TRA yaendelea kumkaba koo Toufiq Salum Turky kodi ya gari milioni 308.5

Sina akili mimi, au wewe na wapuuzi wenzako baadhi wa ccm ndiyo hamna akili! Mnashindwa kutoza kodi stahiki kwenye raslimali kama madini na gesi, mnakimbilia kuwaumiza watu wanaonunua magari! Unaona ni ujanja kwa hao TRA kutoza kodi ya milioni 6 kwa gari iliyo agizwa kwa gharama hiyo hiyo ya milioni 6!

Mbona magari yenu ya kifahari mnayaingiza nchini bila ya kulipa hizo kodi? Hopeless kabisa wewe. Au mnajiona nyinyi pekee ndiyo mna haki ya kutembelea magari ya kifahari!
 
Yaleyale ya kulazimisha kufanya Dodoma kuwa Makao Makuu ya nchi wakati SABABU zilizofanya maamuzi hayo yakatolewa mwaka 1973 HAZIKUWEPO tena 2017.
 
Kwani kununua gari ni utajiri? Tuondokane na mawazo haya jamani!!! Gari ni kitendea kazi tu kama vifaa vingine. Halafu formula ya kodi ni moja hakuna hili gari kaagiza tajiri au mlalahoi
 
Mawazo ya kimaskini hayo
 
Naomba niulize, kwani kodi ina formula moja au inaangalia aliyeagiza ni tajiri au mtu wa kawaida?
 
Naomba niulize, kwani kodi ina formula moja au inaangalia aliyeagiza ni tajiri au mtu wa kawaida?
Kodi HAINA formula moja. Kodi HAIANGALII sura. Kodi inaangalia BIDHAA. Kwa mfano maskini wa kutupwa akiokota sh bilioni moja akaamua kuagiza gari la kifahari aina ya Rolls Royce, atachajiwa kodi ile ile atakayochajiwa tajiri. Kwa hiyo basi sisemi huyu achajiwe kodi kubwa kwa sababu ni tajiri. Nasema achajiwe kodi kwa sababu ya aina ya gari alilonunua. Siku zote na popote duniani kodi inatoa unafuu kwa bidhaa muhimu na kutoza zaidi kwenye bidhaa za anaza. Tupo pamoja?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…