TRA yavunja rekodi ya makusanyo ya mwezi Desemba 2020

Mkuu upo serious, unajua kwa sasa kuna pressure kwa serikali kuhusu vijana waliohitimu vyuo kukosa ajira. Na serikali inalaumiwa kwenye hili kwa kushindwa kutoa ajira za kutosha? au mwenzetu unaishi nchi gani..
kupanga ni kuchagua AMERIKA si wajinga kufupisha umri wa ustaafu serekalini na kwenye majeshi ispokuwa tu kwa wale ambao wana utaalamu ADHIMU na wa kipekee
 
Watutangazie tuna pesa kiasi gani mpk sasa?
 
Toka vyeti feki na sekesele la watumishi hewa hiyo hela iliyookolewa sijawahi kuiona - kuwaamini CCM yataka moyo mkuu!!
Kipindi jk yupo madarakani mishahara ilikuwa bilioni 50 kwa mwezi na vyeti feki na watumishi hewa walikuwpo sasa mbona gape imekuwa kubwa sana bilion mia 60 now ila ccm janga
 
kwa source ipi ya nishati?.
 
TRA wametoa mrejesho wa mapato wa Tril.2 kwa mwezi.Tumekuwa na tabia ya kulia lia hasa wahisani wanapotishia kusitisha misaada kama ilivyotokea mwishoni mwa mwaka 2020 jumuiya ya ulaya(EU) walivyofanya.Kilio kilikuwa kikubwa. Kumbe sisi Watanzania tukijikita kwenye kufanya kazi Msaada kama ule wa EU ni Makusanyo ya mwezi mmoja..! Na kizuri hawa Watoa misaada watakuja kwetu kwa Heshima na Adabu. Tuchape Kazi
 
Mmh! Hapa mkuu, utauwa familia za watu bure lol
 
Bado upigaji upo sana TRA.Tukidhibiti kisawa sawa Trillioni 3 is a possibility.
Watumishi TRA wasio waaminifu wana-tuangusha sana,
wadhibitiwe.
Acha lawama za kipumbavu wewe. Watu wanaingia migogoro mitaani kisa makusanyo afu anatokea bwege mmoja anaanza sema sijui TRA sio waaminifu. Acha wivu wa kike, unaona kama watumishi TRA wanafaidi sio? Basi omba serikali iwashushie mishahara walipwe sawa na walimu afu pia kazi ya kukusanya kodi wapewe POLISI NA JWTZ.

KUWA NA ADABU NA WATUMISHI WA TRA. KILA SIKU MNAWASEMA WAO LKN MAKUSANYO MNAYAONA YANAPANDA HATA HAMJUI KUWA WANATOKA USIKU KAZINI KILA SIKU KUHAKIKISHA WALIPAKODI WANALIPA KWA WAKATI LKN PIA WANAPATA ELIMU SAHIHI KUHUSU KODI.
 
Sidhan kama ni. Ushaur mzur!!, money for people, or people for money. Workers ndo wanaleta Hiyo pesa, mission is about people. Unaioona b600 ni nyingi sn kwakutumia angle ipi of argument?

 
Nawapa hongera TRA ila mikakati ijumuishe maeneo mapya ambayo zamani yalionekana hayajakua ila sasa ni biashara nzuri sana.
Mchango wa sekta ya kilimo, ufugaji, uvuvi na mifugo bado upo chini mno.

Mkulima anajaza malori mazao analeta sokoni halipi hata mia. Hana TIN na haisomi.

Wavuvi waliojaa baharini, mito na maziwa kodi zao vipi? Wafugaji wa kienyeji na kisasa wapi kodi zao wanapouza mazao yao?

Kama ni hivyo ruzuku za halmashauri zipunguzwe ili wakusanye ushuru huko.

Mi naona wengi bado hawalipi kodi.

Online business. Biashara za mtandaoni zinakua sana. Kodi..TRA wanapaswa kuwa na kitengo cha biashara mtandaoni.

Tafiti za kuibua vyanzo vipya na jinsi ya kuvitoza.

Uchumu unakua bila vyanzo vipya?
 
Nimesikia hata wafuga kuku wanatakiwa walipe kodi[emoji72][emoji72]
Ni upuuzi kudharau sekta zisizo rasmi na kudhani hawapaswi kulipa kodi. Ndiyo sababu kwenye nchi ya watu zaidi ya mil. 50 kodi inalipwa na watu wasiofika mil 4. Ni kwa sababu serikalini kuna watu wenye fikra kama hizi.

Kuna mfugaji wa kuku wa mayai 400 ambaye kwa siku ana mauzo ya 12,000 * 10 = 120,000. Halipi kodi bali mwalimu mwenye mshahara wa 540,000 kwa mwezi mzima analipa kodi.

Grow up.
 
Rudi tena kwenye vyanzo vyako vya taarifa wakupe taarifa vizuri halafu ndo urudi hapa kwenye mjadala. Na usisahau kujifunza aina za vyanzo vya mapato.

Nimecheka kwa nguvu, nendeni mkawalishe wananchi wasio na uelewa wa kutosha juu ya hiyo rekodi. Na ili muwadhibitishie kuwa mmekusanya sana, jengeni yale madarasa yanayopelea haraka.
 

Huyo mwalimu aache kazi naye akauze mayai ili apate hela nyingi kama muuza mayai. Kwa taarifa yako huyo muuza mayai ananunua chakula chenye kodi, dawa zenye kodi nk.
 
Huyo mwalimu aache kazi naye akauze mayai ili apate hela nyingi kama muuza mayai. Kwa taarifa yako huyo muuza mayai ananunua chakula chenye kodi, dawa zenye kodi nk.
Kwa hizi akili fupi mtaendelea kulalamika humu mitandaoni milele. Aliyesema mwalimu aache kazi nani? Mimi ni mfugaji we jamaa. I know what I'm talking about. Kununua inputs zenye kodi hakuiondolei bidhaa yako wajibu wa kulipa kodi.

Msichojua ni kwamba sekta kama hizi zikirasimishwa zitawapunguzia mzigo watumishi ambao mzigo wa kodi waliobeba ni mzito sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…