahisa naniza seeikali, waturuki wakasepa, ndo serikali inaendelea kung'ata mmoja mmoja.

TRA wako nao wanadai kodi zao. Kosa liko wapi???
Wewe umefunua ukurasa mpya, pamoja na kwamba hukueleza kinagaubaga hali halisi ilikuwaje.

Naona kuna zaidi ya yale aliyoyaeleza mleta mada hapo mwanzo.
 
Kiongozi ukifungua biashara alafu ikafa unaandika barua kuwajulisha kuwa biashara yako umeifunga hivyo wasiendelee kukudai tena kodi, lakini biashara ikifa alafu ukakaa kimya wao wanaendela kuhesabu tu kodi yao.
Hata ukiwaandikia barua, wataendelea kukutumia msg tu ya kukumbusha ukalipe kodi.
 
Kiongozi ukifungua biashara alafu ikafa unaandika barua kuwajulisha kuwa biashara yako umeifunga hivyo wasiendelee kukudai tena kodi, lakini biashara ikifa alafu ukakaa kimya wao wanaendela kuhesabu tu kodi yao.
Ndo ujinga wenyewe... EFD za nini sasa? Kuna vitu vipo AUTOMATIC... if you dont see transactions then, mtu hauzi...!! Kwa nini benki wao wakiona hujagusa account kwa miezi kadhaa, inakuwa DOMANT..!!???
 
Hiki kitu nakifahamu lakini ni unyanyasaji tunafanyiwa wewe haujaanza biashara ukajua faida yake halafu ukadiriwe kodi means wanakadiria kodi kwenye mtaji wakati uhalisia wanatakiwa kukadiria kodi kwenye Faida, unapokadiria kodi kwenye mtaji unaandaa mazingira ya kuua mtaji.
Mkuu, nadhani pasiwepo ubishi kwa sababu ya kutaka pawepo ubishi tu.

Sina hakika kama makadirio ya kodi yanafanyika kwenye mtaji. Mimi nilidhani kwamba uliyemjibu alikuwa na maana kuwa wewe katika kuanzisha biashara yako utakuwa umechambua na kunyambua faida itakuwa ni kiasi gani. Ni haya makadirio ndiyo yatatazamwa mwisho wa mchezo. Kama ulikadiria faida kiduchu na huku kiuhalisia faida yake umepata kubwa hapo itakubidi ulipe kodi zaidi. Lakini kama mategemeo yako hayakutimia na ukapata faida kidogo kuliko makadirio uliyoweka mwanzo, hapo TRA wana wajibu wa kukufidia.

Au wewe umeelewa vipi mkuu wangu 'Arovera'?

Nitumie pia nafasi hii kuandika kwamba ni wafanya biashara wachache sana wanaoridhika na kulipa kodi inayopunguza faida yao. Malalamiko mengi haya yanayosikika sasa hivi inawezekana kabisa ikawa ni kwa sababu TRA nao wamebania kila sehemu kwa haki na sio lazima iwe ni kudhurumu.

Inashangaza kidogo, hata leo hii mtu unaweza kwenda dukani na usipodai risiti, jamaa wafanyabiasahara hilo haliwapi taabu yoyote.

Huko nchi za wenzetu, kutoa receipt ni kama kuvuta hewa, ni jambo lisilohangaisha watu tena. Na sasa hizi scanning za bar codes zinazidi kurahisisha ukusanyaji wa kodi. Hata kama risiti haitolewi, lakini Kaisari anajua haki yake tayari imeingia kibindoni.

TRA bado wanayo kazi kubwa sana, na lawama nyingi sana zitaendelea kuwazonga, kwa maana kadri wanavyobana mianya, ndivyo vilio vingi sana vinazidi kujitokeza.
 
Back
Top Bottom