TRA yotoa ufafanuzi wa madai ya kutengeneza mfumo wa kuingiza mizigo nchini usio halali

Nimempenda bure huyu Mtanzania mzalendo
 
Mtu aandike barua Feb ajibiwe Aug?? Mie?i 7 baadae. Hapa iko shida kubwa
 
Hongera wewe ni mzalendo sana madam, hakika hili Jipu kubwa sana trillions of money a stolen hatari sana
 
Maelezo yako ndugu Dreams LLC LLC yana make sense kwa kiasi kikubwa..

Yaani watu wanatengeneza mfumo ulio na lopeholes za kuji - corrupt ili waibe mapato..

Pia Mjomba Fujo naye kajiuliza maswali ya msingi tu.

Na maelezo yako haya yanajibu hoja zote za Mjomba Fujo..

CC: Mjomba Fujo
 
Hongera wewe ni mzalendo sana madam, hakika hili Jipu kubwa sana trillions of money a stolen hatari sana
Kwa sababu TRA inatetea msimamo wake sitashangaa wachangiaji wengi hapa ni ama wa TRA au wana uhusiano wa karibu na TRA kwa hiyo wana maslahi yanayosigana. Hoja yangu ni kuwa TRA ina wajibu wa ziada wa kulinda sheria na taratibu zake zisitumike kuathiri kusudi la Serikali,pamoja na kuwaelimisha wadau . TRA katika hoja yao inaonekana hilo suala la wafanyabiashara wadogo ambao hawawezi kujaza content haliwahusu hususan kutoa utaratibu unaofaa, madhara ya kutofuata utaratibu na wajibu wa Clearing and Forwarding Agent ambaye ni wakala wa TRA kumwakilisha TR ipasavyo.

TRA katika hoja yake hajamgusa mwakilishi wake Clearing and Forwarding Agent inakimbilia kumtuhumu mfanyabiashara ambaye aliihusisha TRA tangu mwanzoni na siyo kwamba TRA imegundua kuwa amekwepa kodi! Watanzania tunatakiwa tujue, hata katika kuchangia, wajibu wa kila Tassisi ni nini? Hili siyo suala la ushabiki. TRA ni taasisi kubwa na inatakiwa iendeshwe na mtu mwenye uelewa mpana. Hili suala lilipelekwa kwake amekaa nalo mpaka sasa linapelekwa kwa Mhe. Rais ndipo anatoa utetezi wake wakati umma unasubiri uamuzi wa Rais! Je, huu ndiyo utaratibu?

Sasa TRA inataka Rais amwambie nini Gadi? Huu utaratibu unafanya kazi ya Rais iwe ngumu sana. Sijui kama wengi mnanielewa ninachoandika. Vinginevyo naomba msamaha.
 
Cha kushangaza KIZIMKAZI yy hajui lolote na yuko majuu n stive Nyerere. Kwake hili nalo litapita bila hata kuhoji
 
Waziri wa uchukuzi ni Mzanzibar, KM wa uchukuzi ni Mzanzibar, CEO wa bandari ni mzanzibar(wote dini moja), Mwigulu anahusikaje kwenye bandari? upigaji ni mfumo ovu wa serikali nzima, kuna kuwaje na wizi na wakati hapo bandarini kuna polisi na TISS?
Kwa hiyo wa Uchukuzi ndo ana mfumo wa forodha? Hebu acha chuki na Wazanzibar.
 
Safiii
 
Waulizeni wafanya biashara wa Kariakoo kama kuna hata mmoja ana karatasi ya importation ya mali walizo nazo dukani. Mizigo yote inasafirishwa na kutolewa na GSM. Siri ndio iko hapa GSM na TRA wakanushe na hii kwani ni ya miaka yote
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…