TRC mnazua taharuki na madaraja yenu! Kwa hili mmetukosea sana wananchi

TRC mnazua taharuki na madaraja yenu! Kwa hili mmetukosea sana wananchi

Kwahio tujiwekee wenyewe hivyo vivuko mkuu.. wakati mwingne tusikae kimya eti kwasababu hatuishi huko
*Kwahiyo vs kwahio! Bila shaka hatuwezi kujijengea wenyewe, lakini pia kulalamika tu hakutoshi. Ni mangapi tunalalamika kila siku na wanatupuuza? Point yangu ni kuwa tuchukuwe hatua kwa vitendo na siyo kulalamika. Haya unayolalamikia ni moja ya mambo mengi kabisa yanayotokana na sisi wananchi kutochukuwa hatua.
 
TRC - shirika la reli Tanzania kwakweli mmekuwa kero Kubwa sana kwasasa! Tunaheshim sana kazi mnayofanya lakini nyie hamtuheshimu WANANCHI wa Tanzania.
1. Mmeziba Barabara zoote za waenda kwa miguu, mkilazimisha watu wapite juu ya MADARAJA ambayo kiuhalisia bado hayajakamilika kujengwa. Hakuna alama ya wapita kwa miguu hakuna alama za barabarani! Hata fence juu ya MADARAJA hazijakamilika mnataka watu wadondoke wafe ndo akili iwakae sawa. Au mnataka ajali zitokee ndo mrekebishe

2. Mmeziba Njia zoote za wapita kwa miguu mnawalazimisha wapite kwenye matobo ya chini kabisa! Huu si ubinadamu Wala ustarabu mmezingua kinoooma yaani apo

3. Mmezingatia na watu wenye ulemavu au mnajifikiria nyie tu kuziba hizo njia, wajawazito je? Wazee je? Kwani nyie mnamatatizo gani mbona hamsomeki

Solution: wekeni utaratibu mzuri toweni uzio huo woote, tengenezeni Railway cross nzuri,
Tuache hayo Mambo ya kizaman bhna hata Kama treni ni jipya haimaanishi mfanye mnavyotaka

Maeneo: Majumba sita, Airport, mpaka gongo la mboto na maeneo mengine ambyo siyajui
ASANTEN
Wewe mpumbavu wa wapi? Kwahiyo unataka madaraja wakuwekee nyumbani kwako! Ulipoenda kujenga kwenye reli na kuvuka juu yake ulitegemea kuruhusiwa milele?
 
Hivyo vitobo vya chini wakati wa mvua njia ya maji, wakati wa jua njia ya watembea kwa miguu...

Mama anatosha kutuvusha
 
Suluhu ya tatizo wafanye unavyotaka wewe?

Badili tabia.
Hii nchi ni yakwetu! Na freedom of expression ipo! Kama hawataki kufanya Kama WANANCHI tunavyotaka! Jiulize watakuwa wanafanya kwaajili ya nani wamridhishe
 
Wewe mpumbavu wa wapi? Kwahiyo unataka madaraja wakuwekee nyumbani kwako! Ulipoenda kujenga kwenye reli na kuvuka juu yake ulitegemea kuruhusiwa milele?
Una ushauri mzuri japo umeuweka kweny lugha ngumu
 
Siyo "wananchi", sema mwananchi, wengine huo mpango wako hatuutaki kabisa tena.
Kwahio wewe ndo Umekuwa WANANCHI, mi ninekuwa mwananchi. Kama Legend Kama wew uko hivi sijui unatufundisha nin watoto wako madame Fox, nimekujua miaka mingi saaana. Kwann wewe uwe WANANCHI mi niwe Mwananchi
 
Wa kulaumiwa hapa ni mainjia wetu wao wanakaa masaki osterbay hawajui hadha wapatao wakazi wa huko.
Sijui walisomea wapi hivi unaziba vipi mji kwa wavu pande mbili bila kuweka vivuko vya miguu ili maisha ya wengine yaendelee.
 
Kwahiyo waruhusu mvuke popote na mfanye biashara juu ya reli kama pale Buguruni wanavyofanya, wakiona treni wanaondoa ikipita wanarudisha. Vivuko vya chini ya reli Mbagala vipo hawalalamiki, Iringa kipo Ipogolo chini ya mlima, hawalalamiki ila nyie vijana wa visungura mkipita mnasikia kizunguzungu.
Hawajaweka vivuko kwa wapita njia ukazunguka kilometers tatu ndo urudi ulipotoka so unahitaji dakika 45 kuvuka upande wa pili.
Kabla ya waya ulitumia sekunde 30 kuvuka upande wa pili.
 
Kwa kweli imekuwa kero sana. Hasa maeneo ya mjini, huko porini sina wasiwasi watatoboa tu ili wavuke kirahisi.

Kuna eneo pale Dodoma kikuyu to mkonze. Kile kipande waweke lami ama wawe wanamwaga maji kila siku. Vumbi ni hatari kwa afya za wakazi wa maeneo yale.

Sijui ni kwa nini hawapigi kelele, kuanzia watu mazingira, afya na ustawi wa jamii.
 
Madaraja waliyoweka kuvuka Yana different ya kilometers tatu each sasa hawa wakazi wa katikati watavukaje kwann hawakuweka matobo ya watu wapite chini ya reli.
Utadhani hawajaenda shule.
Treni yenyewe haipiti kila sekunde ingetosha tu kuweka mageti na mlinzi zaidi ya kupiga pesa wamejenga madaraja yasio na mvuto zaidi ya kuchafua tu mji.
Ilitakiwa madaraja ya nguzo na sio ya msingi kama haya.
Kama pesa hawana si ingeanzia pugu tu wakipata pesa ndo wajenge kuja mjini.
Mbona wanyama mbugani wamewawekea matobo kwann isiwe kwa watu mijini
Huwezi kugawa mji pande mbili bila kuacha vivuko angalau kila mita 200
 
Ni tatizo kwa wasomi wa nchi hii wanatunga sera au kuweka michoro bila kuwashirikisha watumiaji wa Michoro hio.
The same shida kwa kivuko cha stand ya maghufuli hawakujali wazee na walemavu utadhani wote wana nguvu ya kupanda juu ya daraja.
Walishindwa nini kuweka watu wapite chini gari zipite juu.
Mwanadamu hazuiliwi na uzio sio mbuzi hawajifunzi daraja la manzese na buguruni pamoja na uzio tena wa vyuma watu wamekata ili wapite.
Muwe mnasoma tabia za watz zipoje na sio kudesign michoro kwa tabia za watu wa ulaya.
 
Back
Top Bottom