Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 12,699
- 22,598
Nimeona utendaji wa kazi na watu kutoka nchi mbalimbali, na katika uchunguzi wangu nimegundua kwamba Watanzania wengi tuna tatizo kubwa sana la tabia ya uzembe kazini, inayosababishwa na uvivu, kutojali, kutokuwa makini, au kufanya kazi ikiwa tu tunasimamiwa na bosi. Hatujui kujituma kwa hiari.
Mtanzania anaweza kupoteza muda akaacha kuangalia jambo la maana akawa anaangalia mitandao ya jamii, You tubu, anaongea na mtu kwenye simu, anatuma meseji au labda tu anapiga story na wenzake ofisini. Tabia hizi zimetupa sifa mbaya katika maeneo mengi ya kazi, kwamba Watanzania wengi ni watu ambao hatuchukulii majukumu yetu ya kazi seriously. Mara nyingi tunafanya kazi kwa mazoea, na kukitokea badiliko kidogo tu tunaharibu mambo.
Sasa katika eneo la ku-operate train za kwenda kasi za SGR, kuongeza safari hadi nane kwa siku kati ya Dar na Moro, na huenda zaidi ya nane huko mbele, hofu yangu kubwa ni uzembe ambao kuna siku tutaambiwa treni zimegongana. Kumbuka SGR yetu ni line moja na sio mbili (dual lines) ambapo kwa line moja treni zitapishana sehemu maalumu. Je, Watanzania tuna uwezo wa kuwa makini katika eneo hili jipya na kuhakikisha suala la treni za SGR kugongana halitokei, tukiwa madereva wa treni au control room ya safari za treni?
Ukiniuliza maoni yangu binafsi, nitakuambia kwa ninavyowafahamu Watanzania wenzangu, uwezekano wa kugonganisha treni za SGR upo mkubwa tu!