Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
TAARIFA KWA UMMA UZUSHI KUHUSU TRENI MCHONGOKO
Dar es Salaam, Tarehe 06 Novemba 2024.
Shirika la Reli Tanzania - TRC linautaarifu umma kupuuza taarifa potofu zinazosambazwa na watu mbalimbali kuhusu kusimama kwa Treni za EMU - Electric Multiple Unit, (Mchongoko) na changamoto za umeme.
Ukweli ni kwamba tangu kuanza kwa safari ya kwanza ya treni zinazotumia nishati ya umeme Juni 14, 2024 hakujawahi kuwa na changamoto ya umeme, tunawashukuru wenzetu wa TANESCO kwa ushirikiano mkubwa wanaoutoa.
Aidha, kilichotokea Novemba 3, 2024 na kusababisha kusimama kwa treni ya EMU kwa takribani Saa 6 ni hujuma kutokana na kukatika ama kukatwa kwa nyaya (catenary) zinazochukua umeme kutoka njia ya umeme kupeleka kwenye treni.
Shirika la Reli Tanzania linauhakikishia umma kuwa hakuna treni ya Mchongoko iliyopata hitilafu ya kiufundi.
Tayari baadhi ya wahusika wamekamatwa na hatua stahiki dhidi yao zimeshaanza kuchukuliwa ikiwemo kufikishwa kwenye vyombo husika.
Shirika linawakumbusha wananchi kuwa bado tuko kwenye kipindi cha mwaka mmoja cha matazamio, na kama changomoto zozote zinajitokeza, TRC itaujulisha umma kwa uwazi kama siku zote tunavyofanya, na taarifa rasmi mtazipata kwenye vyanzo vyetu rasmi na si vinginevyo.
TRC inawashukuru abiria kwa uvumilivu kipindi cha changamoto.
Fredy Mwanjala
Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano