TRA yotoa ufafanuzi wa madai ya kutengeneza mfumo wa kuingiza mizigo nchini usio halali

Yes anayetambulika na TRA ni kampuni ya usafirishaji na siyo mwenye mali (mizigo yote ya loose cargo).Hii ni hata kwenye mizigo ya ndege (Air cargo) Waybill zinakuja kwa majina ya kampuni ya usafirishaji na sio mtu mmoja mmoja,ndio mana nako unapo walipa ,bei zao zina kila kitu humo ndani.Wewe ni kufuata tu mzigo kwao.

Baadhi ya mizigo ni mizito so mtu hawezi akachukua 20 ft or 40 ft container peke yake sababu ita overweight so anapeleka kama loose cargo.Kampuni ya kusafirisha wao ndio watagawa mzigo kwenye kontena nyingi wachanganye na mzigo mwepesi ili kubalance weight.Mzigo wote unaweza ondoka siku moja lakini kwenye kontena tofauti tofauti hata tano.(kampuni zingine zinapakia hadi kontena 5 kwa siku)

Kama sio kila mtu kutoa mzigo kwa jina lake basi waruhusu documents kutoka hiz kampuni za usafirishaji zitambuliwe na goverment agency kama TRA na wengine kama Bima.
NIMEONGEA KWA UZOEFU,NDIO KAZI YANGUπŸ˜›πŸ˜›
 


Nimesikiliza clip na maelezo ya TRA . Inaonyesha ndugu yangu Bw Emmanuel ni kama ametumia kuagiza mzigo kwa kupitia Mtu au Kampuni ambapo mzigo ulifika hadi kwake bila nyaraka kwasababu haukuwa kwa jina lake.Nachokijua mtu kuagiza mizigo kwa kushare container upo kisheria kama sheria ya Tasac sasa inawezekana pia alifanya hivi ila jina la nyaraka lilikuwa kwa jina la kampuni siyo lake au mtu mwingine aliyebeba dhamana ya container. Labda tujiulize wakati anaupokea mzigo kwa nini hakuwa na nyaraka? Ilikuwaje akakubali kupokea mzigo bila nyaraka? Pili kama mzigo ulipita kwa jina la mtu mwingine huoni kama anawauzia kesi TRA kwa kutoa siri za mteja aliyeingiza mzigo kwa jina lake? Na bima watamlipaje bima hali ya kuwa mzigo haukuwa kwenye jina lake? Nadhani ndiyo maana TRA wamemuambia alete nyaraka yeye maana huwezi kuwa na mzigo huku huna nyaraka. Pia kama nilivyoona barua ya TRA kuwa hata hivo hakuna mzigo huo uliopitishwa na hiyo kampuni, ina maana jamaa alipitisha kimagendo, manaa mfumo hayupo na nyaraka hana. Inaonyesha anashida alipwe bima sasa hana ushahidi wa nyaraka bima kaona aende TRA kakuta hola hakuna ushahidi kaamua kuwaua jamaa mtandaoni ili apate huruma. Da ama kweli
 
Mkuu unategemea TRA watakubali kwamba wana makosa ili jumba bovu liwaangukie
 
Umeeleza vzr,humu watu wengi ni mbumbumbu.
 
Ndo hapo tunaposema ccm imechoka.
 
Utaratibu unaotumika kwa hayo makampuni sio mpya na wala hauna shida yoyote.

Shida wanayo TRA kushindwa kusimamia na kupelekea wachache kujikusanyia ukwasi wa kutisha.

Huko duniani huu utaratibu unafahamika kama Delivery duty paid (DDP).

Kwa maana muuzaji atabeba dhamana ya mzigo mpaka kumfikia mteja port husika huku taratibu zote za kikodi, vibali na mambo yote yakikamilishwa na muuzaji, na mzigo unapotoka unakua na nyaraka zote halali za mteja na zikiwa zimelipiwa kodi zote.

Kwa hiyo shida hapa unaweza kuona ipo kwa nani.

Kwa saiv hao wasafirishaji ndio wananeemeka zaidi na zaidi kuliko wafanyabiashara na TRA.

Faida za kurekebishwa kwa mfumo

1. TRA watakusanya kodi nyingi SANAA ambayo inavuja kwa sasa (japo ni wala rushwa wazuri πŸ˜‚ )
2. Wafanyabiashara hawatasumbuana sana na TRA watakua na nyaraka zote muhimu za kikodi hata kutoa risiti za EFD itakua sio shida tena kwao.

Kurekebishwa kwa mfumo kutakuja na maumivu yake pia
1. Bei za bidhaa zitapanda maradufu
2. Kwa wafanya biashara wengi profit margins zitapungua.
3. Kwa makampuni ya usafirishaji ya sasa wanaweza ongeza gharama zaidi ili kufidia gap litakalozibwa hivyo kupelekea gharama za bidhaa kuendelea kuwa ghali.
 
Wakati mwingine ndiomana nina support bandari apewe mwarabu.

Mtanzania hajawahi kuacha rushwa hata moto wa milele uwe unawaka live hapa duniani watu hawataacha kula rushwa.
Bandari, Mahakama, Ardhi, Police huko kote mlungula unatembea vibaya sana.
Kwahili DP World waanze kazi hata kesho
 
kuna shida gani tra kuiandikia kampuni ya bima na kusema mzigo ni wa hango?
 
Huyu jamaa sijui kama atapata msaada wowote
Amulize yule mfanyabiashara kariakoo mziki aliokutana nao

Ova
 
Kuna kitu kama hujakielezea vizuri...
Tra wameshindwa nini hapo?
Na hao kina opo wanajikusanyia vipi ukwasi ili hali mizigo inapita na ukaguz WA tra upo?

Yaani tatizo la huyu jamaa ni tatizo la wengi lakini sio tatizo mpaka upate tatizo....namaanisha nini?
Namaanisha kwetu sisi WA vibox vichache ni sawa kujikusanya na kulipiwa na agent kule nyie mje mmalizane....
Lakini Kwa sisi umenunua oven 20 let's say hata zikija 10 zikawa na heka heka kama kubondeka au hiz ups and down ndogondogo za kutoa nao mzigo sio ishu sana....
Kwa wenye mizigo mikubwa ndo ishu ikiwa tra watakukatalia documents zenye jina lako ili hali wewe hukupitiaha mzigo Kwa jina lako....ikiwemo kama umepata majanga....so Kwa jamaa ni funzo....kwamba Kila mtu apitishe mzigo Kwa documents halali....Hawa ma agent tulipane garama ya usafir.....mambo yatakayokua magumu sana
Natamani kungekua na audio nirekod...
Yaani kupitia maagent ni kurahisisha tu lakin still mizigo iaputa kwenye ukaguz WA tra ambao wanatakiwa kulipa kinachopita..
Sasa hapo sijui tra wanashida gani
 
Huyu jamaa sijui kama atapata msaada wowote
Amulize yule mfanyabiashara kariakoo mziki aliokutana nao

Ova
Kwa kesi ya jamaa wanayo wafanya biashara 90%
Mi mwenyewe nimeshtuka sana....yaani ukipata majanga huna documents za tra....wenye documents za mzigo kuingia ni kina gnm... mapembelo and co
 
Hili swala limetufungua wengi...lakin way forward ni ipi...ukizingatia loose cargo ya box 20 kweli ukapangw folen tra....nayo ni kwikwi

Hata kontena moja mkiwa Watu 10, kila mmoja anaweza kulipa kodi kivyake TRA na Mamlaka ya forodha ikamtumbua. Hizi loose cargo Hao ma agent wanafanya consolidation na kusafirisha mizigo. Wakifika hapa Bongo wanatakiwa wafanye break bulk au deconsolidation ya mzigo wote. Hapo Ile house BL ina kufa na kila mteja mwenye mzigo kwenye hiyo kontena anapewa master BL yake.

Sasa ukokotoaji wa kodi utafata invoice na packing list ya kila mteja na master BL yake. Hapo kila mteja ndani ya kontena moja mzigo wake utatambulika na TRA na kila mmoja atalipa kodi sahihi.

TRA wanajiuma Uma hapa Kwa sababu ishu hii wanaojua vizuri.. Yule msafirishaji anatengeneza invoice moja ku cover ya watu wote.. Anaweza kuficha baadhi ya bidhaa asiziweke ili alipe kodi kidogo.. Aje kumalizana na wateja wake huku awalipishe kisawa Sawa. Hapo TRA wanavuta hela kwenye verification ya mzigo.

Mfumo huu una waumbua TRA maana unainesha unawazuia kukusanya kodi sahihi. Pia hawawambii hawa transporter wafanye deconsolidation kama utaratibu ulivyo.
Kwa kesi ya huyu jamaa anajisumbua tu na nadhani ndio maana wameamua kukimbilia kutafuta huruma ya jamii.

Na kikawaida dhamana ya mzigo ipo Kwa Watu wa forodha, ambao Hao wanawatumia mawakala wa forodha katika kukusanya kodi. Mtu binafsi hauwezi kutoa mzigo wako bila kutumia wakala wa forodha.
 
Kwa mfano....nishanunua jinsi zangu china balo 10.
Nikapitishia agency wangu ambae ni opo...
Machina wangu anachonipa Mimi ni documents za malipo ya mzigo na kinachotakiwa kulipiwa kwenye email.....basi...mzigo wangu unaenda kwenye agency yangu....
Yeye anasafirisha ikifika mizigo hapa ndo ananiita nikalipie let's say dola 350...
Mimi sijui walicholipana na tra....yaani hata sielewi umepitaje pitaje na jina ni la nani...
Kesho na kesho kutwa yametokea mafuriko....natakiwa kulipiwa na bima yangu.....nikapeleka documents kule.....wakasema leta za mzigo kuingia...
Mimi naenda kudai tra....tra wanasema ahawanijui....which is true nimepitishia Kwa agent....Sasa nikirudi kusema tra wanamfumo wao WA nje ya system wanaofanya biashara hizo watanishangaaa....
Maana nafikiri ndo mfumo WA muda mrefu sana.
Lakini Kwa kuwa wanasema sheria hii ya kulipia moja Kwa moja mwenyewe ilikuepo enzi na enzi ila ikawa watu hawatilii maanani hata wenye full container...
Na je kama Kila mtu alilipia mwenyewe forodha itakuaje kulipana na ma agent hasa wakati WA kusafirisha..?
Yaani mtalipanaje....maana kuclear mwenyewe mzigo balo kumi utatumia 3 weeks....
Eeeeh haya mambo Bado Mimi mchanga Kwa kweli siwez yaeleze tuendelee tu kudeal na '"tosh"
 
Bl ni nini?

Unajua sisi tulioshia la saba c tukaamua kujiongeza na u "winga"
Mkuu ni wazi kwamba Kwa maelezo yako hapo juu wafanyabiashara wengi hawajui hizi mambo....
Mi nilikua ni ngumu mnooo....kumbe inatakiwa iandaliwe mchakato WA Kila mteja .....na invoice yake....ya kodi...
Ila Kwa upande mwingine nahis pia wafanyabiashara wanajua ila wanahis kodi itakua kubwa sana Kwa mmoja mmoja..
Na Kwa upande WA tatu nahis Hawa agent Hawa wanatengeza mazingira ya kupata kodi ndogo ili waingie kwenye soko la ushindani....as "Mimi nacharj pesa ndogo Kwa CBM" Kwa kuwa wamekua wengi...
Lakini pia na hisi hao pia wanataka kujikusanya pesa nyingi as ushuru walipe kidogo alafu wakukamue vizuri as if kalipia ushuru mkubwa...
Lakini pia la mwisho uwemda tra wanafaidika na huu mfumo....Kwa namna moja au nyingine Kwa kushirikiana na hizi agency
Ila la mwisho Kila mtu alilipia kodi yake Hawa jamaa kwenye usafiri watatutoza Malaki ya pesa
 
Kila kitu kinaweza kuwekwa vizuri, shida ni wasimamizi.

Hata hizo habari za kutoa mzigo wiki 3, muda mwingine unachagizwa na mambo ya rushwa.

Kama mifumo ipo sawa na transparent hamna janja janja yoyote itakayokwamisha kutoa mizigo kwa wakati.
 
Wafanyabiashara wanajua japo si wote.

Shida nyingine ni ukiritimba, unaweza kusafirisha mzigo wako na kampuni za kimataifa na ukafika vizuri DSM port, ila mpaka unakuja kuutoa utapigishwa kona nyingi, na sio kwamba unautoa wewe bali umempa kazi wakala akutolee, kwa ujumla hii mifumo ipo weak sana ndio maana ni wachache wananufaika sana, na inafanywa hivyo kwa maksudi kwasababu ni mitego ya watu kupiga pesa.

Kuna watu wanapata pesa mambo yakiwa yanakwama kwama tu πŸ˜‚
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…