TRA yampiga faini ya 3,500,000 dereva kisa kapakia tenga 27 za nyanya

Hujawahi kufanya biashara acha kujidanya
Nilikuwa natoa maoni tu.
Nimeshasema tangu awali pale chini kwamba maoni yangu si lazima yawe sahihi.

Kwa hivyo ukiona makosa ktk maoni yangu ni sawa tu huenda wewe upo sahihi.

Ningekushauri nawe uweke maoni yako ili wenye dhamana wayatumie kutatua changamoto iliyopo. Na wengine tujifunze kitu.
 
... "amenyimwa haki yake ya kikatiba ya kuhabarishwa na kuelimishwa"; justification ya hiyo kitu ndipo tatizo lilipo. Ni MKWEPA KODI yupi pindi akikamatwa atakubali elimu ya kodi anayo ila kafanya makusudi kuikwepa? Kila mmoja utetezi utakuwa "sijui" hata kama habari na elimu ya kodi anayo!

Ingelikuwa baada ya kuhabarishwa na kuelimishwa mwananchi anasaini mahali kwamba "nimeelewa" au anapewa cheti ingekuwa rahisi! Ila kwa kuwa always utetezi utakuwa "sikuwa na habari", hakuna namna zaidi ya kutumia ile kanuni maarufu ya kisheria "ignorance of the law excuses no one".
 
Sass mwenye gari risiti ya efd anatoa wapi?
 
Nimekuelewa.sasa ikiwa ndo zile za kusaidia Kama pale mkata?.
Maana gunia moja Mara ya mwisho nilienda walikuwa wanachukua elfu 5.
Hauoni Kama unamuuza dereva?na kusababisha madereva waanze kuogopa kutoa msaada
Hiyo risiti aliyopigwa faini,haihusiani na mzigo,,hiyo ni ya Transporter,,yaani mwenye gari kafanya biashara lazima alipe kodi,
Mwenye nyanya analipa ushuru
 
Nimekuelewa.sasa ikiwa ndo zile za kusaidia Kama pale mkata?.
Maana gunia moja Mara ya mwisho nilienda walikuwa wanachukua elfu 5.
Hauoni Kama unamuuza dereva?na kusababisha madereva waanze kuogopa kutoa msaada
Sheria tatizo haielewi mambo ya misaada ,kila Transporter lazima awe na mashine na kila akipakia mzigo sharti kutoa risiti ya EFD.
Madereva hawatembei na machine bali hutumiwa risiti kwa njia ya wasapu na boss ama kiongozi wao,like transport manager,etc,
Hivyo dreva akipakia mzigo bila taarifa ya boss wake,hawezi kuwa na risiti na akikamatwa ndo hiyo faini sasa ina apply..
 
Kama NI hivyo wanalia wengi
 
Biashara yenyewe ya nyanya
Hakuna biashara yenye risk kama nyanya
Kwanza kuoza kingine soko lenye halieleweki
Unaweza ambiwa bei ya tenga leo ni 27000
Ukafika sokoni unambiwa bei ni 15000 kwa tenga
Haya sasa nenda kawauzie wakina wakina baresa na wengine uone wakatavyo kugarazaaa .

Ova
 
Mzee,nenda kijiji chochote ndani ndani ukapakie mfano njugumawe,,utashangaa kabla fuso haijajaa mdada huyu hapa na EFD machine,anasubiria hela,yaani haina kukwepa,
Au nasema uongo nduguzanguni..?
Ndio maana tumeweza kununua ndege zetu. Na Mheshimiwa akiwatembelea kwenu, ukilia: Oooh! Mzee hatuna Kituo cha afya, jibu: "Hivi Waziri wa Fedha yupo hapa kweli?" Pembeni yake:"Nipo Mkuu". Amri: "Hebu sasa hivi idhinisha Tshs Bilioni mbili kijengwe kituo cha Afya hapa ndani ya miezi mitatu tu!! Kinyume na hapo ujitathmini kama hiyo nafasi inakutosha. Nadhani nimeeleweka". Jibu kutoka pembeni: " Umeeleweka Mkuu". Mkuu anaendelea: "Hilo limekwisha, kuna lingine?" Kimya!! Mkuu: "Jamani twendeni zetu"
 
Kama ni tenga (la mianzi) bei ni 500/= kwa tenga. Kama ni box la mbao bei ni 300/=. Japo hutegemeana na wilaya anayokatia.
NB: hiyo sio kodi, ni ushuru wa halmashauri.
 
Halafu miaka inasonga bila kutekelezwa.
Maagizo ya hivi ni mengi sana yalitolewa lakini yaliyotekelezwa sidhani kama yanafika hata asilimia 10.
 
Kama ni tenga (la mianzi) bei ni 500/= kwa tenga. Kama ni box la mbao bei ni 300/=. Japo hutegemeana na wilaya anayokatia.
NB: hiyo sio kodi, ni ushuru wa halmashauri.
Ila kiukweli hatuwezi kuishi kwa kukamua damu hadi maiti, serikali isiwe kama roboti, akili na busara zitumike!
 
Kwahiyo serikali ilivyozima mitandao ikiwemo ‘Wasapu’ ilikuwa inategemea nini hasa?
 
Nchi haina pesa hii soon TRA watapatatiwa Hadji ya jeshi usu ili wakusanye kodi kwa nguvu
 
Wewe ni mbunge wa jimbo gani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…