pye Chang shen
JF-Expert Member
- Jul 11, 2016
- 11,422
- 6,108
Inaonekana na wewe hujanielewa kusudio langu, usingeandika ushuzi hapaUnaonesha video clip ya mlalamikaji hujaisikiliza, usingeongea utumbo huo.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Inaonekana na wewe hujanielewa kusudio langu, usingeandika ushuzi hapaUnaonesha video clip ya mlalamikaji hujaisikiliza, usingeongea utumbo huo.
Sijuwi kusoma mawazo ya mtu hata nijuwe kusudio lake. Mimi nakielewa nilichokisoma au kama hakieleweki ndiyo hakieleweki.Inaonekana na wewe hujanielewa kusudio langu, usingeandika ushuzi hapa
Yes anayetambulika na TRA ni kampuni ya usafirishaji na siyo mwenye mali (mizigo yote ya loose cargo).Hii ni hata kwenye mizigo ya ndege (Air cargo) Waybill zinakuja kwa majina ya kampuni ya usafirishaji na sio mtu mmoja mmoja,ndio mana nako unapo walipa ,bei zao zina kila kitu humo ndani.Wewe ni kufuata tu mzigo kwao.Hapa uko sahihi kabisa...
Mizigo mnaingiza wengi....naona hapo kaitaja Hadi kampuni ya opo agency....
Sasa ishu Iko hivi Kwa mtizamo wangu...
Kama mtu anaingiza mzigo mkubwa ni Bora mzigo aulipie kodi mwenyewe(sijui hako kamchakato ) kamekaaje.....ila nachojua mpaka Sasa watu wanaingije mizigo Hadi ya milioni 200 kupitia agency hizi...
Na hakuna aliyekua anaona Kuna umuhimu WA kuingia yeye kama yeye....na hata tra walivyosema Kila mtu alipie mwenyewe watu waliona ni usumbufu lakin ukweli ni kwamba kwenye hili janga huyu jamaa sidhan kama atapa stahiki yake...
Alafu kingine tra hawamjui....Hilo ni sahihi maana hajaingiza mzigo yeye...dah
Sasa sisi wenye vi loose cargo tufanyeje jamani....
Na je wakiusimamia mfumo WA kulipa moja Kwa moja kule SI ni wazi kwamba makadirio ya kodi yatakuja makubwa....Bado umlipe agent
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) inapenda kutoa ufafanuzi juu ya taarifa inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu malalamiko ya Bw. Emmanuel Gadi kuwa, TRA imetengeneza mfumo wa kuingiza mizigo nchini nje ya mfumo halali wa Serikali kinyume na Sheria ya Forodha.
Tunapenda kuufahamisha umma na jamii kwa ujumla kuwa, Mamlaka haina mfumo wowote mwingine inaouendesha wa kuingiza mizigo nchini nje ya mfumo wa Forodha wa TANCIS ambao unatumika kwa mujibu wa Sheria ya Usimamizi wa Forodha ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EACCMA).
Bw. Emmanuel Gadi alifikisha malalamiko yake kwa njia ya barua tarehe 27 Februari, 2023 akidai kupewa uthibitisho na TRA wa kuingiza mzigo wa vifurushi 471 vya “Toner Cartridges’’ kupitia kampuni ya Tosh Logistics Ltd. TRA ilifanya uchunguzi wa kutosha na kuthibitisha kwamba, hapakuwa na mzigo wowote ulioingizwa nchini kwa jina la Wintech Tanzania Ltd wa vifurushi 471 vya “Toner Cartridges” kupitia kadhia yenye namba TZDL-22-1382193 ya tarehe 18 Agosti 2022 kama anavyodai.
Hivyo, TRA ilimjibu mhusika kupitia barua yenye kumbukumbu namba CF 8/92/01 ya tarehe 25 Julai 2023 ikimjulisha kuwa, kutokana na kukosekana kwa ushahidi wa “House Bill of Lading” na kutoonekana kwa mzigo huo kwenye kadhia iliyowasilishwa na kampuni ya Tosh Logistics Ltd, TRA isingeweza kuthibitisha kuingizwa kwa mzigo huo nchini.
Kupitia taarifa yake aliyoitoa kwenye vyombo vya habari tumebaini kuwepo viashiria vya ukwepaji kodi kwani ni dhahiri kuwa mzigo huu uliingizwa kwa njia za magendo. TRA inamtaka mlalamikaji kuwasilisha nyaraka na uthibitisho wa kampuni yake kuingiza mzigo huo nchini mara moja ili hatua stahiki zichukuliwe.
===========
Video ya Mfanyabiashara akiituhumu TRA
Mkuu unategemea TRA watakubali kwamba wana makosa ili jumba bovu liwaangukieNimesikiliza clip na maelezo ya TRA . Inaonyesha ndugu yangu Bw Emmanuel ni kama ametumia kuagiza mzigo kwa kupitia Mtu au Kampuni ambapo mzigo ulifika hadi kwake bila nyaraka kwasababu haukuwa kwa jina lake.Nachokijua mtu kuagiza mizigo kwa kushare container upo kisheria kama sheria ya Tasac sasa inawezekana pia alifanya hivi ila jina la nyaraka lilikuwa kwa jina la kampuni siyo lake au mtu mwingine aliyebeba dhamana ya container. Labda tujiulize wakati anaupokea mzigo kwa nini hakuwa na nyaraka? Ilikuwaje akakubali kupokea mzigo bila nyaraka? Pili kama mzigo ulipita kwa jina la mtu mwingine huoni kama anawauzia kesi TRA kwa kutoa siri za mteja aliyeingiza mzigo kwa jina lake? Na bima watamlipaje bima hali ya kuwa mzigo haukuwa kwenye jina lake? Nadhani ndiyo maana TRA wamemuambia alete nyaraka yeye maana huwezi kuwa na mzigo huku huna nyaraka. Pia kama nilivyoona barua ya TRA kuwa hata hivo hakuna mzigo huo uliopitishwa na hiyo kampuni, ina maana jamaa alipitisha kimagendo, manaa mfumo hayupo na nyaraka hana. Inaonyesha anashida alipwe bima sasa hana ushahidi wa nyaraka bima kaona aende TRA kakuta hola hakuna ushahidi kaamua kuwaua jamaa mtandaoni ili apate huruma. Da ama kweli
Umeeleza vzr,humu watu wengi ni mbumbumbu.Ngoja nichanganue hili sakata kwa nilivyoelewa mimi.
Mfanyabiashara Ameingiza bidhaa zake nchini kupitia kampuni ya tosh cargo
Tosh cargo amesafirisha na kukamilisha taratibu zote za forodha na kukabishi mzigo kwa mteja wake.
Shida inaanzia hapo kwenye (Amesafirisha na kukamilisha taratibu zote za forodha)
Wakati mfanyabiashara anapelekea mzigo wake huko unapotakiwa kwenda gari ikapata ajali na kusababisha uharibifu na upotevu wa mali.
Kwakua mfanyabiashara alikua na bima, akaanza mchakato kufatilia ili apate fidia ya mali yake iliyoharibiwa na tukio la ajali.
Kampuni ya bima inawajibika kumlipa mteja wake, lakini kabla hawajamlipa lazima wapate nyaraka zote muhimu kuhusu mali zilizopotea, ikiwa ni pamoja na nyaraka zote halali za kikodi na mengineyo ili wapate uhakika wa thamani na uhalali wa wanachoenda kulipa.
Sakata linaanzia hapa kwenye nyaraka.
TRA hawatambui mali ya mlalamikaji, kwanini hawaitambui na hawajaiona kwenye mfumo?
Kuna mawili hapa;
1. Tosh cargo wameingiza mzigo kama mali yao, hivyo mteja mwenye mzigo hatambuliki na mfumo mzima wa TRA.
2. Rejea namba moja 😂, kama mfumo haukusomi basi unamsoma aliekamilisha clearance ya mzigo.
Kama Nyaraka za TRA hazikutambui kampuni ya Bima itakufidia vipi na umeshindwa kutoa vielelezo vya uhalali wa mali iliyoharibika, vipi kama umekula njama na mtu baki utumie mgongo wa mali yake iliyoharibika kujipatia bima kwa njia ya udanganyifu?
Swali jingine la msingi kwa mfanyabiashara.
Asijekua anataka huruma ilhali nayeye anajua fika changamoto ambazo zingejitokeza.
Je kabla ya kupata matatizo yote ya ajali n.k, aliridhika na nyaraka zote alizokabidhiwa baada ya kupewa mizigo yake, au akili imekuja kukaa sawa baada ya matatizo?
Ndo hapo tunaposema ccm imechoka.Huyo ni hamas, alishaamuwa kufa zamani sana. Kidume hicho hakitaki kuuliwa kibiashara huku kinatazama tu.
Si umesikia walivyomtisha?
Nnavyoijuwa Tanzania, huyo ndiyo wa kuungwa mkpo na kila Mtanzania. Wapo wengi sana wanaoonewa namna hiyo.
Na huyo godown lake lingekuwa halijawaka mto na asingetakiwa na kampuni ya bima kupeleka vielelezo, yasingejulikana kabisa hayo. Hata yeye alikuwa hafahamu, anajuwa kila kitu kinakwenda kihalali tu.
Haya sawa, ikiwa sisi tupo kwenye hatamu tumechoka, sasa nyie mnaefukuzia siku zote mkoje?Ndo hapo tunaposema ccm imechoka.
Utaratibu unaotumika kwa hayo makampuni sio mpya na wala hauna shida yoyote.Sio GSM tu na opo yake a.k.a Simba WA bahari...
Ni makampuni yote kuanzia hao kina gnm....na mapembelo
Wooote ndo wanaotambulika tra..
Watu Wana mizigo mikubwa lakin hawana documents za tra...
Ila swali langu kubwa ni mbona juzi kati tra walivyosema Kila mtu alipie mzigo wake kukawa Kuna maandamano?
Kunani?
Kwahili DP World waanze kazi hata keshoWakati mwingine ndiomana nina support bandari apewe mwarabu.
Mtanzania hajawahi kuacha rushwa hata moto wa milele uwe unawaka live hapa duniani watu hawataacha kula rushwa.
Bandari, Mahakama, Ardhi, Police huko kote mlungula unatembea vibaya sana.
kuna shida gani tra kuiandikia kampuni ya bima na kusema mzigo ni wa hango?Mizigo ya loose cargo nikuwa mizigo ya watu tofauti inakusanywa kwenye kontena moja na kampuni ya usafirishaji inasafirisha kama mali yao.Ndiyo maana unachajiwa kwa CBM na unalipa kwenye kampuni ya usafirishaji bila kwenda mwenyewe forodha.
I think baada ya TRA kupata hili zengwe la huyu jamaa wakaja na mfumo wa kila mtu alipie forodha,ambapo kwenye mgomo wa Kkoo kipindi kile watu waliupinga huu utaratibu.Maana ilikuwa let’s say kontena ina mizigo ya watu 100,kila mmoja inatakiwa akalipie ushuru forodha.
Kitu ambacho hawakujua ndio kama sasa hivi inakuwa ngumu bima kulipa bila nyaraka za uingizaji mzigo.TRA walilijua hili ila kwa kuwa walikuwa wananeemeka bila kesi wakapuuzia.
Kuna mtu atatolewa mbuzi wa kafara kwenye hili.
Kuna kitu kama hujakielezea vizuri...Utaratibu unaotumika kwa hayo makampuni sio mpya na wala hauna shida yoyote.
Shida wanayo TRA kushindwa kusimamia na kupelekea wachache kujikusanyia ukwasi wa kutisha.
Huko duniani huu utaratibu unafahamika kama Delivery duty paid (DDP).
Kwa maana muuzaji atabeba dhamana ya mzigo mpaka kumfikia mteja port husika huku taratibu zote za kikodi, vibali na mambo yote yakikamilishwa na muuzaji, na mzigo unapotoka unakua na nyaraka zote halali za mteja na zikiwa zimelipiwa kodi zote.
Kwa hiyo shida hapa unaweza kuona ipo kwa nani.
Kwa saiv hao wasafirishaji ndio wananeemeka zaidi na zaidi kuliko wafanyabiashara na TRA.
Faida za kurekebishwa kwa mfumo
1. TRA watakusanya kodi nyingi SANAA ambayo inavuja kwa sasa (japo ni wala rushwa wazuri 😂 )
2. Wafanyabiashara hawatasumbuana sana na TRA watakua na nyaraka zote muhimu za kikodi hata kutoa risiti za EFD itakua sio shida tena kwao.
Kurekebishwa kwa mfumo kutakuja na maumivu yake pia
1. Bei za bidhaa zitapanda maradufu
2. Kwa wafanya biashara wengi profit margins zitapungua.
3. Kwa makampuni ya usafirishaji ya sasa wanaweza ongeza gharama zaidi ili kufidia gap litakalozibwa hivyo kupelekea gharama za bidhaa kuendelea kuwa ghali.
Kwa kesi ya jamaa wanayo wafanya biashara 90%Huyu jamaa sijui kama atapata msaada wowote
Amulize yule mfanyabiashara kariakoo mziki aliokutana nao
Ova
Hili swala limetufungua wengi...lakin way forward ni ipi...ukizingatia loose cargo ya box 20 kweli ukapangw folen tra....nayo ni kwikwi
Kwa mfano....nishanunua jinsi zangu china balo 10.Utaratibu unaotumika kwa hayo makampuni sio mpya na wala hauna shida yoyote.
Shida wanayo TRA kushindwa kusimamia na kupelekea wachache kujikusanyia ukwasi wa kutisha.
Huko duniani huu utaratibu unafahamika kama Delivery duty paid (DDP).
Kwa maana muuzaji atabeba dhamana ya mzigo mpaka kumfikia mteja port husika huku taratibu zote za kikodi, vibali na mambo yote yakikamilishwa na muuzaji, na mzigo unapotoka unakua na nyaraka zote halali za mteja na zikiwa zimelipiwa kodi zote.
Kwa hiyo shida hapa unaweza kuona ipo kwa nani.
Kwa saiv hao wasafirishaji ndio wananeemeka zaidi na zaidi kuliko wafanyabiashara na TRA.
Faida za kurekebishwa kwa mfumo
1. TRA watakusanya kodi nyingi SANAA ambayo inavuja kwa sasa (japo ni wala rushwa wazuri 😂 )
2. Wafanyabiashara hawatasumbuana sana na TRA watakua na nyaraka zote muhimu za kikodi hata kutoa risiti za EFD itakua sio shida tena kwao.
Kurekebishwa kwa mfumo kutakuja na maumivu yake pia
1. Bei za bidhaa zitapanda maradufu
2. Kwa wafanya biashara wengi profit margins zitapungua.
3. Kwa makampuni ya usafirishaji ya sasa wanaweza ongeza gharama zaidi ili kufidia gap litakalozibwa hivyo kupelekea gharama za bidhaa kuendelea kuwa ghali.
Bl ni nini?Hata kontena moja mkiwa Watu 10, kila mmoja anaweza kulipa kodi kivyake TRA na Mamlaka ya forodha ikamtumbua. Hizi loose cargo Hao ma agent wanafanya consolidation na kusafirisha mizigo. Wakifika hapa Bongo wanatakiwa wafanye break bulk au deconsolidation ya mzigo wote. Hapo Ile house BL ina kufa na kila mteja mwenye mzigo kwenye hiyo kontena anapewa master BL yake.
Sasa ukokotoaji wa kodi utafata invoice na packing list ya kila mteja na master BL yake. Hapo kila mteja ndani ya kontena moja mzigo wake utatambulika na TRA na kila mmoja atalipa kodi sahihi.
TRA wanajiuma Uma hapa Kwa sababu ishu hii wanaojua vizuri.. Yule msafirishaji anatengeneza invoice moja ku cover ya watu wote.. Anaweza kuficha baadhi ya bidhaa asiziweke ili alipe kodi kidogo.. Aje kumalizana na wateja wake huku awalipishe kisawa Sawa. Hapo TRA wanavuta hela kwenye verification ya mzigo.
Mfumo huu una waumbua TRA maana unainesha unawazuia kukusanya kodi sahihi. Pia hawawambii hawa transporter wafanye deconsolidation kama utaratibu ulivyo.
Kwa kesi ya huyu jamaa anajisumbua tu na nadhani ndio maana wameamua kukimbilia kutafuta huruma ya jamii.
Na kikawaida dhamana ya mzigo ipo Kwa Watu wa forodha, ambao Hao wanawatumia mawakala wa forodha katika kukusanya kodi. Mtu binafsi hauwezi kutoa mzigo wako bila kutumia wakala wa forodha.
Kila kitu kinaweza kuwekwa vizuri, shida ni wasimamizi.Kwa mfano....nishanunua jinsi zangu china balo 10.
Nikapitishia agency wangu ambae ni opo...
Machina wangu anachonipa Mimi ni documents za malipo ya mzigo na kinachotakiwa kulipiwa kwenye email.....basi...mzigo wangu unaenda kwenye agency yangu....
Yeye anasafirisha ikifika mizigo hapa ndo ananiita nikalipie let's say dola 350...
Mimi sijui walicholipana na tra....yaani hata sielewi umepitaje pitaje na jina ni la nani...
Kesho na kesho kutwa yametokea mafuriko....natakiwa kulipiwa na bima yangu.....nikapeleka documents kule.....wakasema leta za mzigo kuingia...
Mimi naenda kudai tra....tra wanasema ahawanijui....which is true nimepitishia Kwa agent....Sasa nikirudi kusema tra wanamfumo wao WA nje ya system wanaofanya biashara hizo watanishangaaa....
Maana nafikiri ndo mfumo WA muda mrefu sana.
Lakini Kwa kuwa wanasema sheria hii ya kulipia moja Kwa moja mwenyewe ilikuepo enzi na enzi ila ikawa watu hawatilii maanani hata wenye full container...
Na je kama Kila mtu alilipia mwenyewe forodha itakuaje kulipana na ma agent hasa wakati WA kusafirisha..?
Yaani mtalipanaje....maana kuclear mwenyewe mzigo balo kumi utatumia 3 weeks....
Eeeeh haya mambo Bado Mimi mchanga Kwa kweli siwez yaeleze tuendelee tu kudeal na '"tosh"
Wafanyabiashara wanajua japo si wote.Bl ni nini?
Unajua sisi tulioshia la saba c tukaamua kujiongeza na u "winga"
Mkuu ni wazi kwamba Kwa maelezo yako hapo juu wafanyabiashara wengi hawajui hizi mambo....
Mi nilikua ni ngumu mnooo....kumbe inatakiwa iandaliwe mchakato WA Kila mteja .....na invoice yake....ya kodi...
Ila Kwa upande mwingine nahis pia wafanyabiashara wanajua ila wanahis kodi itakua kubwa sana Kwa mmoja mmoja..
Na Kwa upande WA tatu nahis Hawa agent Hawa wanatengeza mazingira ya kupata kodi ndogo ili waingie kwenye soko la ushindani....as "Mimi nacharj pesa ndogo Kwa CBM" Kwa kuwa wamekua wengi...
Lakini pia na hisi hao pia wanataka kujikusanya pesa nyingi as ushuru walipe kidogo alafu wakukamue vizuri as if kalipia ushuru mkubwa...
Lakini pia la mwisho uwemda tra wanafaidika na huu mfumo....Kwa namna moja au nyingine Kwa kushirikiana na hizi agency
Ila la mwisho Kila mtu alilipia kodi yake Hawa jamaa kwenye usafiri watatutoza Malaki ya pesa