TRA yafungulia akaunti zote za Wafanyabiashara zilizokuwa zimefungwa kutokana na madeni ya kodi

Wewe ni mtu deluded mwenye cognitive bias ya hali ya juu.
Hilo wala halina ubushi, hila sio muda mrefu utaelewa kukopesheka bila idhini ya IMF na WD sio jambo rahisi.

Wakopaji walikuwa wanamuamini Magufuli anauwezo wa kulipa, tuombe na mama apewe imani ile ile waliyokuwa nayo kwa hayati.
 
Ni vizuri maana wengine mkishika hapo ina maana kila kitu kinasimama ajira za watu hata kile kidogo cha kodi nacho kinapotea kabisa maana kama umefreeze acc...biashara itaendeleaje kwa kulipa kidogo kidogo wanaepusha mengi....hongera
Yule Bwana alituharibia Sana nchi.check mfano ishu ya mishahara ya watumishi sio rahisi kuibalance ije ikae sawa.
 

TRA walikuwa wanafunga account za wafanya biashara kisha dhalimu anazunguka na fedha za kupora kugawa huko mitaani, wakati yeye alikuwa halipi kodi. Eti sheria inawaruhusu TRA kushikilia account za watu baada ya njia zote kushindikana, je sasa hivi baada ya dhalimu kuelekea kuzimu hizo njia ndio zimerejea?
 
Wewe hukuwa mfanyakazi wa Serikali. Hakuna mfanyakazi wa Serikali alikuwa anapata mshahara tarehe 5/ mwezi unaofuata
 
OK nimekupata; tatizo bado unachanganya utaratibu wa jinsi ivyo vitu vinavyodaiwa.

Sijachanganya, nisamehe nitakupa maelezo marefu kwann TRA walionekana wanyang'anyi 2015-2020.

Ukishajikadiria una namna tatu za kulipa. Ulipe yote, ulipe mara mbili au ulipe mara nne. Baada ya hapo utapeleka hesabu zilizokaguliwa na CPA(T) PP kuonyesha kuwa ulichojikadiria kilikuwa sahihi hujaiibia serikali na ww hujaibiwa. TRA watafanya kitu kinaitwa examination of books of accounts. Kama kuna kodi hukuilipa watakuambia ilipe.

Tatizo limekuja TRA wanajisahau wanakaa muda mrefu hawafanyi examination, halafu wakifanya wanakucharge penalty na interest ya muda mpaka kufikia wakati wa ukaguzi ulipofanyika. Hapo sasa ndio dhana ya unyang'Anyi inapokuja.

Mfano, assume umepeleka hesabu za 2014 june 2015. TRA wakakaa nazo mpaka april 2021, wakagundua ulilipa kodi pungufu kwa 30m.
Kutegemeana na aina ya kodi utachajiwa adhabu ya miezi approx 60 na interest. Kama adhabu ni 225,000 then itakuwa:
30m+ (225,0000 ×60) plus interest kila mwezi. Hapo ni mwaka 2014, watafanya hivyo hivyo 2015, 2016, 2017,2018,2019. Kila mwaka na adhabu zake na penalt zake. Ndo unasikia mtu anadaiwa M800 na TRA.

Sasa unajiuliza kwann ukae na hesabu miaka mingi uzilimbikize na hesabu nyingine ili umwadhibu mtu na kumcharge interest? Halafu kwann kama examination yako imeonyesha nimelipa pungufu kwann hukunieleza mwaka husika ili kama umefanya makosa ya examination nyaraka ziletwe, kwann unasubiri pale ambapo kuna uwezekano sitakuwa na nyaraka kukuprove wrong?

Ukumbuke mwaka wa biashara ukimpa mfanyabiashara tax clearence certificate ni wafanyabiashara wachache sana ni watunzaji wa nyaraka kama marisiti, bank slips n.k.

Baada ya yote hayo Wanafunga acc, wanachukua hela bila kujali hiyo hela ni mkopo au ya mauzo ya manunuzi ya mteja. Hapo ndo neno unyang'anyi linapokuja.
 
Pia kuna fedha na vifaa vilivyoporwa kwenye bureau de change virudishwe kwa wenyewe. Mwendazake alikuwa mtu mwovu sana. Kinachonishangaza kuna watu watu walikuwa wanampenda! Mungu mwema sana!
Ukiwa na mawazo ya chapchap huwezi kuelewa kwanini mwendazake alipendwa kwa ubaya na uzuri.Utamaduni wa Mtanzania ni kukwepa deni ndiyo anajiona mjanja.
 
Acha upumbavu wewe unaongea usichokijua. Yaani JK aliyekua anakusanya bil.750 kwa mwezi ndiye bora kulikonhuyu aliekua anakusanya karibu tril. 2 kwa mwezi. Hebu tukumbushe ni mradi gani wa maana wa kimkakati uliofanywa na JK.
Wewe ndiye mpumbavu kwa kukurupuka kwa kudhani kuwa Mwendazake alikuwa anakusanya sana kuliko JK, nitakupa sababu ;
1. Takwimu za Mwendazake zilikuwa za kuchakachua. Alikuwa mwongo kwa kila kitu. Anasema tunajenga kwa hela zetu za ndani halafu kesho unakuta KM Fedha na Waziri wa Fedha wanakopa AfDB au Stan chart

2. Kama alikuwa anakusanya sana kwa nini alishindwa kuongea mishahara ya wafanya kazi kwa miaka 5

3. Wakati wa JK Halmashauri zilikuwa zinakusanya mapato zenyewe hivyo basi zikikuwa hazihesabiwi kwenye kapu kubwa la Hazina. Wakati wa Mwendazake fedha zinazotangazwa na Hazina zinahusisha na za Halmashauri

4. Population wakati wa JK mpaka 2015 ilikuwa 55 Million, wakati wa Mwendazake ilipanda hadi 60 Milion mwaka 2020
 
Mama anifumua vizuri sana legacy.
Samia futa na masheria ya hovyo aliojitungia yule Muovu.
 
 
Mke wangu acha kupaniki,hujawahi kufanya biashara ndio maana huwezi kuelewa TRA ilichokua inakifanya.

We tulia hapo nyumbani wanaume tutakuletea mahitaji ya nyumbani upike,ila haya mambo ya Tra achana nayo maana huyajui.
 
Yafaa TRA iachwe kufanya kazi kwa mujibu wa sheria sio shinikizo hata kutoka kwa rais ambaye anawayumbisha kwenye kutekeleza wajibu wao. Malalamiko ya wafanyabiashara yasiwe ndio hoja ya kutiliwa manani bila kuangaliwa sababu ya kuwepo sheria na taratibu za ukusanyaji kodi zilizowekwa.
 
Data za uchumi huwezi kuzipika. Zinakusanywa na IMF na ndiyo waliotuingiza kwenye nchi za uchumi wa kati. Muda utaongea kama tutaendelea kuwemo kwenye hizo nchi za uchumi wa kati au tutarudishwa tulikotoka. Kuwa na subira. Ninawajua sana watanzania aka wabongo; hawawezi kupata maendeleo bila kuwarusharusha kichura. Ukiwachekea chekea tu utavuna mabuwa.
 
Swali zuri sana nimeandika kitabu mama vingine vitafuata nimeangalia pia soko la nchi zinazoendelea siyo kwa Tanzania peke yake Tanzania being a source of local knowledge
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…