A
Anonymous
Guest
Kwa sasa kuna usumbufu mkubwa sana wa trafiki barabarani ususani maeneo ya mijini, mfano Dar es Salaam.
Sinza Makaburini kuna trafiki wanasimamisha daladala wanaweza kukusimamisha zaidi ya dakika 40 hawaangalii muda wa abiria wanaowahi kazini na kwenye shughuli nyingine.
Ukienda mbele kwenye Taa ya Sinza Mori, LATRA wameweka kambi nao wanakamata magari tena bila Polisi, usumbufu unakuwa ni mkubwa sana.
Ukienda Posta, pale Taa za Namanga Polisi Trafiki wanategesha taa ya kuingia kulia inazima haraka sana hata kabla ya magari matatu kupita basi hapo wooote ambao taa imewazimikia ghafla mnakamatwa mnapigwa faini.
Ukija kama unaenda Posta kuna Taa za pale Sarenda, nako trafiki wametega taa haiwaki njano kuonesha kuwa nyekundu inakuja bali inazima tu paaaap, inakukuta upo kwenye nyekundu basi hapo pia trafiki mbele ameshajiandaa na hawi mmoja wanakuwa zaidi ya wanne kwa sababu washa tega taa kwa hiyo hapo lazima wawapige faini.
Ukija tena pale Kambarage House, Taa za pale wametega pia hazina njano ya kukuashiria kuwa jiandae kusimama nyekundu inakuja, taa ya kijani inazima paap-paap kwenda mjini watega kwa mbele.
Kurudi Moroko watega kwa mbele hapo wanakupiga faini, trafiki ndio wanasababisha foleni huku wakitaka kupiga watu faini na hi ni lengo la kutimiza target wanazopewa za kulazimisha watu makosa imekuwa ni usumbufu sana jijini.
Pia ukipita barabara ya kutoka Ubungo hadi Kibaha mwisho wa njia nne wapo pia.
Kuanzia Kimara kwenda mbele Trafiki wanatega kamera, wanasema speed yaani 50 wakati ile barabara ni kubwa, sehemu ambayo watu wanavuka kuna taa za lazima tu utasimama.