TRA yampiga faini ya 3,500,000 dereva kisa kapakia tenga 27 za nyanya

Mashine ni ya ofisi, sio ya dereva, na dereva kajiongeza, na huku kujiongeza ndio hufanya vyakula viwe bei nafuu hata wanyonge wanaweza kumudu kula, sasa tukikaza kila kona hadi kwenye vyakula tutaumiza wanyonge, busara iwe inatumika
Enzi hizo, watu walikuwa huru sana kujiongeza. Hazina ikaishiwa hela kabisa. Nakumbuka Walimu wetu walipata shida sana kwenye mishahara. Kunusuru ikabidi "Sur tax" ianzishwe kwenye magari.
 
Rais alisema kama mzigo wako haijavuka tani moja usilipe kodi.
Na karudia rudia mara kibao.

Kwa hio sijaelewa.
Au yale yalikuwa maneno ya majukwaani???
Mkuu utofautishe kati ya kodi ya mazao inayomhusu mkulima na kodi ya biashara ya usafirishaji (transportation) kitu chochote bila kujali aina ya kitu inayo mhusu mmiliki wa gari au kampuni ya usafirishaji.
 
Chief nini huangaliwa mpaka mzigo wa thamani hiyo ukapigwa faini kama hiyo?
 
Wakulima nao Wana EFD?.
Mzigo unatoka shamba efd inatoka wapi?
Mkuu naongea hivi vitu kwa uzoefu hapa.
Ni hivi watendaji wote kule vijijini wana mashine za EFD na ni Lazima ukatiwe risiti yenye jina lako sambamba na leseni ya biashara. Mkuu ukikosa hiyo risiti au kwa Bahati mbaya ukapoteza. Trust me kama unatoka Singida Basi hata pale Kateshi hufiki maana kutoka Singida Mpaka Babati kuna geti kama nane hivi na zote zinakagua risiti.
 
Inakuwa risiti ya bei gani?
 
Chief nini huangaliwa mpaka mzigo wa thamani hiyo ukapigwa faini kama hiyo?
Kwenye suala la faini chief kweli sina ushahidi nalo ni kiwango gani unatakiwa ulipe.
Ila ukitokea huna hivyo vitu basi mnaweza kukaa mkaongea mkamalizana kisela.
Lakini kwa hiyo faini hapo SINA UHAKIKA KAMA NI SAHIHI, labda jamaa atuoneshe risiti ya hiyo faini
 
Tunakoelekea, bei ya mazao yanayoharibika kwa haraka itapanda sana, kula vitu kama nyanya na vitunguu itakuja kuwa ni anasa, serikali ichukue hatua sasa juu ya hili, ikiwezekana pawe na exemption kwa mazao ya chakula yanayoharibika kwa haraka na yasiyozidi kiwango flani kudaiwa risiti za usafirishaji, lazima tutumie akili, tutaua wakulima na wananchi njaa bila sababu za msingi, ahsante kwa mchango wako mzuri sana, tutaufanyia kazi. Ngoja nijadiliane na mbunge hapa.
 
inakuwa risiti ya Bei gani?
Kwa mfano ukiwa na tenga mia za nyanya Basi kila tenga ni shilingi 1000 tu kwa hiyo kwa tenga 100 ni shilingi laki moja.

NARUDIA TENA KAMA UNAFANYA BIASHARA ZA MIKOANI KUBEBA MAZAO BASI HAKIKISHA UNA RISITI NA PIA IPIGE PICHA.
WAKUU WALE JAMAA WA TRA WANA NYODO KISEN*E KAMA UKIKOSA HIVYO VITU
 
Kwa hiyo tenga 27 ni elfu 27.
Sasa mbona faini ni milioni 3
 
Kuna kipindi papo kwa papo kila Jumamosi saa 3 usiku mh. Polepole anatatua kero za watu pale pale
 
Angalia post iliyofuata baada ya hii post yangu uliyoi quote.
Jamaa katuma video kabisa
Dah! Alikua kiserikali kabisa, maana akivaaga mashati ya kijani anaakuaga haaminiki ila hapo kila kitu alichoongea ni amri huyu dereva apaze sauti yake mpaka imfikie au kama wana umoja wasaidiane kupiga kelele maana kazi ya udereva wa maroli bila kucheza ndondo hamnaga kitu pale
 
Kwa hyo tenga 27 Ni elfu 27.
Sasa mbona faini Ni milioni 3
Ndio maana kuna sehemu nimesema sina uhakika na hiyo faini labda jamaa atuletee ushahidi.
Mara nyingi unaweza kupigwa faini ya laki tatu mpaka tano ila inategemea na mzigo.
Mimi bado kwenye hiyo faini niko kama TOMASO. Mpaka niione ndio ntaamini
 
Faini hiyo ni kwa wale wenye maduka.
Na hiyo risiti sio risiti ya mzigo ni risiti za viongozi wa vijiji.
Ila risiti yenyewe ya mzigo Ni ngumu kuipata maana mzigo unatoka shamba hautoki sokoni.
Ndo mana kuna sehem nimesema sina uhakika na hiyo faini labda jamaa atuletee ushahidi.
Mara nyingi unaweza kupigwa faini ya laki tatu Mpaka tano ila inategemea na mzigo.
Mimi bado kwenye hiyo faini Niko kama TOMASO. Mpaka niione ndo ntaamin
 
Faini hyo NI kwa wale wenye maduka.
Na hyo risiti sio risiti ya mzigo Ni risiti za viongozi wa vijiji.
Ila risiti yenyewe ya mzigo Ni ngumu kuipata maana mzigo unatoka shamba hautoki sokoni.
Risiti ni rahisi sana kuipata, kama nilivyokuambia wanakatisha risiti ni hao watendaji wa vijiji. Maana watendaji wana EFD MACHINE na pia huwa kuna mawakala wa vipimo wanazungukaga
 
Kwa hyo tenga 27 Ni elfu 27.
Sasa mbona faini Ni milioni 3
Kosa linakuwa ni kutotumia mashine ya Efd, swala la ni nini na cha thamani gani ulibeba haliwahusu Tra, faini ya kutotumia Efd ni kuanzia mil 3 Hadi 4.5
Ni moja ya sheria kandamizi sana ambayo chimbuko lake ni bungeni, nakumbuka miswada iliyoleta sheria ya adhabu hii ilijadiliwa kishabiki sana bungeni na wabunge wa chama pendwa.
Unyama unaofanywa na TRA una baraka zote za bunge japo maafisa wao kadhaa nao wamejiongeza .
 
Rais alisema kama mzigo wako haijavuka tani moja usilipe kodi.
Na karudia rudia mara kibao.

Kwa hio sijaelewa.
Au yale yalikuwa maneno ya majukwaani???
Unachanganya mada, unachoeleza hakihusiani na nilichoandika, tafadhali soma tena vizuri.
 
Kwani sheria ya kutumia EFD inataka mwenye mauzo kuanzia shilingi ngapi hadi ngapi kwa Mwaka awe na mashine ya EFD?

Iwapo huyo dereva amenunua kwa wakulima au wachuuzi wadogo wadogo wengi mbali mbali kwa kuokoteza njiani Je hao wa wachuuzi wadogowadogo au wakulima wadogowadogo wenye tenga moja au mbili nao wanatakiwa kuwa na EFD mashine?
 
Risiti ni rahisi sana kuipata ,kama nilivyokuambia wanakatisha risiti ni hao watendaji wa vijiji. Maana watendaji wana EFD MACHINE na pia Huwa kuna mawakala wa vipimo wanazungukaga


Watendaji wa vijijini siku hizi wana EFD machine?
Tangu lini?
Je ni Wote nchini au wa mijini tu?

Unajua nature ya kazi za dereva wa masafa marefu?

Je ni rahisi kwake kutafuta mtendaji wa kijiji alipo apatiwe risiti?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…