Kwa sababu TRA inatetea msimamo wake sitashangaa wachangiaji wengi hapa ni ama wa TRA au wana uhusiano wa karibu na TRA kwa hiyo wana maslahi yanayosigana. Hoja yangu ni kuwa TRA ina wajibu wa ziada wa kulinda sheria na taratibu zake zisitumike kuathiri kusudi la Serikali,pamoja na kuwaelimisha wadau . TRA katika hoja yao inaonekana hilo suala la wafanyabiashara wadogo ambao hawawezi kujaza content haliwahusu hususan kutoa utaratibu unaofaa, madhara ya kutofuata utaratibu na wajibu wa Clearing and Forwarding Agent ambaye ni wakala wa TRA kumwakilisha TR ipasavyo. TRA katika hoja yake hajamgusa mwakilishi wake Clearing and Forwarding Agent inakimbilia kumtuhumu mfanyabiashara ambaye aliihusisha TRA tangu mwanzoni na siyo kwamba TRA imegundua kuwa amekwepa kodi! Watanzania tunatakiwa tujue, hata katika kuchangia, wajibu wa kila Tassisi ni nini? Hili siyo suala la ushabiki. TRA ni taasisi kubwa na inatakiwa iendeshwe na mtu mwenye uelewa mpana. Hili suala lilipelekwa kwake amekaa nalo mpaka sasa linapelekwa kwa Mhe. Rais ndipo anatoa utetezi wake wakati umma unasubiri uamuzi wa Rais! Je, huu ndiyo utaratibu? Sasa TRA inataka Rais amwambie nini Gadi? Huu utaratibu unafanya kazi ya Rais iwe ngumu sana. Sijui kama wengi mnanielewa ninachoandika. Vinginevyo naomba msamaha.