TRC: Kulitokea hujuma katika Treni ya Mchongoko, baadhi ya waliohusika wamekamatwa

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Snapinsta.app_465004885_962535372580857_4701266904344955177_n_1080.jpg

TAARIFA KWA UMMA UZUSHI KUHUSU TRENI MCHONGOKO

Dar es Salaam, Tarehe 06 Novemba 2024.

Shirika la Reli Tanzania - TRC linautaarifu umma kupuuza taarifa potofu zinazosambazwa na watu mbalimbali kuhusu kusimama kwa Treni za EMU - Electric Multiple Unit, (Mchongoko) na changamoto za umeme.

Ukweli ni kwamba tangu kuanza kwa safari ya kwanza ya treni zinazotumia nishati ya umeme Juni 14, 2024 hakujawahi kuwa na changamoto ya umeme, tunawashukuru wenzetu wa TANESCO kwa ushirikiano mkubwa wanaoutoa.

Aidha, kilichotokea Novemba 3, 2024 na kusababisha kusimama kwa treni ya EMU kwa takribani Saa 6 ni hujuma kutokana na kukatika ama kukatwa kwa nyaya (catenary) zinazochukua umeme kutoka njia ya umeme kupeleka kwenye treni.

Shirika la Reli Tanzania linauhakikishia umma kuwa hakuna treni ya Mchongoko iliyopata hitilafu ya kiufundi.
Tayari baadhi ya wahusika wamekamatwa na hatua stahiki dhidi yao zimeshaanza kuchukuliwa ikiwemo kufikishwa kwenye vyombo husika.

Shirika linawakumbusha wananchi kuwa bado tuko kwenye kipindi cha mwaka mmoja cha matazamio, na kama changomoto zozote zinajitokeza, TRC itaujulisha umma kwa uwazi kama siku zote tunavyofanya, na taarifa rasmi mtazipata kwenye vyanzo vyetu rasmi na si vinginevyo.

TRC inawashukuru abiria kwa uvumilivu kipindi cha changamoto.

Fredy Mwanjala
Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano
 
Kwamba hawakujiandaa na uwezekano wa hizi hujuma kutokea ?

Tatizo hawa majamaa wamekuwa waongo sana hata siku wakisema ukweli ni vigumu kuwaamini...

Kwahio kama nina safari ya muhimu kuwahi sehemu nitajuaje kama hio trip ndio kuna ratiba ya kutokea hio so called hujuma... !
 
kukatika ama kukatwa kwa nyaya (catenary) zinazochukua umeme kutoka njia ya umeme kupeleka kwenye treni.

Hata nyie hamna uhakika!
 
Kwamba hawakujiandaa na uwezekano wa hizi hujuma kutokea ?

Tatizo hawa majamaa wamekuwa waongo sana hata siku wakisema ukweli ni vigumu kuwaamini...

Kwahio kama nina safari ya muhimu kuwahi sehemu nitajuaje kama hio trip ndio kuna ratiba ya kutokea hio so called hujuma... !

Na hili ndio lengo haswa la wauhujumu kama kweli wapo. Ila kama usemavyo, ukiwa muongo sana, siku utakayosema ukweli hakuna atakae kuamini. Ndipo tulipofikia.😡
 
Nilisema toka awali, Aboud na Shabibby washughulikiwe mapema, vinginevyo watatusa sana nchi hii. Route mbona zipo nyingi tu zina uhaba wa mabasi, si wapeleke huko?
Subiri huu mwaka uishe Kwanza halafu tutaanza kuona vituko just wait.
 
TRC muwe mnatoa na ratiba za siku miundombinu inahujumiwa...

Inaonekana hakuna hata utaratibu wa kufanya patrol au hata surveillance ya masaa 24 ya miundombinu...

J'3 - J'5 Hujuma ya ngedere na tumbili kupigisha shoti nyaya...
Alh - J'2 Hujuma ya wakata nyaya za umeme...
 
Hao bundi na ngedere wana tabia mbaya sana#€&-*'
 
Back
Top Bottom