Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 5,352
- 15,876
Baada ya Msanii mkongwe wa Bongo Fleva, Selemani Msindi "Afande Sele" kutoa maoni yake kuhusu ratiba ya treni ya SGR kutokea Mkoano Morogoro kuelekea Dar es Salaam. ufafanuzi umetolewa na Shirika la Reli Tanzania (SGR).
Alichokisema Afande Sele kipo hapa ~ Afande Sele: TRC mliwaza nini kuondoa ruti ya Elfu 13, 500 Asubui Morogoro-Dar na kuweka ya 50,000 ambayo wananchi wengi hawaimudu?
TAMKO LA TRC...
"Mimi ni Fredy Mwanjala, Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano cha Shirika la Reli Tanzania, kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania, Mhandisi Machibya Shiwa, napenda kutoa ufafanuzi wa tuhuma ama taarifa potoshi hizi zinazoendelea kusambaa katika mitandao ya jamii eti Shirika la Reli Tanzania limeondoa ruti ya shilingi 13,500 kutoka Morogoro kwenda Dar es Salaam baada ya hapo kuweka ruti ya shilingi 50,000. Habari hizo ama tuhuma hizo si za ukweli, ufafanuzi uko hivi.
Shirika la Reli Tanzania linapokea maoni, linapokea ushauri na mitazamo katika ubreshaji wa uendeshaji wa treni zake za umeme za SGR. Katika maboresho hayo ya ruti ndefu, kulikuwa kuna ongezeko la ruti kutoka Dodoma kwenda Dar es Salaam na Dar es Salaam kwenda Dodoma na zote zinasimama Morogoro.
Dodoma treni ilikuwa inaondoka saa 11:15 alfajiri, tukaongeza treni ya saa 1:35. Treni hiyo sasa ndiyo inasimama Morogoro saa 3:50. Treni hiyo inachukua nafasi ya ile treni iliyokuwa inaondoka Morogoro saa 3:50.
Treni hiyo ndiyo ambayo nauli yake ilikuwa 13,500. Treni hiyo imesogezwa mbele sasa inaondoka saa 8:15 hapo hapo Morogoro kwa nauli hiyo hiyo 13,500.
Kisha, kuna safari ya kurudi kutoka Dar es Salaam kwenda Morogoro ambayo inakuwa ni saa 10:30 mpaka saa 10:40 kurudi Morogoro kwa nauli ile ile ya 13,500.
Kwa hiyo treni inayotoka Dodoma saa 11:15 inayosimama hapo Morogoro saa 3 takriban na dakika 50, hiyo ndiyo nauli yake shilingi 50,000 anayoisema Afande Sele. Tunaendelea kupokea maoni, mitazamo, ushauri, hata hayo yaliyozungumzwa na Afande Sele akidai anazungumza kwa niaba ya wananchi wa Morogoro ni maoni, ni mtazamo, ana haki ya kutoa maoni, ana haki ya kuzungumza, ana haki ya kusikilizwa kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Na sisi, kwa kuwa ni shirika sikivu, tunasikia maoni ya Watanzania, tunapokea kwa ajili ya maboresho ya wakati ujao...